Fuel crisis: Serikali ifanye maamuzi magumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fuel crisis: Serikali ifanye maamuzi magumu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MWananyati, Aug 9, 2011.

 1. M

  MWananyati Senior Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli kama Hayati mwalimu alitabiri kwa uhakika kabisa kuwa serikali ikishikwa na wafanya biashara utoaji wa maamuzi utakua mgumu. Na akataka siasa itenganishwe na biashara. He was right.

  Wafanya biashara wa mafuta wameamua kwa ujeuri wao kuwatesa Watanzania. Bei kushushwa tu kidogo, bila hata kuathiri faida yao, wameona jambo hilo si sawa, na kuamua kugoma. Haijawai tokea wafanyabiashara hawa, kupinga pindi serikali inapoongeza bei ya mafuta. Tunateseka.

  Serikali tafadhali mfanye maamuzi magumu. Na kwa namna tatizo lilivyojitokeza, nategemea mtakua mmejiandaa kukabiliana na hali hii. SIFIKIRI, NA HAIINGII AKILINI KAMA KWELI SERIKALI INAYOONGOZA WATU ZAIDI YA MILIONI 40 ITAWAPIGIA MAGOTI WAFANYABIASHARA HAWA AMBAO WAMEUKOSA UTU, NA KUONESHA DHARAU YA WAZI KWA SERIKALI.

  Ni wakati wa kurekebisha sheria nyingi ili ziwabane wafanyabiashara. na hili litawezekana iwapo wafanyabiashara watakaa mbali na siasa. Wafanyabiashara wanatikisa nchi kwa kutumia migongo ya wanasiasa. Tumechoka

  Rais wetu, tafadhali huu ndio wakati wako. Fanya uamuzi sahihi kuwasaidia Watanzania, Sipendi na sitaki kuona hasira ya Watanzania ikiwaka juu yako.

  Wataalam, wanasheria saidieni tupate ufumbuzi wa haraka wa tatizo hili

  Asante
   
 2. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Serikali ipi ifanye maamuzi magumu? Hii iliyo na viongozi wenye magamba magumu?
   
 3. M

  MWananyati Senior Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  []Serikali ipi ifanye maamuzi magumu? Hii iliyo na viongozi wenye magamba magumu?[]


  Mtanzania Imara,

  Old men said, "If u cant defeat them, join them". Tumia kichwa kufikiri, hapa ni Tanzania sio Somalia. Kuna tattizo we inaonekana upo tuuu, huwazi chochote zaidi ya kusubiri ku-crash everything, sasa hili la lkwako linajenga nini zaidi ya kuleta mdororo?
   
 4. MduduWashawasha

  MduduWashawasha JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 1,568
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Tatizo la TZ maamuzi magumu yanatolewa pale labda mtu akitembea na dem wa kiongozi yaani upuuzi mtupu
   
 5. N

  NguchiroTheElde Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Jun 13, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo siyo wafanyabiashara bali ni EWURA yaani serikali. Biashara ni kipaji na taaluma. Serkali haijui kufanya biashara na kamwe haitaweza kufanya biashara kwa ufanisi. Mfupa uliomshinda Nyerere Kikwete atauweza? Nyerere aliingiza serikali katika kila biashara hadi ya kusaga mahindi na kuuza chumvi. Matokeo yake akaifilisi nchi. Au mmeshasahau hayo ya juzi juzi tu?

  EWURA imejaa wasomi lakini wengi wao ni mbumbumbu. Wamesoma hadi chuo kikuu lakini hawajui kuwa bei hupanda au kushuka kufuatana na supply na demand, kitu ambacho hata bibi yangu anakijua fika ijapokuwa hajaenda shule. Bibi yangu anajua kuwa wakati wa kuvuna mahindi bei inashuka kufuatana na bidhaa hiyo kuwa nyingi sokoni and vice versa. Sasa kama unasoma hadi chuo kikuu bila kuelewa mambo ya msingi kama haya ina maana elimu yetu ni kama ya Taliban - haieleweshi watu ukweli bali inawapumbafusha.

  Kutokana na ukweli huo kuwa serikali ikiingilia biashara inaiua basi Serikali yenyewe ilitangaza kujitoa na kuacha supply and demand iamue ni bidhaa gani zitaletwa sokoni, kwa kiasi gani na kwa bei gani. Ndivyo ilivyo katika nchi zote zenye maendeleo. Dhana ya serikali kupanga bei ya bidhaa ambazo siyo mali ya serikali ni ya kikomunisti na imekwamisha maendeleo popote ilipojaribiwa.

  Watendaji wa Serikali hii wanajua hayo fika kwani ndio walikuwa watekelezaji wa maamuzi ya Nyerere na walishuhudia madhara yake kwa wananchi na kwa nchi nzima. Labda useme wanafurahia wakiona nchi inadidimia na wananchi wake wanateseka ndiyo maana wamekuwa wakirudisha kinyemela sera haribifu za serikali kuingilia biashara kwa kutangaza "bei elekezi" huku wakilazimisha bei hizo "elekezi" zifuatwe kwa tishio la kufungiwa biashara au faini kubwa.

  Cha kusikitisha ni kuwa baadhi ya wateja wenzetu wana fikra mufilisi kama hao viongozi wa EWURA na serkali kwani wanaunga mkono wazo la serikali kufungia leseni vituo visivyouza petroli. Kama sasa hivi kituo hakiuzi petroli ndiyo kusema ukikifungia ndiyo utapata petroli? Ama kweli yule mtu aliyesema "Watanzania tunapenda kujiumiza wenyewe, yaani tuko self-destructive".

  Kama ni maamuzi magumu basi EWURA ifute agizo lake na iache hali iendelee kama ilivyokuwa kabla ya wao kuingilia soko na kulivuruga kabisa. Siyo kujitia jiwe wakati wewe ni kokoto tu.
   
 6. H

  H6MohdH6 Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shukrani kwa wachangiaji wa mada hii muhimu kwa taifa. WaTz inabidi tuzingatie ule usemi unaosema "asiyejifunza kutokana na makosa ya huko nyuma ni rahisi kuyarudia makosa hayo" Taifa lisiloweza kusahihisha makosa yake bali linayarudia rudia haliwezi kuendelea kamwe.
   
 7. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #7
  Aug 9, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,125
  Trophy Points: 280
  mkuu serikari ichuke maamuzi gani magumu? RIDHIWANI ANAMILIKI KAMPUNI YA LAKE OIL Na hawa ndo supplya wamafuta ya ikulu na kwingineko sasa maamuzi gani hayo?
  FAMILIA YA JK INANUFAIKA NA HII SHIDA YA MAFUTA, LA SIVYO ANGEKUWA AMEISHA TOA TAMKO DAY NYINGI SANA
   
Loading...