Front-Running na Market Manipulation: Sababu za Hedge Funds Kushitakiwa Marekani

Front-Running na Market Manipulation: Sababu za Hedge Funds Kushitakiwa Marekani

Fbn

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
14,138
Reaction score
33,525
Soko la fedha ni lenye mtiririko mkubwa wa fedha, na mara nyingi hedge funds au mabenki makubwa hujaribu kutumia nafasi zao kupata faida. Hata hivyo, baadhi ya vitendo vinavyojulikana kama front-running na market manipulation vinapingana na sheria za Marekani, na vinaweza kusababisha kesi za kisheria zenye mabilioni ya dola.
66df4919ae4f15d384b80caf_621e6aaf965f43cf4e3bd159_How-Does-a-Hedge-Fund-Work.jpeg

Tuje kwenye utambuzi wa maana hizi mbili kwanza kabla sijawaleta kwenye mikasa yenyewe..

Front-Running ni Nini?​

LQTA5_800.jpg

- ni pale mfanyabiashara au broker anapoona kwamba oda kubwa itakuja sokoni, kisha anatangulia kuweka trade yake mwenyewe ili kufaidika na msukumo wa bei unaosababishwa na oda hiyo.mfano pale Broker anajua taasisi kubwa itauza EUR/USD lots nyingi,kabla ya oda hiyo haijaingia sokoni, broker anatangulia kuweka sell mapema.Baada ya taasisi kuu kuingia sokoni na bei kushuka, broker anaifunga sell kwa faida.

Market Manipulation​

imagesdd.jpg

-ni pale soko linapojaribiwa kusogezwa kwa makusudi ili kudanganya washiriki wengine.Mifano maarufu ambayo ufanywa ni kama

Spoofing -Kuweka oda kubwa feki upande mmoja wa soko, kisha kuziondoa haraka ili kuunda taswira ya “pressure.” Au ni mbinu ambapo mfanyabiashara huweka oda kubwa sokoni, sio kwa nia ya kweli ya kununua au kuuza, bali ili kudanganya washiriki wengine wa soko wafikirie kuna nguvu kubwa upande fulani. Mara tu bei ikihama kutokana na hiyo presha ya bandia, oda hizo huondolewa haraka kabla ya kutekelezwa.

spoofing_press_conference_board_v4.png

Pump and Dump-Kununua kwa wingi ili kusukuma bei juu, kuvutia wengine kuingia sokoni, halafu wanauza ghafla kwa faida.
pump-and-dump-in-stock-market_1-800x445.jpg

Cornering- Kudhibiti supply ya chombo fulani (mfano future contracts) ili kulazimisha wengine kununua kwa bei yao.

Kesi Halisi zilizotokea Marekani


Mnamo Mei 6, 2010, Wall Street ilishuhudia moja ya matukio ya kutisha zaidi katika historia ya masoko ya kifedha na kupewa jina “Flash Crash”. Bei za hisa na index kuu za Marekani ziliporomoka ghafla kwa dakika chache, zikapoteza zaidi ya $1 trilioni kwa thamani ya soko, kisha zikarejea tena haraka.
2010-flash-crash.jpg

Aliyepelekea haya alijulikana Navinder Singh Sarao, mfanyabiashara wa kibinafsi kutoka West London.
Sarao hakuwa tajiri mkubwa, wala hakufanyia kazi kampuni kubwa ya Wall Street. Alikuwa “day trader” wa nyumbani, akikaa kwenye kompyuta yake ndogo karibu na Heathrow. Lakini alikuwa na kitu kimoja kilichomtofautisha katika ujanja wa kutumia spoofing.
imagessssas.jpg

Sarao alitumia mbinu hii kwenye S\&P 500 E-mini futures, moja ya bidhaa muhimu zaidi sokoni la Chicago (CME). Kwa kuweka oda kubwa za uongo, alionekana kama “shark” kwenye maji, akitengeneza mawimbi ambayo wafanyabiashara wengine walivutwa nayo.

