Franco Luambo Makiadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Franco Luambo Makiadi

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Bakulutu, Feb 1, 2012.

 1. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,895
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Watu wanaimba,wengine wana bana pua,wengine studio za kichina zinawashine suati zao...LAKINI..huyu jamaa... alikuwa mwanamziki kweli na kipaji kutoka kwa Mungu.Mfalme wa rhumba(Le grand maiter),mchawi wa gitaa(guitar sossuor).

  Kwa upande wangu mimi ndio chaguo langu la kwanza dunian pamoja na kundi lake loooote la Le Tuitor Puisant (All Power)ok jazz,kuanzia Madilu,Sager essuso,Simaro lutumba masia,Sam Mangwana'KICHWA BALAA', josky kiambukata,Mavitukuvisi & much moreee!

  Je wewe unamuelewaje Franco na TP Ok jazz nzima??????
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mkuu wewe umeniona nini nna headset hapa nasikilita Tangawusi. Huyu jamaa mungu alimtunuku hasa, nikisikiliza nyimbo zake nakumbuka miaka ya mwanzo ya themanini nikiwa mdogo kaka zangu walikuwa wakizisikiliza sana hizi nyimbo na mzee wangu! na hata quality ya nyimbo zake ni za hali ya juu sana zilirekodiwa kwenye mitambo ya kisasa sana tena mnoo! hebu sikiliza Tokabola sentiment aliyoimba Josky kiambukuta!
  Nakumbuka mwaka 1984 nikiwa songea tulikuwa na kanda yake, moja ya wimbo uliokuwepo ni mbanda ako ti kikumbi, saa yale matamshi ukisikiliza ni km anaimba matakoni kivumbi, basi si nikajirekodi kweli hiyo chorus eti matakoni kivumbi eeeeh mwanamama hahaha sister angu alikuwa anacheka hana mbavu.
  Wimbo wa Mario part 1 unanikumbusha sana bustani ya nyanya aliyolima kaka yangu mwaka 1984-85. nilikuwa nikirudi toka shule wakati huo nipo std 4 basi nakuta bro kauweka, nikiingia ndani tu mdingi anaamka ananiambia badirisha yuniform nenda kamwagie nyanya, wakati huo mie sina mpango kabsaa wa kwenda bustanini, natorokea kiwanjani kupiga chandimu, nikirudi tuu saa moja moja ni bakora kwa kwenda mbele!

  Hebu sikiliza Matata ya mwasi basi kwa leo halafu uniambie Franco amekukuna vipi
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Sikiliza Arzoni, hili ndo rhumba bana

  ..na kinshasa mama eeen arzonieee
   
 4. Mlamoto

  Mlamoto JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Note the spelling,

  Le grand Maître
  Le Tout puissant

  Nami nawakubali mno.
   
 5. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,895
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Chimurungu umenivunja mbavu saana kaka,TANGAWISI..nilikuwa naimba paka mwizi mama,paka mwizi awawe mama awaweee..MBANDA ATO KIKUMBI..ninayo mpaka clip yake nilichukua youtube,onapatikana kwenye albamu ya RESPONSER DE AMOUR..nikiwa na washa Pc yangu yangu hapa hebu ckiliza hizi pin then utnijulisha,FUATE YA COMMERCANT..franco na sam ngwana,miswi misapi na mabele ebale ya zaire,makese ya meme pamoja non weweeee!
   
 6. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,895
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Thaz...cunajua France tena kaka..
   
 7. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,895
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  kaka CHIMUNGURU HEBU NI CHECK KWENYE 0785452424 tuongee zaidi nilikuwa natafuta sana wadau wa hizi ngoma.
   
 8. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Papa Wemba Jossart Nyoka longo, Bozzi Bozziana, Gina wa Gina, Evoloko Joker (le wuatro langa langa plus Un) ni wanafunzi wake...
  Koffi na Tabu Ley, ni wafwasi wake pia... Franco the greatest of them all!
   
 9. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,895
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Alikuwa anastudio ya kundi lake pekee inatwa LONGISA studio...BINA NA NGAI NA RESPECT...MISSILE....NGUNGI(ft tabulei)...MATATA NA MWASI(dali kimoko yupo..wimbo una dakika 15)....LAYLE..TOJOUR!!..MUONGO NA MULOSI NI WATU YA KUCHOMA..WAPI WADAUUU???
   
 10. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,895
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Aaah kwa ukweli hii ngoma nilikuwa nayo ila cjawai kuickiliza ..nitamu..huo mdomo wa bata unavyo pulizwa ...arzoni munene na africa..arzon munene ya portol...
   
 11. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,895
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Ahhh mwali..papa wemba na VIVA LA MUSICA ,nyoka longo na ZAIKO LANGA LANGA 'WANA NKOLOMBOKA' waazilishi wa sokuous aka soukus vibration,walimlea pepe kale,kabla ajawaponyoka na kutoka na mtindo wa KWASA KWASA aka mayenu na kitu chake PON MOUN PAKA BUJEE..akiwa na papi tex .TABULEI ndio mtani wake wa jadi akiwa na kundi lake la Afrisa intanationale alilo liunda na dk nico kasanda na madilu kabla hawaja mkimbia 1962 na 1963.KOFFI aka mukulu bilanga..mopao mokonzi mwamuzik msomi mwenye degree ya uchumi na dikteta wa ma rapa...
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mwali si kweli uliyoyaandika.

  Hao wote wa mwanzo ni kundi la Zaiko Langa Langa na kama sikosei ni Papa Wemba ndiye alikuwa na harufu ya Franco.

