Freemasons katika siasa na dini

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,299
3,411
Nataka kusema kwamba, Ulaya wameitawala Libya,wanajua utamu wa utajiri wake wa mafuta. Ulaya na Marekani ndiyo wenye makampuni makubwa, “Supermajors” ya mafuta hapa duniani. Utawala wa Gaddafi ulitaka kubinafsisha mafuta yote yawe kwa maslahi ya Walibya, ooh…wakamkosea Mzungu.

Freemasons wanatafuta kumiliki chumi za dunia nzima na mafuta ni ‘damu’ inayobeba uhai wa dunia na mataifa yao. Sasa, twajua kwa nini Freemasons waliingiza Libya katika Mhimili wa Uovu(The Axis of Evil) wapate kuishambulia na kumuulia mbali Gaddafi na wapinzani wa sera zao. Na kwa misingi hii hii tujue kwa nini Iran itashambuliwa na Marekani ikileta ubishi wowote. Uingereza, Ujerumani, Hispania, Ufaransa, Italia, Ureno, Uswisi hawa ni vichwa saba katika mnyama wa Ufunuo 13, ufunuo 17, Danieli 7.

Marekani, ni mwanakondoo wa Ufunuo 13:11-18 na hawa wote wanahaha kuhakikisha wanafanya kampeni kali na propaganda kupitia mashirika yao ya habari yenye nguvu duniani, kuwapaka matope watu wasiopendwa,ili wapinduliwe kijeshi na AJENDA YAO YA SIRI itekelezwe.

Katika unabii wa Biblia, katika kitabu cha Danieli 2:43 mataifa haya ya Ulaya yameoneshwa yakiwa yanabebwa na historia ya iliyokuwa Dola ya RUMI. Mataifa haya hufananishwa na vidole vya sanamu ya Nebuchadnezzar, katika sura ya Pili ya Danieli. Ni sawa na pembe 10 za mnyama wa ajabu ambaye ni Rumi katika Danieli 7:7.

Hizi dola 10 za Ulaya, zilizoinuka baada ya dola ya Rumi, zina tabia ile ya Rumi ya Washenzi wa kale(Danieli 7:24). Pembe ndogo(Danieli 7:24,25) ni nguvu isiyo mamlaka ya kisiasa ambayo ilizifukuza Ulaya tawala tatu za Wavandali, Waheruli na Ostrogoths. Nguvu hii ilianza kuitawala Dunia mwaka 538 AD. Huu ndiyo utawala uliohuishwa baadaye na utaitawala dunia nzima na kulazimisha watu kuuabudu(Danieli 7:24,25).

Utawala huu utapewa mamlaka na shetani na mawakala wake,Freemasons,Illuminati,Marekani na washirika wake wa Magharibi, wataunganisha siasa na dini, watalazimisha Mfalme aabudiwe, watakaokataa watawekewa vikwazo vya kiuchumi, watafungwa jela ama kuuliwa. Sasa, demokrasia wanayojidai kueneza iko wapi? Kama watu watalazimishwa kuabudu dini moja, wakikataa wanafungwa, mtu kwa kuwa ni mtawala anajiita Mungu(Danieli 7:25 na Ufunuo 13:1-10) ndiyo demokrasia gani hii? Utawala uliozuka baada ya dola ya Rumi kusambaratishwa na washenzi wa Kaskazini, ukafukuza dola tatu za Wavandali(mwaka 454 AD),Heruli(493 AD) na Ostrogoths(538 AD) na kuanza kutawala dunia kwa jumla ya miaka 1260.

“Pembe Ndogo” yenye macho kama mtu mwanaume, huwakilisha mamlaka itakayoongoza serikali ya Dini na Siasa- Religio-Political Power. Mtawala huyu anaitwa, ‘Mpinga Kristo’ ama Chukizo la Uharibifu lililonenwa na Nabii Danieli(Mathayo 24:15). Katika Ufunuo wa Yohana 17: 5 upo mfano wa utawala huu wenye nguvu na wa ina yake unaoandaliwa kuitawala dunia,kidini,kiuchumi,utamaduni na kila nyanja.

Yohana wa Ufunuo wa Yohana 17:5 ,katika mwaka 96 AD alioneshwa utawala huu wa mseto wa dini na siasa. Akaoneshwa Jiji liitwalo “Babeli ya Siri” likiwa limebebwa na mamlaka(mnyama) za serikali za Ulaya na Marekani. Babeli, ni Jiji la kale sana, zama za Dikteta Nebuchadnezzar, mwaka 6060 BC. Siku hizi, Babeli ni moja ya Maajabu saba ya Dunia,kutokana na utajiri wake wa dhahabu ulioporwa katika mahali walikopindua na kuua, bustani zenye kuning’inia katika kuta ndefu zenye futi za mraba 400.
1619385778207.png


Bustani hizi zilikuwa juu kutani kiasi cha futi 75 kutoka ardhini. Hii ni nchi ya Wakaldayo wa zamani waliokula nguruwe na kunywa mvinyo kwa wingi. Na kabla ya kula vyakula hivi vya kitajiri, walivitoa sadaka kwa miungu yao mikuu, Bel na Murdoch.

