Free style Battle thread

Free style Battle thread

naona makanjanja mnatamba,
mmesahau ka tupo mababa,
kila mmoja ajiona ye mwamba,
game ya watoto,nmekaa pemben mwamba,
utunzi mwepesi nawakusanya kama pamba...
 
ghetto gani ghetto lenyewe la kishamba/
kuanzia godoro hadi mashuka ni ya mtumba/
ghetto lipo porini huko mnapaita kibamba/
acha fiksi huwezi nifunga kamba/

unamchamba au unajamba/

kujisifia gheto hizo ni swagga za kishamba/

shy land sisi tunajisifia mashamba/

mashamba yananifanya kila siku mi natamba/
 
unamchamba au unajamba/

kujisifia gheto hizo ni swagga za kishamba/

shy land sisi tunajisifia mashamba/

mashamba yananifanya kila siku mi natamba/

mkulima umedandia treni kwa mbele nitakugonga/
nina vina vingi zaidi ya mlima kitonga/
usilete usharobaro ugali nitasonga/
chunga kijana punguza kuchonga/
sieleweki utasema umekutana na kinyonga/
 
sisemi mmejitahidi...ila nasema mmetisha,

japo sipo kwenye mood....ila mmenidatisha,

kwa hii yenu speed...Kiukweli mmenikosha,

mnaonaje kwenye hii thread...wana Hip_hop tukakesha?
 
Back
Top Bottom