Free talk: Mwanamke shtuka!

Tatizo hili huanzia wanapokuwa shule... UTAWASIKIA... mimi nasomewa... sijihangaishi wakati ntakuja kuolewa...
 

Wanatuacha kila siku, sisi tukiwaacha basi wanasusa kila kitu. Waliosomesha wakaachwa ni wachache kuliko ambao hawakuachwa, ila wamekomaa na kuachwa tu.
 
Hahaa..

Unataka kusema kwamba tusomeshe? Manake naona unazunguuuka sana..


Mimi mwanamke wangu awe na viable bussiness idea ...namsupport in every means ...from earth to the moon and backwards..ila kusomesha binti yuko kwao never..
 

Na ni kweli umetoa gazeti


Ulipokuwa binti!!! Siku hizi umekuwa mmama?

Huwa napenda michango yako hujaa busara na hekima.
 
Ishu ni hawa wanawake wenye idea hii ni wachache..

Wazee baba ukikuta mwanamke wako ana akili za kujikwamua kiuchumi msaidie atimize ndoto yake..

Don' t let her down..


espy na Heaven Sent nawatakia usiku mwema.View attachment 805531
Unfortunately wanaume ndo wa kwanza kuua ndoto zetu. Mara sitaki msomi, sijui mfanyakazi sijui nani mweeh, eti mnaogopa mwanamke mwenye kipato huwezi kumcontrol tofauti na asiye na kipato ambaye utamtreat utakavyo na haondoki ng'oooo. An inferior, weak and abusive man, lazima ahofie mwanamke mwenye kipato kwa sababu wengi wakiwa abused; sio wa enzi za mama zetu za kuhofia nikiondoka ntaendaje kuanza maisha (sio kiburi ila kuna muda unaona kabisa hapa tulipofikia mmh). Utegemezi unanunua hadi utu wako sometimes, mtu anakuabuse weee ila upo tu unajivumilisha hadi yakupate makubwa. Respect and treat well your woman uone kama mwanamke mwenye akili ataondoka akuache
 
Kuna ujinga fulani huwa wanajazana hivyo wanajikuta badala ya kutengeneza wanaharibu.
 
Hahaa..

Unataka kusema kwamba tusomeshe? Manake naona unazunguuuka sana..


Mimi mwanamke wangu awe na viable bussiness idea ...namsupport in every means ...from earth to the moon and backwards..ila kusomesha binti yuko kwao never..
Financial support sio lazima kusomesha bana.
. Kuna business ambazo unaweza ukamsupport baby ukajikuta umetoa kiasi kinachotosha kumsomesha mtu kabisa teh
 
Kuna ujinga fulani huwa wanajazana hivyo wanajikuta badala ya kutengeneza wanaharibu.
Teh tumewashtukia mbona, watapata tabu sana kama wataendelea kuona ni sawa kutomtreat vyema mkeo na yeye anatakiwa aendelee tu kujivumilisha
 
Ila ukipata mwanaume anayekuheshimu na akakupa support to the maximum mpe haki ya kuenjoy the superiority as a MAN.

Kosa ni pale dharau, ignoring nyingi zinapoanza...! Kuna wanawake hawajielewagi ...lazima tabu ziinuke.

Na shwatan alivyo mbaya..! Everything goes down in a friction of second.

Mtupe heshima pia pale tunapokuwa wa kwanza kuwasupport.
 
Umenena vyema Espy, kwa kweli ni wanawake wachache sana kwasasa wanaofikiria maendeleo kwa jitihada zao wenyewe pasipo kuwepo mkono wa mwanaume.

Unakuta dada kaajiriwa (binafsi/serikali) na ana muda hata wa zaidi ya miaka mitatu kazini lakini hana lolote alilowekeza zaidi ya kuhangaika na fashion kila siku... Wengi hatukumbuki kuwa nafasi na muda tulionao sasa baadaye tunaweza tusiupate, nyakati zinabadilika uchumi nao unakuwa sio rafiki.. Siku utakayoingiwa na akili ya kufanya kitu angalau kikaonekana cha manufaa kwako na kwa yeyote ajaye (mume/watoto) ndo utakapo ng'amua kuwa huna tena uwezo wa kufanya hivyo na ndipo itabaki tu simulizi kuwa yule dada enzi zake alikuwa yuko vizuri kiuchumi...Muda huo akili unayo lakini huna vitendea kazi.

Mambo mengine tuwe tunayaacha yanatupita, si lazima kuyumbishwa na dunia, kushoto upo, huku upo , kule upo yaani kila kinachokuja umo....

Tujaribu pia kuangalia na aina ya marafiki wa kuambatana nao, wao kila siku wazungumzia fashion mpya tu na kutambiana madanga, wafikiri lini utapata wazo la kusema uinvest kwenye kitu cha maana???

Nimewahi kuwa na rafiki, alinizidi kwa umri (miaka 6) lakini sioni alichokuwa akinifaidisha zaidi ya kunipa stori tu za kupelekana maduka ya mikoba + nguo + viatu + stori za madanga aliyonayo...

Nikimshauri mawazo mazuri utasikia maisha yenyewe hayaeleweki, tutumie....Nikaona hili BOX halinifai...

*Kama una uwezo na nafasi ya kufanya kitu fanya, huyo mume endapo utajaaliwa aje akute angalau una pa kuegemea...Mkiunganisha nguvu pamoja angalau mnakuwa mmejisogeza sogeza....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…