Kaka
Bluray alishangaa kuona post ya habari za mgonjwa imeshehenezwa innuendos nyingine zisizo hishma kabisa.a
Wengine kaka yetu huyu Obay kitambo, tunamjua cheche zake enzi zile, kabla ya Aqua, Franco had style and pioneered stuff wakati huo kina Mr. II hawa hawajafika mjini. Huyu labda anaweza kurudi kwenye era za kina Saleh Jabri na Kim Mgomelo kama si nyuma zaidi.
Umkute hapo Franco kwenye mtambo, hapo Eddo kashika mic, mpakana wewe unapata mshawasha kushika mic.
Nakumbuka mashindano ya Rap Lang'ata 1990 aliwarusha watu sana, mpaka kina Kelvin G na Connie Francis wakakubali.
Kwa hiyo tukashangaa maneno yasiyo taadhima kwa mtu alwatan.
Ndiyo mambo ya mtandao hayo, anything goes.