Freeman Mbowe mbeba maono asiyepoteza mwelekeo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Leo ni siku muhimu kwa kaka, mwenyekiti na shujaa wa kupigania uhuru wa kweli kwa nchi yetu.

FREEMAN AIKAEL MBOWE. Hii ndiyo siku aliyobatizwa. Baada ya kuzaliwa mwezi wa tisa, wazazi wake kwa ushirikiano na wadhamini wake wa ubatizo Mwl. JULIUS NYERERE (baba wa taifa) walisubiri hadi siku taifa litakuwa huru ndipo abatizwe. Kama alama ya ukombozi, wazazi wake (bilogical na wale wa ubatizo) waliamua kumpa jina "Freeman" yaani "mtu huru".

Tuseme kwa udhaifu wetu katika historia ya siasa nchini "Freeman angekuwa mtu huru katika nchi huru".

Leo tunasherekea kitu mnachokiita "uhuru" wakati wengine "wako derezani" kibaya zaidi watetezi wa haki, usawa nabuhuru wa kweli wako jela kwa kosa la kudai uhuru mkamilifu.

FREEMAN MBOWE ni nani katika ngano za uhuru wa Tanganyika na Tanzania yenyewe?

Huyu ni mtu wa pekee Tanzania. Ni zawadi tuliyopewa kama taifa. Amekubali na kubeba mzigo wa kutetea uhuru kwa mateso makubwa. Amefikisiwa kabisa ili apige magoti kwa watawala. Amenyanyaswa, ameshambuliwa mwili wake wakitaka kumuua. Lakini amesimama imara akiyaangalia maono yake ya ukombozi yaliyoujaza moyo wake. Amedharau yote ili tu aone ndoto yake ya kuifikia Tanzania yenye neema kwa watu wote inafikiwa.

Watesaji, wanyanyasaji, wanaodhulumu haki na uhuru wa wananchi na wale wanapora fursa na mali za wananchi wanasherehekea uhuru. Sherehe yao ni kufuruhia mafanikio ya kuwapumbaza wananchi ili waendelee kufaidi utukufu wa utawala wao dhalimu.

Freeman ameamua kuwa kikwazo kwao.

Freeman amechagua kuteseka licha ya kwamba kama angechagua kunyamaza angefaidi kama wao au hata zaidi.

MUNGU alitupa Freeman, mtoto ambaye anaona mbali. Kule anakotaka kutufikisha ni kwema mno. Anataka kutufikisha katika nchi ya asali na maziwa. Sisi sote tunafahamu hilo. Watesi wetu wanafahamu hilo.

Yeye anapaona pale anakotaka tufike wote kwa pamoja. Ndiyo maana moyo wale umejaa shukrani na utayari wa kubeba mateso anayoyapitia ili huo uhuru unaotakiwa kufikiwa na wote upatikane.

Tunakushukuru ee Mungu wetu wa Mbinguni kwa kutupa zawadi hii kubwa. Tunaoiona tunaanguka mbele yako kwa shukrani na woga mkubwa. Wasioiona wanabeza na wengine kupambana na mpango huu.

Tunajua Ee Baba yetu wa Mbinguni kwamba wewe umemuweka mtumwa wako huyu ili aongoze kwa mateso anayoyapitia hadi atufikishe kule ulikomaanisha wana wa nchi hii wafike.

Ni hakika kwamba lazima mpango wako utakamilika. Wanaouzuia wanafanya kazi bure maana mpango wako haujawahi kuzuiwa na mwanadamu. Tunaweza kuchelewa; lakini kufika ni lazima.

Nami kwa moyo mkunjufu ninakushukuru ee Baba Mungu wa Mbinguni, uliyeumba vinavyoonekana na vizivyoonekana kwa kutuletea tunu hii hapa duniani na kumpa nguvu ya kutuongoza tufike pale unapotaka.

Ninatumia kalamu yangu hii leo kumpelekea salaam za pongezi Freeman Mbowe katika siku yake hii ya kupata ubatizo mtakatifu wa Kikristo.

Ninamwombea kwa MUNGU ili afurahie mateso anayoyapata kwa lengo la kupigania viumbe vyote vya Mungu nchini Tanzania.

Natamani sana thawabu atakayopata MBINGUNI baada ya kumaliza kazi yake hapa duniani.

Hakika kaka yangu FREEMAN MBOWE taji yako Mbinguni inang'aa sana.

Ninaliangalia kwa shauku na tamaa kubwa gwaride la jeshi la malaika mbinguni litakalokuwa limejipanga huku na huku kukalaki utakapopokelewa na Bwana Yesu siku ile utakapoingia Mbinguni.

Kaza mwendo kaka Freeman. Mwendo bado kidogo sana tufike mwisho. Hutalipwa na yeyote hapa duniani bali subiri thawabu yako kubwa mbinguni utakapoishi na watakatifu wote milele.

Happy baptism day Freeman Aikael Mbowe.
Uko huru katika nchi isiyo huru.
 
Leo ni siku muhimu kwa kaka, mwenyekiti na shujaa wa kupigania uhuru wa kweli kwa nchi yetu

FREEMAN AIKAEL MBOWE. Hii ndiyo siku aliyobatizwa. Baada ya kuzaliwa mwezi wa tisa, wazazi wake kwa ushirikiano na wadhamini wake wa ubatizo Mwl. JULIUS NYERERE (baba wa taifa)...
Mwanahabari Huru ulipoteleaga wapi ndugu?

Anyway, it does not matter kwa sbb labda ulikuwa kwenye kifungo cha muda mrefu (long term ban) cha JF...

Personally, I happy that you're back. Karibu jukwaani tena....
 
Leo ni siku muhimu kwa kaka, mwenyekiti na shujaa wa kupigania uhuru wa kweli kwa nchi yetu

FREEMAN AIKAEL MBOWE. Hii ndiyo siku aliyobatizwa. Baada ya kuzaliwa mwezi wa tisa, wazazi wake kwa ushirikiano na wadhamini wake wa ubatizo Mwl. JULIUS NYERERE (baba wa taifa)...
Mwamba sana wa siasa huyu. Kinachonisikitisha ni kwamba anapambania majitu yasiyojielewa!
 
Leo ni siku muhimu kwa kaka, mwenyekiti na shujaa wa kupigania uhuru wa kweli kwa nchi yetu

FREEMAN AIKAEL MBOWE. Hii ndiyo siku aliyobatizwa. Baada ya kuzaliwa mwezi wa tisa, wazazi wake kwa ushirikiano na wadhamini wake wa ubatizo Mwl. JULIUS NYERERE...
Tuko pamoka ma Huyu Mwamba. Wiki Inayo Mungu anafungua Magereza na kuwaweka Huru.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom