Assalam Alaykum,
Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyoeleza, uzi huu utajikita kujaribu kutoa mwanga kwa wasiofahamu juu ya uharamu wa biashara ya forex kwa mtazamo wa sheria ya kiislamu.
Kwa siku za hivi karibuni, kumekuwa na uhamasishaji mkubwa sana juu ya biashara hii ya forex kupitia mitandao ya kijamii hapa nchini Tanzania. Waislamu wengi wa Tanzania, kwa kutofahamu dini yao ama kwa kughafilika tu, wamejikuta wakiingia kichwa kichwa kwenye biashara hii pasipo kuelewa kama ni halali ama haramu kwa mtazamo wa sheria ya dini yao.
Binafsi niliifahamu biashara hii ya forex ( na nyinginezo kadhaa) na kufungua Forex Trading Demo Account kati ya mwaka 2010 na 2011 wakati nipo chuo kikuu nje ya nchi (sitoitaja nchi), kipindi nasoma undergraduate. Kiukweli ni biashara inayolipa sana japo ni wachache sana wanaofikia daraja (level) ya kuwa washindi (in a long-term basis), wengi hupoteza pesa kwa sababu ni biashara inayohitaji elimu na uzoefu wa muda mrefu na uvumilivu wa hali ya juu na bahati pia.
Namshukuru Mwenyezi Mungu aliniongoza na nikafahamu kuwa biashara hii hainifai mimi kama muislamu na nikaweza kuachana nayo (japo iliniuma kimtindo, maana ni biashara inayolipa). Mimi nilichoangalia ni radhi za Mwenyezi Mungu kwangu hivyo nikaacha kujishughulisha na kuingiza kipato cha haramu kupitia hii biashara. Binafsi, Akhera kwangu ni muhimu kuliko Dunia.
Niliipoona biashara hii ya Forex imepamba moto nchini, nilijisikia vibaya kuona vijana wenzangu wa kiislamu wakiingia kichwa kichwa. Najua wengi ni kutojua dini tu, maana hata mimi nilikuwa vivyo hivyo mwanzoni. Hivyo niliona dhima kubwa ya kuwafikishia onyo juu ya kujihusisha na biashara hii. Nimeutua mzigo na mbele ya haki kwa Mwenyezi Mungu nitakapoulizwa nitajibu kwamba nilijitahidi kuwaeleza waislamu juu ya uharamu wa hii biashara.
Muhimu
Kuuza na kununua currencies tofauti (kama tanavyofanya kupitia Bureau de Change) si haramu kwa sheria ya kiislamu, kinacholeta uharamu kwenye biashara ya Forex ni System inayoendesha biashara yenyewe (yaani STP na ECN brokerage Systems).
Masheikh wengi wa Tanzania bahati mbaya hawana elimu ya Dunia, na hata hiyo elimu ya dini wengi wapo juu juu tu. Hivyo kamwe usijisumbue kwenda kuwauliza kuhusu Forex. Wengi hata hawajui Forex ni kitu gani kama ambavyo watanzania wengi walikuwa hawajui forex ni kitu gani.
Nakuletea Sheikh Hacene Chebbani kutoka Algeria ambaye anaishi Canada tokea mwaka 1997. Sheikh Hacene ana Masters in Islamic finance (UK, 2012) pia ana BA in Islamic Sharia kutoka Islamic University of Madinah (1993).
Nakuomba fuatilia lecture aliyoitoa Sheikh Hacene kwa wanafunzi kupitia Youtube kuhusu uharamu wa biashara ya Forex kwa mtazamo wa sheria ya kiislamu.
Sheikh anazungumzia masuala mbalimbali ya hii biashara, tafadhali ewe muislamu usiache kuitazama lecture hiyo ili upate elimu juu ya masuala hayo.
Kwa wale watakaoshindwa kuitazama, angalau ondoka na Summary ifuatayo ambayo nimeiwasilisha kwa mtindo wa maswali na majibu (Q&A) kama ifuatavyo:
Swali: Je biashara hii ina Riba??
Jawabu: Ndiyo, Kuna riba kwenye biashara ya Forex
Swali: Je, Islamic forex Trading Accounts (Swap Free Accounts) zipo na brokers wanatoa hii huduma??
Jawabu: Ndiyo zipo. Forex brokers karibia wote duniani wanatoa huduma ya account maalum kwa ajili ya waislamu tu (Islamic Forex Trading Accounts).
Swali: Je, Islamic Trading Accounts zinahalalisha biashara ya forex kwa mtazamo wa Sheria ya kiislamu?
Jawabu: Hapana, Islamic Trading Accounts bado hazihalalishi biashara hii ya Forex kwa waislamu.
Pia Sheikh Hacene amezungumzia masuala mengine kama Margin, Leverage na nidhamu ya ukopeshaji/ukopeshwaji wa mtaji.
Nimetua dhima hii na kilichobaki ni juu yako wewe muislamu, chagua kutii ama kukaidi, Dunia ama Akhera. Hilo ni juu yako.
Namshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu
Ahsante.
Pia soma fatwa hii hapa chini kutoka jopo la wanazuoni wa kiislamu: