Freeman Mbowe: Kukata tamaa ni laana, CHADEMA hakifi

Freeman Mbowe: Kukata tamaa ni laana, CHADEMA hakifi

Hivi upinzani/Chadema ikifa, Taifa litafaidika na nini? Kama kuna upinzani hali ni hii, je upinzani usipokuwepo itakuaje?

Mwendawazimu pekee ndio atakayeunga mkono juhudi za kuua upinzani.
Naunga mkono hoja, upinzani umesaidia sana kuweka speed gavana kwa jamaa na siku upinzani ukifa kabisa sijui itakuwaje
 
Ila kiuhalisi Mbowe anahitaji kukijenga Chama upya maana wanayoyafanya wabunge wake na wagombea urais ukweli ni mzungumkuti,
Kila mtu akikutana na rais ni kumsifia tu badala ya kusema maoni yao halisi na maumivu yao
Jela kunataka moyo
 
  • Thanks
Reactions: lup
Lakini kuacha kuimba ile "Hoja ya ufisadi" nayo imetuvunja sana moyo.
 
Mbowe Sasa amawatoa Wasiwasi Wanachama wa Chadema kuhusu kufa Au kutokufa Kwa Chadema Sio kushika Au kutoshika Dau

Awamu ya Tano Mafanikio makubwa ya Chadema Ni kutokufa
 
Magufuli kishawatupa vijana wa mitandaoni mnapiga miayo tu kudadeki ! unaambiwa hata zile hela za kulaza magari kwenye matawi yenu ya ccm zote kawanyang'anya , sasa hivi hawategemei tena , tegemeo lake kubwa kwa sasa ni polisi
Hahahahahahaha mkuu upo?
 
Hivi upinzani/Chadema ikifa, Taifa litafaidika na nini? Kama kuna upinzani hali ni hii, je upinzani usipokuwepo itakuaje?

Mwendawazimu pekee ndio atakayeunga mkono juhudi za kuua upinzani.
Wanaoua upinzani ni wale wanaouza vyama kukabidhi MAFISADI ya CCM.
Nadhani kuna faida wanaipata.
 
Of course kukata tamaa ni laana kwa chadema, ni lazima uwaambie hivyo ili waendelee kukulipa na kukuneemesha huko wao wakiishia mlo mmoja kwa siku, I mean nani angekataa privilege ka a hiyo?
Kweli Mkuu mlo mmoja haungalii uko chama gani..
FB_IMG_15253419355779021.jpg
FB_IMG_15255827122353464.jpg
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema madiwani 46 ambao wamejiuzulu nafasi zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanatekeleza mpango wa CCM wa kuitisha Chadema kwa kuwa jambo hilo linafanywa na CCM kwa lengo la kuwakatisha tamaa wana CHADEMA

Mbowe amesema kuwa wapo watu wanadhani kitendo cha baadhi ya madiwani kuhama CHADEMA na kwenda CCM ni kukiuwa chama hicho na kusema suala hilo haliwezi kutokea kwani madiwani wa CHADEMA nchi nzima wapo zaidi ya 1130 huku madiwani 46 ndiyo waliohama na kwenda CCM na kusema kitendo hicho kinawapa funzo katika maandalizi ya kutafuta viongozi ambao kweli wanaweza kukisimamia chama na si wale wanaotafuta fursa za kutoka kupitia uongozi.
View attachment 768939

ni Africa tu pekee kiongozi anapokitoa chama kutoka wabunge 4 na madiwani 46 mpaka wabunge 77 na wadiwani 1134 anaambiwa ajiuzulu kwa maana anakipeleka chama kubaya. Mbowe angekuwa anaongoza kampuni ningenunua shares mara mbili nilizozonazo kulingana na track record ya performance yake.
 
Mi ningejiuliza kwanza kama hiyo performance record ni sustainable au ilitokana na kura za hasira za wapambe wa MAFISADI waliouziwa chama?
2020 tutajua kama hiyo performance ni original au ya kichina.
 
