Wanajamvi,
Mimi nilikuwa mfanyakazi wa alphatel mwaka 2001. Kwa kifupi, kuna alphatel ambaye mmili ni fred Lowassa na shivacom ambayo mmiliki ni Rostam Azizi.
Kampuni ya pili ni Integrated Property Limited, wale waliovunja hile nyumba ya sanaa na kujenga majengo yao mawili pale. Rostam na Freddy ni wamiliki wa kampuni hii.
Barare Ltd, wao wanamiliki hoteli ya kitalii huko Mbuzi mawe Serengeti pamoja na shamba la hekari 1950 hapo kigamboni, isitoshe wanamiliki pia hotel tano zanzibar.
Fred ni best friend wa Masha, na wapigaji wa ukweli wote wanaweka vikao pale 777 kwa Mlatie ili wapige pesa ndefuuu.
Mke wa Fred anamiliki shares 30% pale Hyatt Hotel.
Familia hii ina utajiri wa kutupwa, sijui wenzetu walitutangulia lini?
Fred ana kadigrii kamoja, mke wake ni form 6, wana watoto wanne, mmoja kwa bahati mbaya ana matatizo ya ubongo(coincidence, uchawi?? i don't know)
Swali langu:
Hii familia imepataje utajiri wa kutupwa hivi, achana na nyumba Uk, Sweden na Malta
Tuache kudakia mambo ya familia ambayo hatuyajui vizuri.
Fred ni personal friend wangu. Tunajuana kuanzia tukiwa na miaka 10.
Kwenye maisha mahusiano ni muhimu sana. Lowassa amekuwa rafiki wa watu ambao wamefanikiwa na wenyewe walikuwa wanampenda. Rostam kama alivyosema ni kama ndugu na alikuwa kati ya wamiliki wa Voda. Hivyo kama kuna tender za kibiashara kwanini usiwape marafiki zako tena kama wana uwezo wa kufanya kazi. Sisi wa Kaskazini hata kama familia ina uwezo hatutegemei kukaa kama wenzetu wa pwani kama machief na kula pesa za serikali tunafanya kazi ni utamaduni wetu kufanya kazi na pesa haibadilishi watu. Fred ni rafiki yangu kutoka miaka 10, tutaenda Ilboru wote , yeye akawa mzizima na mimi Tambaza urafiki haujawahi kubadilika kutokana na pesa hata siku mmoja. Huo ndio utamaduni ambao Lowassa na wengine wengi tu wa kaskazini tunao. Tofauti na fikra za wengi familia ya Lowassa imetajirika kwa biashara na sio serikali. Kikwete ndiye katajirika kwa serikali sio Lowassa. Lowassa kuna kampuni kabisa na zinalipa kodi. Tofauti labda tu ni kusema yeye kuwa mwanasiasa imesaidia kukutana na wafanyabiashara. Lakini angalia familia kama ya kikwete ni kufanya biashara kwa sirisiri ! sasa kwanini unaficha biashara kama ni halali!.
Nisingependa kuongelea pesa za watu. Kama ni mawazo ufanye nini nikuambie hili.
Usikubali kufanikiwa peke yako maana siku ukianguka utakuwa peke yako. Saidia marafiki zako na ndugu zako nao wafanikiwe. Huo ndiyo utamaduni wa mafanikio. Vilevile usipende pesa za haraka fanya mambo ambayo yatabaki. Nakuhakikishia utajiri unao ongelea hauzidi asilimia 10% ya utajiri wa familia ya Lowassa