FT Kombe la Dunia 2022: Mechi ya Senegal 0-2 Uholanzi, Novemba 21, 2022

44mg44

JF-Expert Member
Jun 16, 2019
2,135
2,142
Wawakilishi hao wa Afrika wamepoteza kwa magoli 2-0 katika mchezo wa Kundi A kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2022.

Licha ya kuonesha ushindani mzuri kwa muda mrefu, #Senegal waliruhusu magoli dakika za mwisho kutoka kwa Cody Gakpo dakika ya 84 na Davy Klaassen dakika ya 90+9.

Kwa matokeo hayo Ecuador wanaongoza kundi wakiwa na pointi 3, sawa na Uholanzi huku Senegal na Qatar wakifuatia kwa kutokuwa na pointi.


=========

~ Kipindi cha pili kinaendelea, matokeo bado ni 0-0.

~ Kipindi cha pili kimeanza.

~Kipindi cha kwanza kimekamilika, matokeo ni 0-0.

Huu ni mchezo wa Kundi A, tayari mechi ya kwanza ilichezwa jana wenyeji Qatar wakiangukia pua kwa kufungwa magoli 2-0 dhidi ya Equador.

=========

Salaam! Leo Waafrika tunaanza kutupa karata yetu kwa kuanza kuvuna tulichopanda kwa miaka minne iliyopta!
• Je, kukosekana kwa Sadio Mane kutaathiri vipi timu ya Senegal?
• Hizi timu zmewahi kukutana mara ngapi na matokeo yalikuwaje?
• Mech inaanza saa ngapi kwa masaa ya huku Afrika Mashariki?
• Senegal ana asilimia ngapi ya kushinda hii mechi?
 
Salaam! Leo waafrica tunaanza kutupa karat yetu kwa kuanza kuvuna tulichopanda kwa miaka minne iliyopta!!
• Je kukosekana kwa Sadio Mane kutaathiri vip tim ya Senegal??
•Hiz timu zmewahi kukutana Mara ngap na matokeo yalikuwaje ??
•Mech inaanza saa ngap kwa masaa ya huku Africa mashariki??
• Senegal ana asilimia ngap ya kushinda hii mech ??
Nashauri ni heri ulale au ule mtori hapo kwa Mangi kuliko kujitakia kufa mapema kwa presha ya pira la Uholanzi ilihali POTENTIAL ICON "Sadio Mane" ambaye angewatoa kimaso maso Senegal hatakuwepo hadi kombe la dunia kuisha.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Ayatollah kala kichapo cha mbwa koko! Hizi takataka nyingine sijui zinafuzu vipi world cup.
 
Back
Top Bottom