Freeman Mbowe njiani kuelekea Uwanja wa Taifa

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe muda mfupi ujao ataingia uwanja wa Taifa kuhudhuria mechi ya Simba na Yanga.

Kiongozi huyo ataingia uwanja wa Taifa akitokea Jijini Mbeya ambapo jana alihudhuria mechi ya Mbeya City na JKT na kukaa Jukwaa la Mbeya City ambapo timu hiyo ilishinda 1-0

Taarifa zinasema Mbowe hatakaa Jukwaa la VIP linalotumiwa na viongozi uwanja wa Taifa bali atakaa Jukwaa la wananchi wa kawaida kama alivyofanya jana Mbeya.

Jana kiongozi huyo alikataa kukaa Jukwaa kuu alipokuwa mkuu wa wilaya ya Mbeya badala yake akaenda na msururu wa msafara wake kwenye wananchi wa kawaida hali iliyosababisha uwanja mzima kumshangilia kwa mayowe ambapo mkuu wa wilaya alionyesha hali ya kukata tamaa na wasiwasi mkubwa.
 
Angalau mpira anahudhuria maana sherehe za kitaifa walisusa kabisa Chadema.
 
Kijana unamatatizo ya mtindio wa ubongo, ndio sababu huishi kuandika pumba na ushuzi himu jamvini.magamba yamekuvuruga sana.
 
asisahau kupiga picha na mfungaji wa goli la 3 la yanga
 
Angalau mpira anahudhuria maana sherehe za kitaifa walisusa kabisa Chadema.
Unazungumzia zile sherehe za mbio za kibatari cha magamba? Then mnakesha mkifanya ngono zembe na kujaza wasichana wa shule za msingi mimba? Hizo chadema na mh.mbowe hawawezi kuhudhuria hata kidogo.
 
Hii nayo ni habari ya kisiasa kweli !!!? Mod unasemaje.
 
Mbowe alitufurahisha sana wananchi wa Mbeya pale alipokuja kukaa na sisi mashabiki..! Na hatimaye Mbeya City tulishinda 1-0 Chadema yatosha
 
Unazungumzia zile sherehe za mbio za kibatari cha magamba? Then mnakesha mkifanya ngono zembe na kujaza wasichana wa shule za msingi mimba? Hizo chadema na mh.mbowe hawawezi kuhudhuria hata kidogo.

Mkuu bila hizo mbio za kibati Mwenezi wangempata wapi????
 
...

.....Weraaaaaaaaaaaa weraaaaaaaaaaaa dadek 2015 njoo haraka upesi!!!!
 
Ninafarijika sana kuwaona viongozi wa Chadema wakiwa karibu na wananchi kama hivi...!
 
Kijana unamatatizo ya mtindio wa ubongo, ndio sababu huishi kuandika pumba na ushuzi himu jamvini.magamba yamekuvuruga sana.

Ukimfuatilia huyu jamaa kwa makini utagundua lazima anavurugwa ki -elton john.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe muda mfupi ujao ataingia uwanja wa Taifa kuhudhuria mechi ya Simba na Yanga.

Kiongozi huyo ataingia uwanja wa Taifa akitokea Jijini Mbeya ambapo jana alihudhuria mechi ya Mbeya City na JKT na kukaa Jukwaa la Mbeya City ambapo timu hiyo ilishinda 1-0

Taarifa zinasema Mbowe hatakaa Jukwaa la VIP linalotumiwa na viongozi uwanja wa Taifa bali atakaa Jukwaa la wananchi wa kawaida kama alivyofanya jana Mbeya.

Jana kiongozi huyo alikataa kukaa Jukwaa kuu alipokuwa mkuu wa wilaya ya Mbeya badala yake akaenda na msururu wa msafara wake kwenye wananchi wa kawaida hali iliyosababisha uwanja mzima kumshangilia kwa mayowe ambapo mkuu wa wilaya alionyesha hali ya kukata tamaa na wasiwasi mkubwa.
Harakati za Uchaguzi ndani ya Chama chake zimeanza. Wahafidhina bwana wana mambo miaka yote alikuwa wapi au ushabiki umeanza mwaka huu tu! Ngoja Zitto aende utawasikia vijana wake wakisema anatafuta umaarufu wa kisiasa ila Mbowe aa! Kweli kunya anye Kuku akinya bata kahara. HAKUNA MWANASIASA ASIYETAFUTA UMAARUFU DUNIANI. Kila siku ni kulinda Umaarufu na kuhangaika kuuongeza. By the way yuko Timu gani??
 
Angalau mpira anahudhuria maana sherehe za kitaifa walisusa kabisa Chadema.

Hawawezi kuhudhuria kwenye sherehe za kifisadi!!!!! walioasisi hizo sherehe walikuwa la lengo zuri sana, lakini serikali ya sasa ivi imezifanya ni mtaji wa kuingiza kipato kwa kupeana tenda za maandalizi ya sherehe huku mahospitalini hakuna dawa, na mashuleni waalimu wanajinunulia chaki!!!! shame on you ZeMarcopolo with your uzalendoless comment
 
Harakati za Uchaguzi ndani ya Chama chake zimeanza. Wahafidhina bwana wana mambo miaka yote alikuwa wapi au ushabiki umeanza mwaka huu tu! Ngoja Zitto aende utawasikia vijana wake wakisema anatafuta umaarufu wa kisiasa ila Mbowe aa! Kweli kunya anye Kuku akinya bata kahara. HAKUNA MWANASIASA ASIYETAFUTA UMAARUFU DUNIANI. Kila siku ni kulinda Umaarufu na kuhangaika kuuongeza. By the way yuko Timu gani??

....unajaza server yetu.....
 
Back
Top Bottom