Fredrick Mwakalebela kufikishwa mahakamani?

Fredrick Mwakalebela kufikishwa mahakamani?

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,352
frederick-mwakalebela.jpg

Frederick Mwakalebela
​

ALIYEKUWA KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela amefunguliwa kesi No OB/RB/16369/2014 katika kituo cha Polisi cha Oysterbay cha jijini Dar es Salaam.

Mwakalebela ambaye pia ni Kamanda wa UVCCM Manispaa ya Iringa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM, alifunguliwa kesi hiyo juzi na atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa kujibu tuhuma zilizoko mbele yake.

Taarifa za awali kutoka katika kituo hicho zinasema Agosti 23, 2011 Mwakalebela alisaini mkataba na Abdi Kassim wa kumuuzia nyumba iliyopo Kiwanja Na 25 Mivumoni Wazo Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa Sh Milioni 30.

Taarifa hiyo inaonesha Abdi Kassim aliyenunua nyumba hiyo kwa niaba ya mtoto wake Kassim Abdi Kassim alifanya malipo hayo kwa awamu mbili tofauti kwa makubaliano kwamba baada ya malipo hayo alitakiwa kupata nyaraka zote zinazohusiana na nyumba hiyo ikiwemo hati halali ya umiliki.

Pamoja na malipo hayo kukamilishwa taarifa hiyo inasema, Mwakalebela alishindwa kumkabidhi Abdi Kassim nyaraka hizo na baadaye ikagundulika kwamba nyaraka za nyumba hiyo zilitumika kupata mkopo mwingine benki.

Pamoja na kupewa siku 14 kutoka Agosti 25 awe amewasilisha nyaraka hizo kwa Abdi Kassim, bado zoezi hilo halikufanikiwa na ndipo alipofunguliwa kesi hiyo.

Mwakalebela mwenyewe amekuwa akitafutwa mara kwa mara kuzungumzia tuhuma hizo bila mafanikio yoyote.

Hata hivyo taarifa kutoka katika pande mbili hizo zinaonesha kwamba, suala hilo linaweza kuondolewa mahakamani kama mlalamikaji atapata haki yake.

Taarifa zaidi zinaonesha kwamba Abdi Kassim amefanya mahojiano na moja ya kituo cha redio nchini na kuzungumzia suala hilo kwa kina.

FrancisGodwinBlog
 
huyu si ndio alikuwa na kesi ya rushwa uchaguzi wa kupata mwakilishi(ccm) ubunge 2010??
 
caveat emptor /ˈɛmptɔː/

noun

the principle that the buyer alone is responsible for checking the quality and suitability of goods before a purchase is made.

"caveat emptor still applies when you are buying your house"
 
buyer be aware...naona uchaguzi mkuu ukija na mbwembwe zake
 
hahahaaa,watamwoneaje mkuu?

si unajua watu wanene wanaonekana wazembe wazembe na huko Jela inasemekana kuna mambo ya kuoneana oneana kama boarding schools za kizamani tha nadhani ndo jamaa anahofia hiyo kitu
 
kama ni CCM, tutarajie kuundwa tume ya kuchunguza ukweli wa jambo hilo, na matokeo ya tume hiyo ni baada ya miaka 50.
 
Back
Top Bottom