Form 6 kuweni makini kwenye uchaguzi wa Kozi

Mwanakulipata

JF-Expert Member
Jul 17, 2018
713
1,181
Ndugu zangu mliohitimu kidato cha sita mnategemea kwenda kusoma elimu ya juu, kuweni makini na kile mnachotaka kwenda kusoma,

Maamuzi ya siku moja yanaweza yakagharimu maisha yako yote ya kila siku, utabaki ni mtu wa kuilaumu serikali, kujilaumu kwanini haukuchagua kozi ile ukachagua hii,

Obviously kuna zile kozi ambazo ni shavu na zinajulikana na kila mtu ukiona umezikosa hizo kozi, sio mbaya ukatumia cheti cha o level ukaenda kusoma Diploma kwa hicho hicho unachokitaka baadae utaendelea na degree kama kawaida na miaka itapungua yakusoma,

Kuna wale wanao ogopa familia zao, familia imeng'ang'ania aende akasome degree hatakama ni ya ualimu na wakati huku mtaani kuna walimu wa 2015 hawana ajira, kumbuka baadae ukishamaliza hiyo degree yako hapo nyumbani wazazi watakufukuza ukajitegemee hawatokuwepo nawewe kwenye msoto, maamuzi unayowewe kama wewe.

“Kuna kozi nyingine ukisoma chuo lazima ujue kuendesha Bodaboda kama Backup”

Kila la kheri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha hayana formula na hakuna kozi mbaya wala nzuri.

Inategemea na jinsi gani utakavyotumia elimu yako utakayoipata kukusaidia kukabiliana na changamoto mbali mbali.

Binafsi nilipochaguliwa kusoma BSc chemistry mwaka 2013 kila mtu alisema ni kozi mbaya na nimepotea. Wengi walinishauri nikasome ualimu enzi zile ajira za ualimu uhakika. Wengine kama umekosa MD na pharmacy omba diploma na maneno mengi.

Baada ya kumaliza tu chuo 2016 nikapata ajira kampuni binafsi kama quality assurance officer na mshahara ulikuwa mzuri Sana. 2017 nikapata ajira shirika la umma mshahara mzuri allowance kibao na ma rupu rupu ya kufa mtu.

Classmates walionicheka kipindi kile wakaenda kusoma udaktari serikali haina hata mpango nao wako kwenye vijizahanati vya private wanalipwa pesa ambayo mimi naipata kwa wiki kwa just extra duties. Waliosomea ualimu ndo kama unavyojua wako mtaani hawana hili wala lile.

So mimi ushauri wangu Vijana wasome wanachokipenda na sio kufuata mkumbo wala maneno maneno ya watu.
 
Maisha hayana formula na hakuna kozi mbaya wala nzuri.

Inategemea na jinsi gani utakavyotumia elimu yako utakayoipata kukusaidia kukabiliana na changamoto mbali mbali...
Well said.

Wengi wana comment na kusema mambo kwa emotions zao tu... huku wakiachaa ukweli pembeni
 
Mwaka 2013 tofauti na sasaivi braza, japokuwa ni kweli kila mtu na bahati yake lakini kwanini tuishi kwa kubahatisha...

Wewe upo radhi uone mdogo wako anaenda kusoma Petroleum engineering kwa kusema kila mtu anabahti yake...mambo yapo wazi na yanaonekana kabisa wahitimu ni wengi mno..ni heri vijana wachague kozi ambazo zitakuwa hata ni rahisi kujiajir
 
@Dindai
 
Ndugu zangu mliohitimu kidato cha sita mnategemea kwenda kusoma elimu ya juu, kuweni makini na kile mnachotaka kwenda kusoma,

Maamuzi ya siku moja yanaweza yakagharimu maisha yako yote ya kila siku, utabaki ni mtu wa kuilaumu serikali, kujilaumu kwanini haukuchagua kozi ile ukachagua hii...
Nakazia
 
Mwaka 2013 tofauti na sasaivi braza, japokuwa ni kweli kila mtu na bahati yake lakini kwanini tuishi kwa kubahatisha...

Wewe upo radhi uone mdogo wako anaenda kusoma Petroleum engineering kwa kusema kila mtu anabahti yake...mambo yapo wazi na yanaonekana kabisa wahitimu ni wengi mno..ni heri vijana wachague kozi ambazo zitakuwa hata ni rahisi kujiajir
huwezi kijiajiri kama hujasoma unachokipenda,

Acha kupotosha vijana waache wakasome wanachokipenda moyoni,ndio siri ya kujiajiri kwao huko
 
huwezi kijiajiri kama hujasoma unachokipenda,

Acha kupotosha vijana waache wakasome wanachokipenda moyoni,ndio siri ya kujiajiri kwao huko
Vijana wote mliomaliza six Soma kitu unapenda, mengine mbwembwe tu, To live is to earn a living.
 
Ukweli ni kwamba hatahao form six hawajui wakasomee Nini, wanaojua wanacho kipenda ni wachache sana, hivyo sisi Kama wakubwa zao, tuna wasisitiza waachane na kozi za kisiasa, Kama petroleum, sijui textile, Mara achaelogy, au ba tourism, watapoteza muda wao bure,
 
Hili unalosema ni la kweli mkuu...inabidi kama unandugu yako au kijana wako umuelekeze nini chakufanya maana baadae utakuwa mzigo kwako.
 
Baada ya kumaliza tu chuo 2016 nikapata ajira kampuni binafsi kama quality assurance officer na mshahara ulikuwa mzuri Sana. 2017 nikapata ajira shirika la umma mshahara mzuri allowance kibao na ma rupu rupu ya kufa mtu.
Bila shaka wewe utakuwa TBS au TFDA unakula bata tu. Hongera kwa kufuata njia uliyoina ni sahihi
 
Back
Top Bottom