Wakati masoko tayari yalikuwa na mchanganyiko wa hofu na mauzo ya kasi, spoofing ya Sarao ilichangia presha ya chini zaidi, na kuharakisha ile kuanguka ghafla –Flash Crash.

Baada ya uchunguzi wa kina, CFTC (Commodity Futures Trading Commission) na DOJ (U.S. Department of Justice) walimfungulia mashitaka. Mnamo 2015, alikamatwa na kushtakiwa kwa udanganyifu wa soko kupitia spoofing.

Mwishowe, Sarao alikiri kosa. Mahakama ilitambua kwamba, ingawa hakusababisha peke yake ile Flash Crash (sababu zilikuwa nyingi, ikiwemo algorithms za HFT), yeye alichangia kwa kiwango kikubwa kupitia spoofing yake.
Maana ya Algorithms za HFT (High-Frequency Trading) ni programu za kielektroniki (algorithms) zinazotumiwa na mashine za kibiashara ili kufanya mauzo ya kifedha kwa kasi ya ajabu – mara nyingi ndani ya mikrosekunde (mamilioni ya sekunde).
svw.png

Mnaweza kuelewa zaidi jinsi EA :
View: https://www.youtube.com/watch?v=z4nCTdQlH8w

Kitu cha kushangaza zaidi? Licha ya kutumia mbinu hiyo kwa muda mrefu na kutengeneza mamilioni ya dola, Sarao hakuonekana kama mfanyabiashara wa kifahari – aliishi maisha ya kawaida, hata akionekana kama mtu mwenye tabia ya kujitenga kijamii.



---

Mnamo mwaka 2015, pazia kubwa liliinuliwa, na ulimwengu ukagundua kuwa hata majina makubwa ya kifedha – yale mabenki makuu yanayoheshimika zaidi – yalikuwa yakicheza mchezo mchafu kwenye soko kubwa kuliko yote kwenye Foreign Exchange (Forex).

Forex ndilo soko lenye mzunguko mkubwa zaidi duniani, zaidi ya $5 trilioni kwa siku. Moja ya vipengele muhimu sokoni humo ni kile kinachoitwa “London Fix”– bei ya kumbukumbu inayowekwa kila siku ili kusaidia wawekezaji wakubwa, makampuni, na taasisi kujua kiwango cha haki cha kubadilisha fedha.
images.jpg


Badala ya kuruhusu bei kuamuliwa kwa uhalisia wa mahitaji na usambazaji, wafanyabiashara kutoka Citibank, JPMorgan, Barclays, UBS, na wengine walijikusanya kwenye chat rooms za siri zenye majina ya ajabu kama “The Cartel” au “The Bandits’ Club.”

Humo walipanga njama kupeana taarifa za oda kubwa za wateja wao mapema.Kufanya front-running**: kuingia sokoni kabla ya oda za wateja, kisha kunufaika na harakati za bei zitakazotokea.Kupanga wakati wa kushinikiza bei juu au chini, ili “London Fix” itoke kwenye kiwango chenye manufaa kwao.

Kwa mfano: Ikiwa walijua kampuni kubwa itabadili dola bilioni kuwa euro saa 4 jioni, wangeuza au kununua kabla ya wakati huo, kisha kukamata faida kubwa, huku wateja wao wakibaki na bei isiyo ya haki.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na U.S. Department of Justice (DOJ) na Financial Conduct Authority (FCA, UK) ulifichua mchezo huu wa miaka mingi.Hapa ndo mtu unashangaa umekaanga account.

Mnamo Mei 2015, mabenki haya makubwa yalilazimishwa kulipa jumla ya $5.7 bilioni kama faini. Viongozi kadhaa wa trading walifutwa kazi, wengine wakafunguliwa mashitaka binafsi.