Of course kukata tamaa ni laana kwa chadema, ni lazima uwaambie hivyo ili waendelee kukulipa na kukuneemesha huko wao wakiishia mlo mmoja kwa siku, I mean nani angekataa privilege ka a hiyo?
Akili yako ni finyu to the extreme. That’s all I can say.

Wakinanani “wanaokula mlo mmoja” waendelee kuilipa chadema? Au unadhani ela mnazopeleka Chato zinatoka wapi?
[HASHTAG]#jingakabisa[/HASHTAG]
 
Mi ningejiuliza kwanza kama hiyo performance record ni sustainable au ilitokana na kura za hasira za wapambe wa MAFISADI waliouziwa chama?
2020 tutajua kama hiyo performance ni original au ya kichina.
Maybe, ingawa kama wapambe wa mafisadi ni wengi kiasi hicho, basi nchi iko mashakani. Na hili suala la mafisadi Tanzania ni la aina yake. Ni kielelezo cha jinsi nchi ilivyozama kwenye tope la unafiki usiopimika. Ndio nchi pekee ambapo mafisadi wanavuma kweli kweli lakini "hawajulikani"! Manake ni kizunguzungu kwa kwenda mbele!

Imeanzishwa mahakama ya mafisadi mara ghafla tukapigwa pwagu kuwa mafisadi wameshtuka; eti wameogopa na kuacha kufisidi hivyo mahakama imekosa wateja! Ikafa kabla haijaanza kazi. Dili zote kubwa za kifisadi zinajulikana na wahusika wanafahamika lakini mara tunaambiwa haitakiwi "kuwasumbua"; ni wazee wa heshima wanatakiwa kupumzika bila bugdha!

Haya, basi hata huyo anayevumishwa kuwa fisadi mkuu aliyeko CHADEMA akamatwe na kufikishwa mahakama ya mafisadi, kimya! Badala yake tunasikia watu wakidai kupata "muujiza" wa kusalimiana naye na kumsifu kuwa ni mwanasiasa aliyekomaa; asiyetumia lugha za kuudhi kama wapinzani wengine! Halafu, baadaye sauti nyingine zinakuja na kibwagizo cha "fisadi mkuu aliyeuziwa chama". Pathetic!
 
Nimekuja hapa kuwaambia Ukonga kukata tamaa ni Laana, Kama tunapigania mageuzi tuelewe hii safari ni Ndefu, kwamba haya ya miaka 27 tuofikia leo tumepitia katika mabonde na Milima miiba na mawe kufika hapa tulipofika. Lakini bado hatujafika tunapotaka kufika tujiandae kwa pamoja tuongeze Nguvu zetu kufika katika safari yetu.

Lazima tujiandae vyema, Kazi kubwa inayofanywa na chama chama Mapinduzi ni kuwakatisha Tamaa, na jambo ambalo limefanyika hivi Karibuni ambalo limeonekana limewarudisha nyuma wanachadema wengi ni la madiwani.

Kuna watu wanasema wanachadema wananunuliwa wanaunga mkono juhudi lakini duh watu wengine ni Mizigo lakini utafanyaje wanachadema wanakata tamaa madiwani wanaisha...... Wengine wanahofu madiwani wanarudi chama kunakufa hiki chama hakifi chadema nchi nzima ina madiwani 1184 madiwani mpaka Dakika hii wameondoka ni madiwani 46.

@freemanmbowetz
Mwenyekiti wa chadema TaifaView attachment 768795
Kife mara ngapi?,Mbowe acha upuuzi!
 
Of course kukata tamaa ni laana kwa chadema, ni lazima uwaambie hivyo ili waendelee kukulipa na kukuneemesha huko wao wakiishia mlo mmoja kwa siku, I mean nani angekataa privilege ka a hiyo?
Fact
 
Back
Top Bottom