Danieli na vijana wenzake wa Kiebrania waligoma kula chakula hiki na pombe zilizotolewa dhabihu kwa miungu kabla ya kuliwa eti ili kumfanya mlaji awe na nguvu za miungu hii mwilini mwake! Wakasema, kula nguruwe hizi na kunywa pombe ilikuwa kujitia unajisi na chakula cha Mfalme(Danieli 1:1-8).

Babeli, mabaki yake yangalipo hata leo huko kando ya Mito miwili ya Tigris na Euphrates, mchangani-na unaweza kufika kwa treni, ni eneo la utalii siku hizi, sasa ni makao ya mashetani na ndege wachafu kama popo, bundi n.k
1619385924820.png
1619386000255.png


Jiji hili la siri hufananishwa na mwanamke, katika Ufunuo wa Yohana 17:5-9. Hata jiji la Mwanza, huitwa, “Jiji-Dada” la Wurzburgh, Ujerumani. Kumbe mji hupewa heshima ya mwanamke? Babeli wa mafumbo katika Ufunuo 17:5-9 ni Jiji la Siri, litakalobebwa na Ulaya siku za karibuni,ili kuua watu watakaokataa kumsujudia shetani na Freemasons-ndiye mtawala atakayefuata baada ya Marekani na washirika kuitiisha dunia.

Mwanamke huyu, “Babeli” ndani yake kuna waabuduo sanamu, wala nguruwe,walevi, waabudu jua na mfumo wa sayari zote, wenye imani za kuongea na mizimu(spiritualism) n.k Mwanamke huyu, amezaa watoto, anaitwa ‘MAMA WA MAKAHABA’ na machukizo ya nchi.

Katika Biblia, ukahaba ni pale watu wa Mungu wanapo anza kuungana na waabudu sanamu na miungu,ulevi, ibada ya mizimu na uongo na kuacha usafi na kicho kwa Mungu muumbaji(Hosea 1:2) ‘Uzinzi’ ni kumwacha Mungu na kuabudu sanamu na miungu(Hosea 1:2).

Mji huu Babeli, katika Ufunuo 17:3-11 unabebwa na Ulaya na Marekani, “SUPER POWERS” zenye nyuklia na uchumi mkubwa na wana sera moja. Iran watapigwa na Marekani, Israeli na Ulaya kwa sababu wakiachwa, wakawa na Nyuklia,watapinga kuibeba Babeli hii!! Mji huu Babeli wa siri una ‘Meya’ wake anajiita Mungu duniani na ahera, huwakilisha nambari 666. Mji dada wa Babeli umebeba kikombe cha ulevi wa mafundisho, ndiyo propaganda za uongo duniani ni uchafu katika imani ya kidini, Kiislam, Kiyahudi ama Kikristo.

1619386273512.png
1619386345349.png

Mji huu Babeli uliua wapinzani wake,maana ulikuwepo zamani,mwaka 538-1798 AD.Ulikoma Feburuari 10 mwaka 1798 baada ya miaka 1260 ukawa mwisho wa Dark Ages. Mwanamke huyu ambaye ni ‘Mji Dada’wa Babeli ya kale, wakati wa Nabii Yohana akiandika kitabu cha Ufunuo(mwaka 96 AD) haukuwepo, na ukafufuka toka kuzimu Feburuari 11 mwaka 1929 AD.(Ufunuo 17:8-9) Mji dada wa Babeli uko juu ya milima saba. Mji ulikoko katika vilima saba Ulaya! Tazama Ufunuo 17:9 UONE SIRI hii, na milima saba pia huwakilisha falme saba za kale, Babeli, Wamedi na Waajemi katika serikali ya mseto, Wagiriki, Rumi ya kipagani, Rumi ya Kikristo, Pembe Ndogo na Serikali Mpya duniani yenye Dini na siasa(Ufunuo 17:9-11)

1619386626880.png


Naam, Marekani na washirika wanajiandaa kuleta duniani dini mpya ya muungano wa Freemasons,Illuminati n.k Ni mfumo wa dini(system of religion) ambao ni bandia.
Bidhaa bandia(counterfeit) zinaigiza zile bidhaa halisi.Bidhaa feki hufanana na feki, lakini ubora wake ni duni na utazitambua kwa alama yake ya biashara-trade mark- kwa mfano bidhaa feki za Panasonic huitwa,Panasoanic,hukosa ubora wa Panasonic,tujihadhari! Dini counterfeit ina alama(ALAMA YA MNYAMA) mnyama ni mpinga Kristo yaani utawala bandia wa Kristo Duniani.(2Wathesalonike 2:3-4).

