Form two national examination, balaa linakuja!

kiwatengu

Platinum Member
Apr 6, 2012
17,640
14,782
Kama wastani wa ufaulu hautashushwa hadi 21. basi tungojee disaster kubwa, kuna shule zitakuwa na wanafunz 7 tu kidato cha tatu! mwakani.
 
7 ni wengi sana, kwa mfano wilaya nzima ya kilwa waliofanya mtihani wa mock f2 walikuwa zaid ya 1500 waliopata wastan wa 30 na zaid hawafik 50, nachingwea watahiniwa 2300 waliopata wastan hawazid 90, liwale watahiniwa 1700 waliopata wastan hawazid 70
 
Leo vijana wanafanya B.Maths and History! jamani matokeo yakitoka naomba lile wazo la kuwa na kanda maalumu kielimu litekelezwe, ili kunusuru baadhi ya mikoa ambayo elimu bado ni tatizo! ianze Lindi na Mtwara(kanda ya kusini.) balaa linakuja.
 
Hii inatokana na mfumo mbaya wa elimu, kwangu mimi 30% ni failure, kwa hiyo unaendelea na wanafunzi wengi ambao ni failure, unategemea nini huko baadae! Issue sio kushusha passing marks, bali kuoverall system nzima ya Elimu kwa iliyopo sasa ni mkorogano mtupu......sijui hata kama syllubus zinafuata, naona kama kila shule ina syllubus yake......Sidhani hata kama Wizara inafanya ukaguzi na usimamizi wa shule hizi.....enzi zetu ulikuwa ukisoma Azania na ukija Ilboru mambo hayasumbui kivile....leo hii chukua mwanafunzi umuamishie shule nyingine...utaona habari yake.....
 
Naunga mkono hoja kwa asilimia 100. Hakuna sababu yoyote ya kuwa na jeshi kubwa linalotaha mayai katika mitihani ya Kidato cha Nne. Shule zisichukuliwe kama vituo vya kulelea watoto ili wakue. Wanaenda shuleni kupata ujuzi na maarifa. Mazingira yao yaboreshwe na uwepo ufuatiliaji wa karibu. Atakayeshindwa hakuna sababu kusubiri atage yai baada ya miaka minne ni vema akafikiria cha kufanya mapema kuliko kupoteza muda wao ukizingatie elimu siyo bure. Kwa nini uchukue fedha za wanafunzi wakati wameshaonesha kutokuwa na uwezo?
 
Hii inatokana na mfumo mbaya wa elimu, kwangu mimi 30% ni failure, kwa hiyo unaendelea na wanafunzi wengi ambao ni failure, unategemea nini huko baadae! Issue sio kushusha passing marks, bali kuoverall system nzima ya Elimu kwa iliyopo sasa ni mkorogano mtupu......sijui hata kama syllubus zinafuata, naona kama kila shule ina syllubus yake......Sidhani hata kama Wizara inafanya ukaguzi na usimamizi wa shule hizi.....enzi zetu ulikuwa ukisoma Azania na ukija Ilboru mambo hayasumbui kivile....leo hii chukua mwanafunzi umuamishie shule nyingine...utaona habari yake.....[/QUOTE
Kuongeza wastani si tatizo, tatizo ni kwamba hizi shule za kata zina walimu wa kutosha kuwafundisha wanafunzi? Z
amani wastani ulikuwa ni 30 na shule zilikuwa chache na walimu walikuwepo na ndio maana failures haikuwa kubwa sana.mimi naona watakaoathirika na haya mabadiliko ni watoto wa maskini wanaosoma shule za kata ambazo hazina vifaa vya kujifunzia pamoja na walimu.
 
@ mnyalutanana; Hoja kubwa ni kwamba hata ushushe wastani wa kufaulu mpaka 20% bila ya kurekebisha kasoro zilizopo kwenye mfumo mzima wa Elimu zikiwemo hizo za Shule za Kata unafanya kazi bure. Hakuna haja ya kushusha wastani wa kufaulu hapo form II huku ukijua kabisa kwa kufanya hivyo unawapeleka hao form II failures (waliopata 30% na zaidi) kwenda kufeli tena form IV! Tena kwa kushusha wastani wa kufaulu maana yake utakuwa na failure wengi wanaoenda/watakaofeli form IV? kinachofanyika hapa ni siasa zaidi......AIBU. Nilitegemea Wizara ibakize ileile 50% au zaidi ya hapo na ifanyie kazi changamoto zinazofanya wanafunzi wasifikie hiyo 50%!
 
Kama wastani wa ufaulu hautashushwa hadi 21. basi tungojee disaster kubwa, kuna shule zitakuwa na wanafunz 7 tu kidato cha tatu! mwakani.

Hakuna kuangalia idadi ya watu, kama tuko serious tuchukue 50% waliobaki warudie tu !!!
 
Kama wastani wa ufaulu hautashushwa hadi 21. basi tungojee disaster kubwa, kuna shule zitakuwa na wanafunz 7 tu kidato cha tatu! mwakani.

hivi mtu aliokosa 50% FII huko FIV atakwenda kupata nini ???!!! tuwe serous, vijana wafundishwe vizuri, waalim wapate
nyongeza za mishahara, mazingira ya shule yaboreshe ikiwa ni pamoja na maabara na maktaba!!
Tumechoshwa na mulugese !!!
 
pwenti..... N'DAI LIKE MKUU
 
dah hii ni balaa! thats nasuggest huku kusini tupewe kanda maalumu kielimu
 
Waziri Kawambwa alisema Serikali imemaliza kujenga shule, sasa inahakikisha inaboresha elimu ndio maana wamerudisha huo mtihani.
Tunasubiri matokeo ili apate kujua ugumu wa kuboresha elimu unaomkabili.
 
katika mtihani wa mock f2 mkoa wa lindi, zaidi ya shule 30 wanafunz wake wote walifeli kupata wastan wa 30, na shule zingine kama 30 hivi zilipata mwanafunzi mmoja mmoja mwenye wastan wa 30. hali ni mbaya huku kusini.
 
ndio kuboresha elimu huko??naomba kujua kama kuna ulazima wa mtihani wa form 2???kwa nini elimu ya msingi isiboreshwe ikiwa ni pamoja na kuwalipa waalimu na kuwathamini ili wafanye kazi ipasavyo?
 
Nipo shule ya kata. F ii kufauru itakuwa maajabu kwa kuwa. 1 hawajahi soma baadhi ya masomo tangu f i. 2 mazingira mabov
 
Mimi kama mwalimu hili ni janga kubwa. Hizo takwimu hapo juu za ufaulu ktk wilaya zina ukweli. Ile mock waliovuka wastani wa 30 hapa shuleni kwetu ni 1. Vijana ni wazito na hawataki kuelimishwa mfumo wa kutokea msingi umewaharibu. Itachukua muda mrefu kwa janga hili kupungua. Eti wanafunzi 1700 wilayani waliofaulu ni 90. Huruma sana. Maboresho yaanze shule za msingi kwa mishahara ya walimu na maslai yao wapate motisha ya kufundisha.
 
Back
Top Bottom