Hili likawa moja ya kashfa kubwa zaidi za kifedha karne hii – kwa sababu halikuwa kosa la mtu mmoja, bali mfumo mzima wa pamoja wa kupanga bei kwenye soko la dunia.

Kashfa ya FX Benchmark Manipulation ilionesha namna taasisi zinazotegemewa kulinda masoko, zinaweza kugeuka washirika wa udanganyifu. Pia ilikumbusha ulimwengu kwamba, katika soko la trilioni za dola, hata makampuni makubwa yanaweza kuangukia tamaa ya kutumia mbinu za “front-running” na “price fixing” dhidi ya wateja wao.

---


Mwishoni mwa miaka ya 2010 na kuingia 2020s, masoko ya kifedha Marekani yalizidi kutawaliwa na algorithms na bots(hizi expert zinazotengenezwa MQL4 au MQL5 kutegemea zifanye kazi kuendesha soko bila kutumia mda kuingia sokoni). Wafanyabiashara wa “prop trading” walitumia programu hizi kuingiza oda kubwa mno—oda zilizotokea kama mawimbi makubwa sokoni—lakini dakika chache baadaye zikaondolewa ghafla.

Kwa mfanyabiashara wa kawaida, ilionekana kama soko linabadilika kasi, lakini ukweli ni kwamba hizi oda zilikuwa kimitego ya kisaikolojia kuwafanya wengine wabadili mawazo ya washiriki wengine wa soko, kisha bots zikafaidika kwa upande mwingine. Hii ndiyo inaitwa spoofing.

---
1. Kesi ya Randy Chen na Tanius Technology (2020–2021)
Katika mwaka 2020, wakati dunia ilikumbwa na changamoto za COVID-19, mfanyabiashara mmoja wa California, Randy Chen, pamoja na kampuni yake Tanius Technology, walikuwa wakifanya kazi kimya kimya kwenye Treasury futures za CME.
Kwa zaidi ya miezi kadhaa, bots zao ziliweka zaidi ya oda 1,000 za uongo. Mara tu wafanyabiashara wengine walipoamini kuwa kulikuwa na mwelekeo mpya wa bei, Chen na timu yake walikuwa tayari upande wa pili, wakipata faida haraka.

Lakini CFTC ilipogundua, walikuja na ushahidi wa takwimu na “audit trail” ya kila oda. Mwisho wa siku, Chen alipigwa faini ya $150,000**, kampuni yake $600,000, na akapigwa marufuku kwa miezi 6 kuingia soko la forex.

---
2. Kesi ya HSBC USA (2012–2020, hukumu 2023)

Kwa benki kubwa kama HSBC, mtu angefikiri udhibiti wa ndani ungalikuwa mkali. Lakini kwa karibu muongo mmoja, baadhi ya wafanyabiashara wake walihusika kwenye spoofing na udanganyifu wa swaps.
Walitumia bots na oda za uongo kuathiri bei na kupata faida zisizo halali.
Wakati ukweli ulipofichuliwa, CFTC ilitoa adhabu kubwa zaidi kulipa $45 million na maagizo ya kurekebisha mifumo ya udhibiti.

---
Kesi hizi zinaonyesha vita kati ya ubunifu wa kiteknolojia na sheria za masoko Bots zilikuwa kama wachezaji wasioonekana, zikicheza mchezo wa kasi usio na huruma. Lakini CFTC, kupitia “Spoofing Task Force”, ilijifunza kuchunguza alama za vidole vya kielektroniki zinazobaki kila mara oda zinapowekwa na kufutwa.

ELIMU HII NI KWA AJILI YA WATU WA MASOKO
 
Sasa una conclude vipi kwamba tusiwekeze kabisa kuepuka wahuni wa mtandao au kuna uwwkezaji salama tuufuate?

Mimi huwa naweka kwenye ETF na individual stock chache, je huko nako tunapigwa?

Niliacha kufanya options na futures trading muda sasa.
 
Back
Top Bottom