Four cylinder Vs six cylinder

Habari wakuu naomba kuweka kwenu huu mjadala mtu anayetumia cc 2000 lakini four cylinder na anayetumia cc 2000 lakini six cylinder.
Hapo tofauti ni nin
Kama engine zote ni sawa kitechnologia mwenye 6 cylinder atafaidi yafuatayo
Higher engine eficiency
Lower fuel consumption
Less vibration at low engine revolution
Smoothness springy like feeling during driving at higher speed.
Engine iwe 1500cc afu iwe single cylinder ...mafuta itakunywa kama rocket..lakini wakaongeza idadi ya cylinder zisaidiane...umoja ni nguvu.
 
Inawezekana hajakuelewa watu wa Lumumba vchwa vizto mno ila mada umeimaliza
 
Logic ni kuwa kama gari ina cyljnder 4 na cc 2000 ni sawa na gari ya cylinder 6 ya cc 2000 ambapo ulaji wa mafuta ya 6 itakuwa na nafuu kidogo.
Zote ulaji wa mafuta zinafanana,tofauti yake ni kwamba hiyo 6 cylinder itakuwa inaakimbia sana kuliko 4 cylinder
 
Hiyo ina matokeo gani katika utumiaji wa mafuta wa GARI!
 
Six cylinder ina nguvu sana na inakimbia kukiko 4 cylinder! Na six cylinder inakunywa mafuta madogo kiasi ukilinganisha na 4 cylinder.
Nguvu ya gari inatoka kwenye mafuta!! Haiwezekani GARI litumie mafuta kidogo halafu liwe na nguvu sana kuliko linalotumia mafuta mengi!!!
Ukweli ni kuwa mtengenezaji wa GARI kama anataka GARI liwe na nguvu kubwa ni lazima liwe na cylinder nyingi na matumizi yake ya mafuta yatakuwa ni makubwa!!! Usitarajie hata siku moja V8 itumie mafuta kidogo kuliko V6, na V6 itumie mafuta kidogo kuliko V4. Hii ni kweli kama magari yote tunayoongelea yako vizuri!! Ukiona V4 inatumia mafuta zaidi ya V6, ujue hiyo V4 ni mbovu!!!
 
Siyo nadra, hilo halipo!!! Huwezi kukuta gari mbili zenye idadi tofauti ya cylinder lakini CC ni sawa!! Hivi vipimo viko standard!!
 

Kweli kabisa, na ndio maana huwa wanaandika , mfano 6.8 litres v8 engine
 
Nissan xtrail zina mapiston makubwa aidha sensor zimeharibika
 
Kweli kabisa, na ndio maana huwa wanaandika , mfano 6.8 litres v8 engine
Hio ngoma sio mchezo, sahivi v8 kubwa ya Toyota ni 3UR-FE iko kwenye vx v8 zile new model inagonga 5.7litres! Sema mwendo upo yani hasa ukipata la petrol unainjoy sana overtaking! Kisahani 260km/hr
 
6 cylinder inakua na horse power kubwa hivyo na mwendo wake unakua mkubwa.....hiyo inatokana na 6 cylinder inakua na valve 6 badala ya nne....
Ulimaanisha 6 cylinder inakuwa na valve 6 au Piston 6? Mara nyingi gari zinakuwa na valve 4/piston. Kwamba za input ni mbili na output ni mbili.
 
Rotary engine hiyo mkuu. Hataro sana halafi pia ni engine za ajabu sana; hazina piston kama hizi traditional engine zetu! Shida ya hizo engine ni maintanance yake tu. Ikifa hiyo engine ni kununua mpya tu, hainaga overhaul
 
Umeelezea vizuri, umeeleweka
 
good pia six mara zote huwa haitoi muungurumo mkubwa km four na hii inachangiwa na kuwa na cyrinder nyingi zaidi ya gari zenye four. chukulia mfano pikipiki yenye piston moja au mashine ya disel yenye piston zilivyo na kelele
kama tunaangalia kelele ndege nayo itakuwa na piston ngapi s
 
kama tunaangalia kelele ndege nayo itakuwa na piston ngapi s
Mkuu comment yako, na profile picture vinaendana.
Huyo kuzungumzia gari wewe umeruka kwenye ndege, wakati wowote utarukia kwenye meli.
Jaribu kuangalia kwa kina hiki kitu. Resonance in relation to number of piston with a consideration of fuel consumption .
Kabla ya kukua kwa technology tulikuwa na kitu kinaitwa governor ambayo ilikuwa mechanical. Ilikuwa inatumia proposional principal, ie unapofungua mafuta na ndivyo yatakavyolika.
Baada ya kukua kwa technology tukapata, proposional +derivatives governor, ie hata ufungulie mafuta hadi mwisho, mafuta yatatumika kulingana na mzigo, na hata ukibania mafuta unajisubmbua kwani engine itakosa nguvu
Baadae technology ikazidi kupanuka, tukapata proposional +derivatives +intergral governor. Hii imefuata kanuni ifuatayo, ukubwa wa pua si wingi wa makamasi. Ie unaweza kuta engine ina v12, lkn ulaji wake ukawa sawa na 6cylinder. How? Ni rahisi.
Sio kwa kuwa umetengeneza choo basi kila wakati ukajisaidie, no. Utaenda chooni pale utakapobanwa.
V12 on normal loads sio piston zote 12 will be supplied with fuel, may be 6 of them.
How do they achieve comfotability? Minimization of resonance, na ndio maana zipo kimya.
Kanuni ya hapo juu in applying only ktk magari.

Mkumbuke consumption inavyo hesabiwa.
Consumption kwenye barabara = power of engine xload x conditions of load x time ÷ distance covered.
Ile consumption ilioandikwa kwenye gari ni bench tested results. Ni engine imewekwa juu ya bench ikawashwa.
Wakora
 
cc maana yake ni cubic capacity,ukubwa wa hizo cylinder ambako piston zinawekwa. cylinder chache ziwe na cubic capacity sawa na cylinder nyingi sijaelewa au naweza sema haiwezekani
kila mtu anatafsiri anavojua !! sio ulivoandika ni cubic centimeter
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…