Freeman Mbowe amgomea OCD - Wananchi wakachachamaa, OCD akatoweka

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
images


Katika hatua nyingine, Mbowe alijikuta akipinga hoja ya ofisa wa polisi aliyesemekana kuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nanyumbu, alipomtaka ashuke jukwaani kwa madai kuwa muda wa kuhutubia ulikuwa umepiga.​

Ofisa huyo alimtuma mmoja wa viongozi wa Chadema amfikishie ujumbe Mbowe, kwamba alitakiwa kukatisha hotuba yake na kushuka jukwaani, ndipo Mbowe aliposema na kuhoji:

"Mimi ni Mbunge na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, OCD sikiliza usitutishe, tumetembea maelfu ya kilomita kwa ajili ya kuwaokoa Watanzania wakiwemo watoto wako…unakuja kuniambia funga mkutano?"
Kwa mujibu wa Mbowe, muda wa kuhutubia mkutano huo ulikuwa bado unampa fursa ya kuzungumza na wananchi wa Nanyumba, jimbo lililowahi kuwakilishwa na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

Hivyo, aliendelea kuhutubia na mwishowe kuuza kadi na kuorodhesha majina ya wanachama wapya, wakiwemo waliojitokeza kuyaongoza matawi ya Chadema kwa muda, kabla ya kufanyika uchaguzi baadaye mwaka huu.

Chadema ilimaliza mikutano yake ya Operesheni Okoa Kusini iliyofanyika mkoani Mtwara jana na leo wanaanza mikutano kama hiyo kwenye vijiji, kata na wilaya za mkoa wa Lindi.

 
..."Mimi ni Mbunge na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, OCD sikiliza usitutishe, tumetembea maelfu ya kilomita kwa ajili ya kuwaokoa Watanzania wakiwemo watoto wako…unakuja kuniambia funga mkutano?"...


Kaaz kweli,,,,,,dah
 
Tunawahitaji watu wenye ujasiri wa kama kina Mbowe na Dr Slaa... Mimi nafikiri umefika muda wa kutengeneza list ya viongozi hawa wa Serikali wanaopindisha sheria ili kuwabeba CCM na Mafisadi ili tuanze nao hata huku mtaani maana mizaha imekuwa mingi sana... wakati watu tunalala njaa... Hivi anamlinganisha Mbowe na nani nchi hii?
 
thubutu!!!!hawawezi ezo zama zimeisha kabisaaaaaaa,chezea nguvu ya uma,wao wenyewe wanatamani kuwa wafuasi ila ndo ivyo baba hapendi.

Hawa chadema wanaumiza sana maana viongozi wa serikali wanahofia kupoteza unga dola ikihamia Chadema?
 
Huyo OCD pia alikuwa hamaanishi, ila alitaka iandikwe angalau wakubwa wake wasikie kuwa alikuwepo na alifanya kazi.
 


..."Mimi ni Mbunge na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, OCD sikiliza usitutishe, tumetembea maelfu ya kilomita kwa ajili ya kuwaokoa Watanzania wakiwemo watoto wako…unakuja kuniambia funga mkutano?"...



OCD alikuwa anatingisha kibiriti akakuta Cha kamanda Mbowe kimejaa full full; wapigania ukombozi wa wanyonge hawatishiwi nyau; wamekwisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom