Free talk: Mwanamke shtuka!

Ndo aina ya wanawake mnaowataka lakini, anakaa tu home anadaka kwako. Ndo wazuri hao, hata unyanyase vipi atajivumilisha tu
Hamna bhana, wapo wanaofanya kazi lakini bado kwenye majukumu anakutwisha yote, akijitahidi anaweza tu kujigharamia saluni na kuvaa mwenyewe basi, ila napo mwanaume usipokuwa ngangari bado na hayo utatwishwa. Hapo bado sijagusia kumuwekea mafuta kwenye gari plus matengenezo yake, khaaa nyie viumbe nyiee loh!!
 
Hamna bhana, wapo wanaofanya kazi lakini bado kwenye majukumu anakutwisha yote, akijitahidi anaweza tu kujigharamia saluni na kuvaa mwenyewe basi, ila napo mwanaume usipokuwa ngangari bado na hayo utatwishwa. Hapo bado sijagusia kumuwekea mafuta kwenye gari plus matengenezo yake, khaaa nyie viumbe nyiee loh!!
Sasa brod tuseme tangu mnadate hukugundua kuwa baby ako ni slay queen? Hawajifichagi ujue wanaomaintain status zao
 
Habari wana MMU.

Kuna hili jambo ningependa tujadiliane ama tushirikishane kidogo.

Hakuna asiejua kuwa kila mwanamke kabla hatujavurugwa na dunia huwa matamanio yetu ni siku moja kuolewa na kutengeneza familia na mwanaume fulani hivi amazing(fantancy vs reality).

Sasa tatizo linakuja kuwa huwa wanawake wengi wana mentality kuwa maandalizi ya familia ya baadae haswa kwa mambo yanayohusu assets na gharama zingine ni majukumu ya mwanaume na sio mwanamke.
Hivyo unaweza kukuta binti ana kazi nzuri tu ila hata kujiwekeza kununua hata kiwanja walaaa hawazi au hata kufungua biashara. Anawekeza kwenye mikoba,mawigi,simu za bei ghali,viatu nk. Vitu ambavyo ukivipigia mahesabu unakuta ana viwanja vitano vikubwa tu huku kijijini kwetu.

Hebu fikiria unaolewa ukiwa angalau umejiwekeza kiasi fulani hivyo mkiunganisha nguvu na mwenza wako angalau mnapiga hatua kadhaa kwa haraka kuliko kusubiria mwanaume afanye kila kitu.

Wakati mwingine unakuta binti anadate mwanaume mwenye expossure ya kutosha na mfanyabiashara mzuri, hata kuomba basi hata aelekezwe abc's za biashara, hata kuunganishwa kibiashara nehiiii.

Au unadate mwanaume mwenye uwezo mkubwa kifedha hivyo kazi yake ni kuomba kununuliwa simu ya milioni 2 nk, vitu vya anasa ambavyo kwa kiasi kikubwa havikuongezei lolote la maana zaidi ya sifa za kijinga. Ni kwanini usimuombe mtu wa aina hiyo hata business idea, au angalau uanze jambo lako ie biashara,ujenzi nk kisha umuombe akuongezee kiasi fulani cha pesa? Kwa mwanaume mwenye upeo atakuona una akili na anaweza kukusogeza mahali pazuri.

Mwingine unakuta ni mama kabisa ila hata haiwazii kesho ya mtoto wake ambae anamlea peke yake, yuko busy na starehe na kutumbua pesa za child support, kesho na keshokutwa baba hayupo mtu anaanza kuhaha wakati nafasi ilikuwepo akaichezea

Maisha yamebadilika sana jamani basi nasi wanawake tubadilike in a positive way, tuyaishi maisha halisi na sio ya kuigiza ili angalau tunapoingia kwenye maisha ya ndoa angalau tuwe na cha kuongeza sio ndio ukiolewa umtwishe mwanaume majukumu ya familia mnayoijenga,familia ya kwao na ya kwenu pia. No wonder wanakufa mapema hawa watu.

Tuzitumie fursa vizuri pale zinapopatikana kabla haijawa too late.

Jamani hapa simchagulii mtu maisha ila hakikisha hautokuwa na majuto baadae kuwa "laiti ningejua"!!! Maana hakuna anaependa kesho yake iwe ya kuunga unga.

Nawasilisha.


Clap!, Clap!
 
Noo...you took me wrong..

Huwezi kucompare sex na kumsomesha mtu...afu pia ujue Sex kuna mutual pleasure..kuna mutual benefit..

Sex kwani naenjoy mimi peke yangu..?

Vaa viatu vya mwanaume hebu;

Unapewa kitobo kweli, umesomesha mtu miaka 3 ama 4..kamaliza unataka kujenga nae future anakuja jamaa from nowhere binti bila kujali anasepa na msela mwingine..real..?

Sasa hapo ndio unajua kuwa uliingilia wajibu wa mtu..

Mimi hili nimeliona kwa macho yangu kwa marafiki zangu..! Wala sikusoma story..! I will never do it.
Kusomesha kwa ajili ya kitobo ni hatari sana.
 
Have ma" like babe-girl

Unajua nini umesema maneno maziiito mno mwenye kusikia na asikie,.japo KUPANGA NI KUCHAGUA hatuingiliani lifestyles lakini penye ukweli lazima tukumbushane...
Yeremia 17:5-8 ukisoma utaona mtu anaye mtegemea mwanadamu anakuwaje...
Mungu akatubariki sawasawa na utajiri wake,kusukwa-sukwa hata kumwagika...!!!!


Wewe mdada una akili sana, wanawake wenye mawazo kama haya hawazidi hata 0.5%. wenyewe wanawekeza ktk vitu ambavyo si assets( Income generating investments), badala yake wanawekeza ktk liabilities.
Bravo. Nimekupenda bure.
 
Back
Top Bottom