Mnyama yaani Mpinga Kristo ni mtawala bandia wa dunia hii(2 Thesalonike 2:3-4) Mpinga Kristo anajifanya Mkristo(1Yohana 2:18,19)Wapinga Kristo hutokea miongoni mwa wakristo, na wana tabia kama za Babeli ya zamani,ulevi, ibada ya sanamu,ulaji wa nguruwe,kiu ya utawala duniani, ibada ya jua nyota na sayari n.k Wapinga Kristo wameacha Injili na kuhubiri siasa makanisani,ili kuwapindua viongozi waliopo kote duniani-wanajidai kuhamasisha demokrasia, na hujihusisha sana na ushoga,ulawiti na ufisadi wa kiroho,ingawa wao hukazania sana watu waache ufisadi!!

Mpinga Kristo ndiye Pembe Ndogo ya Danieli 7:25 na ni mnyama wa Ufunuo 13:1-10. Mfumo wa Ibada bandia, humbeba Mpinga Kristo wa Ufunuo 13,17 Danieli 7:25 na 2Thesalonike 2:2-4.

ubarikiwe kwa kusoma

1619386573819.png
 
Wasabato majungu hayatawafikisha mbinguni. Shauri yenu
Mada fikirishi nimeikubali ,kwann usipinge kwa hoja alipoweka majungu,au maslahi yameguswa?

Isaack newton,martin luther,john knox, n.k waliposoma kitabu cha daniel na ufunuo walisema wazi wazi, kuhusu,, papacy system ,

mtu kama newton alitumia karibu miaka 42 kukichunguza kitabu cha daniel

ndio watu wa awali kusema waziwazi kuhusu papacy and illuminati

1619389045913.png
1619389083536.png


KAMSOME HUMU UTAJUA WASAATO UNAWASINGIZIA,, KUNA VICHWA VILIUSEMA UTAWALA WA ROMA
 
Mada fikirishi nimeikubali ,kwann usipinge kwa hoja alipoweka majungu,au maslahi yameguswa?

Isaack newton,martin luther,john knox, n.k waliposoma kitabu cha daniel na ufunuo walisema wazi wazi, kuhusu,, papacy system ,

mtu kama newton alitumia karibu miaka 42 kukichunguza kitabu cha daniel

ndio watu wa awali kusema waziwazi kuhusu papacy and illuminati

View attachment 1764292View attachment 1764293

KAMSOME HUMU UTAJUA WASAATO UNAWASINGIZIA,, KUNA VICHWA VILIUSEMA UTAWALA WA ROMA
nimemshangaa huyo ndugu
 
Wasabato majungu hayatawafikisha mbinguni. Shauri yenu
Hoja zenu haziwezi kusimama zenyewe bila kutaja Papa au Roman Catholic
unamjua william tyndale? unajua kwanini kanisa lako lilimchoma moto?

kafatilie

1619389798156.png



1619389823438.png
 
Jamii nyingi mno zina secret cabal, hata historia ya Afrika inaonesha hivyo....secret cabal siyo freemasons na freemasons siyo secret cabal, kuna kitu watu wapotosha au tunataka kupotoshwa ili kukipa nguvu kitu kingine.

Watu wengi huwa tunakurupuka sana kuelezea masuala tusiyoyaelewa vizuri, tunababaisha kutokana na kukosa "secret codes".Unapoandika juu ya Freemasons na kufahamu kilichopo nyuma ya freemasons tunaishia kudanganya watu na kuibua taharuki tu.
 
Mada fikirishi nimeikubali ,kwann usipinge kwa hoja alipoweka majungu,au maslahi yameguswa?

Isaack newton,martin luther,john knox, n.k waliposoma kitabu cha daniel na ufunuo walisema wazi wazi, kuhusu,, papacy system ,

mtu kama newton alitumia karibu miaka 42 kukichunguza kitabu cha daniel

ndio watu wa awali kusema waziwazi kuhusu papacy and illuminati

View attachment 1764292View attachment 1764293

KAMSOME HUMU UTAJUA WASAATO UNAWASINGIZIA,, KUNA VICHWA VILIUSEMA UTAWALA WA ROMA
So,is the papacy cabal society or freemasons?
 
Freemason ni mfumo Tu wa nguvu za Giza uliopo ulaya , huku tuna mfumo wetu wa waganga wa kienyeji, mmiliki Yule Yule kaya tofauti , na waliostarabika zaidi basi freemason wanachukua nafasi , Dunia ni ya Mungu Ila shetani ndo mkuu wa dunia hii .....
 
Hizi dini zilizoanzishwa na vikundi vya watu uchochoroni, zimejikita sana kwenye majungu.
Huwezi kuta dini kubwa kama Islamic, roman catholic zinapoteza muda kujadili iman za watu wengine
Tena hao wasabato wamejikita sana kusoma umbea wa elen G white na hadithi zake za uongo kuhusu Freeman
 
Back
Top Bottom