  Koffi Olomide huwa hataki kukubali ila wengi wanasema kuwa kwenye mziki alitambulishwa na Papa Wemba.

  Inapokuja kwa Tabu Ley, ni BIG NO!. Tabu Ley alitoka kwenye mikono ya Dr. Nico Kassanda ambaye unaposema mchawi wa gitaa, huyu mzee alikuwa hawezekani. Ni Dr. Nico na Grand Kalle (siyo Pepe Kalle) walioandika wimbo maarufu wa Independe Chacha. Kuna kijana kaupiga tena na kutengeneza remix moja nzuri sana.  Franco na Luambo hata sijui kama walikuwa marafiki au kwa chini walikuwa maadui hasa Tabu Ley akijikakamua kufuata nyayo za Franco. Kumbuka Franco alianza zamani sana miziki. Nilishawahi kuona CD yake iliyorekodiwa mwaka 1956, jasho likanitoka.

  Luambo walikuja baadaye kutengeneza Album na Ley na moja ya wimbo hadi leo unapendwa sana na watu waliokula chumvi nyinyi na vijana wanaopenda kutafuta miziki ya zamani. Huu hapa NGUNGI.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Iliitwa Loningisa. Hapa nimepita tu. Lakini kuna zile nyimbo alizoimba na mdogo wake Bavon Marie Marie mmeshazisikia?
  Kama nilivyosema hapa nimepita tu.
   
 14. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Jasusi. weke tytle basi ya wimbo tuutafute. Nina CD kadhaa za Franco ila sijui upi ni upi. Kuna wanamuziki kibao unakuja tu kusikia baadaye kuwa kumbe walikuwa kwenye kundi la TP OK Jazz.
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sikonge,'
  Franco alianza muziki mwaka 1952. Kuna album waliimba pamoja na Tabu Ley miaka ya 80 sikumbuki jina lake. Nikiiona kwenye maktaba yangu nitarudi hapa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #16
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  wanamuziki wengi walipitia shule ya Franco. Michelino. Sam Mangwana. Madilu System na wengine wengi.
  Mtakumbuka kuwa Fan Fan Mosesengo aliyekuwa anapiga solo kwenye bendi ya Mzee Makassy Dar-es-salaam alitokea TP Ok.
  Fan Fan pia ndiye mwanzilishi wa Super Matimila ya Remmy.
  Wimbo wa Bina ngai na respect ulirekodiwa na TP Ok mwaka 1981.
  Baadaye bendi ya Ochestra Safari Sound chini ya Kasheba ikauimba kwa kiswahili
  "Mara ya mwanzo umeniomba tucheze....."
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Unaitwa NGUNGI na nimeuweka hapo juu. Infact, walitengeneza Album nzima.

  Naikumbuka sana hiyo Album kwani nilikuwa nikimtembelea Sister Dar, basi naichukua Vynil na kusikiliza siku nzima.  From Youtube:
  (From left to right: Michèl Boyibanda, Josky Kiambukuta, Wuta Mayi, Sam Mangwana, and Franco)
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #18
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Wazee huyu Luambo hata mimi na mkubali kuwa wimbo Bina na Ngai na Respect, acha kabisa.Sikonge vipi Verkys nae namkubali sana.
   
 19. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #19
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu, huyu jamaa (Georges Kiamwangana) pana wakati alimfunika kabisa Luambo na Tabu Ley hasa alipokuja na mtindo (wimbo wa New generation).

  Upigaji wake Saxaphone ulikuwa unatisha na alikuwa kama sikosei ana bendi 3 au nne huku Orch. Kiam aliyokuwa akiimbia Nyboma (namhusudu sana jamaa) na Lupua Lipua zikiwa Kenya. Baadhi ya wanamuziki walikuwa wakienda Kenya na kurudi Kinshasa na nashindwa kuelewa alikuwa akimanage vipi hayo yote.

  Bendi nyingine alizokuwa akiwatengenezea miziki (wengine ndipo wanadai zilikuwa zake) ni Les Grands Maquisards, Orchestre Kiam, Bella Bella, Lipua Lipua, Les Kamale na Empire Bakuba. Nafikiri hata urafiki wa Pepe Kalle na Nyboma vs Dali Kimoko ulianzia huko. Na nilishaambiwa kuwa pale Kinshasa ndiyo alikuwa na ukumbi mzuri wa muziki na ukiweza kupata ruhusa upige pale, basi wewe ni MKALI maana ni wachache sana kama akina TPOK JAZZ ndiyo walikuwa wakipiga ukumbi wake. Pia alishiriki kwenye film ya La VIE BELLE iliyochezwa na Papa Wemba na alicheza kama mzee mwenye Shoe shiners kibao mtaani na wanakodisha vifaa vya kazi kwake na jioni wanamlipa.

  Wimbo wa Baruti na Mikolo Mileki Ming ulinichengua sana. Infact ni kaka zangu ndiyo wasikilizaji na mie nikiiga tu maana nilikuwa dogo sana ila kumbukumbu yangu ni nzuri sana.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #20
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  niliwahi kusikia kuwa alifariki kwa Ukimwi, 1989 nadhani.
  Ugonjwa ambao hata yeye mwenyewe aliupiga vita kupitia wimbo wake wa SADA (tafsiri ya AIDS kwa Francais).
  All in all, Franco was great...
  Nakumbuka wimbo wake wa Balo Baki ft. Mangwana...
  Kuna pale penye wanaimba Kiswahili,
  "...Mimi na wewe, kisa gani Mwanamboka?"
   
Loading...