Kununua hisa za kampuni si haramu kiislamu. Sababu unakuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni/biashara. Ila hiyo kampuni unayonunua hisa isiwe inajihusisha na biashara haramu: ( mfano pombe, kamari, hisa za mabenki zinazojihusisha na riba etc)
Mfano kununua hisa za kampuni ya Apple (NASDAQ: AAPL) sio haramu, ni halali kabisa, sababu biashara zao ni kutengeneza simu na computer. Mfano pia hisa za makampuni ya kutengeneza magari, meli, ndege, satellite communication systems, ujenzi etc zote hazina tatizo na ni halali kabisa. Epuka hisa za kampuni za kutengeneza zana za kivita, makampuni yanayokopa kwa riba, utengenezaji wa vilevi etc