FOREVER LIVING VS. ARVs | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

FOREVER LIVING VS. ARVs

Discussion in 'JF Doctor' started by KIWAVI, Jan 12, 2010.

 1. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2010
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,749
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  Wadau, leo katika mihangaiko yangu hapa dodoma nimekutana na shida kubwa, watu wansema kwamba forever living products has Aloe Vera inaondoa ukimwi na wana ushahidi

  Ombi langu kwa wale waliojaaliwa kupata ilmu ya medika, watupe undani kwani tunakwazika sana na taarifa tofauti
   
 2. O

  Omumura JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Uhondo wa ngoma ingia uicheze!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Sidhani kama kusoma medicine tu kutamfanya mtu akujibu swali lako, anatakiwa mtu aliyespecialize zaidi kwenye hii mitishamba.
  Otherwise, that could be gud nyuz!
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Hakuna dawa inaweza kuuondoa UKIMWI once ukishaingia mwilini.
  ARVs zinasaidia tu katika kupambana na kumuongezea mgonjwa muda wa kuishi na wala zenyewe hazitibu UKIMWI.Dawa pekee ni kuzuia usiambukizwe VVU/HIV. BASI!
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,934
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Kwanza ni lazima ujue kuwa kuna tofauti kubwa tu kati ya UKIMWI (AIDS) na VVU (HIV). VVU bado hakuna dawa ya kuviangamiza au kuzuia visitende kazi katika mwili wa binaadamu. Unaweza ukawa na VVU lakini usiwe na UKIMWI. Na kimantiki, unaweza ukawa na upungufu wa kinga mwilini lakini usiwe na VVU (magonjwa kama kansa ya damu husababisha kinga ya mwili kupungua).

  Kwa sehemu kubwa UKIMWI, hupimwa kwa kuangalia kiasi cha CD4 (zikianza kuwa pungufu ya 200 counts, then kitaalamu una UKIMWI na ndipo hapo wengi huanza kutumia ARVs). Kuna 'vyakula' vingi tu ambavyo husaidia kuongeza kinga ya mwili (including baadhi ya products za Forever Living) na hivyo kumsaidia mtu mwenye VVU asiingine kwenye stage ya UKIMWI mapema kama bado au kumsaidia mwenye ukimwi kuongeza kinga yake.

  Binafsi, bado siamini kama products za Forever Living (FL) zinaweza kuwa mbadala wa ARVs hasa ukizingatia kuwa ARVs zipo za aina nyingi na zinaendana na stage na aina ya VVU. Sidhani kama products za FL zinazingatia haya.
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Jan 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kwakweli nimekua nikisikia habari za hayo madawa ya forever, ila inapaswa kujiuliza swali moja je yanatengenezwa nchi gani, je mamlaka ya chakula na madawa imeyauhusu kutumika, je yana dozi kweli ama yananywewa kama mwarubaini tu yaani kunywa weeh mpaka uone matokeo , na je imethibitika yanatumiwa nnchi nyingine.
   
 7. American lady

  American lady Member

  #7
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wadau endeleeni kujipa moyo mtashinda.hakuna cha dawa wala nn na uvicheche wa malaya ukimwi utaishaje?dawa ni moja tu kuacha ngono zembe tikishajifahamu tumeshanyemelea michangudoa huko gizani tunaanza kuzua ooh! dawa zimepatikana.dawa tunazo wenyewe hatuzitumii.
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  watu wa forever wanaamini kwamba wanaweza kutibu KI-SUKARI kwa dawa zao...!tulibishana mpaka sauti zikatukauka
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  ila haya madawa mala foreva livingi mala sijui nini hata sijui inakuwaje cause hivi yanatibu kweli??
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  Geoff mie pia huwa nashindwa kuyaamini ..nimeshatumia yale ma Aloe Gel nakunywaga tu eti kwa afya hizi Colgate zao ,sijui Lotion na vitu vya urembo mbaya zaidi vina bei sana kwa mtu mwenye maisha ya chini mtu huwezi kabisa ku afford
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  wasanii sana hawa viumbe
  MIMI NI MWANACHAMA HAI WA TIENS!..ninajua ins and outs
   
 12. P

  Pathetic New Member

  #12
  Jan 15, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani tusifarijiane tukaja danganyika kirahisi. Mpaka sasa hakuna dawa yenye uwezo wa kuondoa VVU kwa mtu aliye athirika. Hii ni kutokana na tabia ya VVU ambavyo ni virusi vilivyo kwenye kundi la RETROVIRUS.
  Virusi hawa kwanza wanauwezo mkubwa sana wa kujibadilishabadilisha, kiasi cha kwamba ndani ya mwili wa mtu mmoja kunakuwa na aina tofautitofauti ya virusi hawa ( Kitaalamu Quasy species)(strains). Hii hufanya kinga ya mwili kushindwa kuwaondoa.

  Pia virusi hivi huathiri seli zinazohusika na kinga mwilini zenye kitambulishi cha CD4, kama CD4 +ve T-Lymphocytes, Macrophages(monocytes), na Dendritic cells. Ndani ya hizi seli kirusi hiki huweza kukaa kwa miaka mingi wakiwa katika hali ya utulivu i.e. latent state. Na dawa haiwezi kuja kuwaua hawa virusi ndani ya hizi seli bila kuziua hizi seli , kitu ambacho ni hatari kwa afya ya muathirika.
  Hawa virusi wanazaliana ndani ya hizi seli zinazohusika na kinga ya mwili na ili kutoa virusi wapya hizi seli hufa. na ndo maana kiwango cha CD4 seli ndani ya mwili hupungua.

  Kilichowezekana sasa ni kupunguza kasi ya kuzaliana kwa hawa virusi ndani ya mwili na hivyo kupunguza kasi ya kuuwawa kwa CD4 +ve seli na hatimaye kupandisha kinga ya mwili. Ila seli zilizo athirika zitaendelea kuwa na virusi bali watakuwa hawazaliani.

  Tuendelee kumuomba mungu tafiti zinaendelea kufanyika ili tuweze kupata kinga mbadala ya VVU/UKIMWI.
  Mpaka sasa kinga pekee madhubuti ya ukimwi ambayo itakupunguzia uwezekano wa kupata VVU/UKIMWI kwa asilimia kubwa sana ni abstainace from having unprotected penetrative sex with multiple patners.
   
 13. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  jamani ni vile tu watanzania tunautamaduni wa kuenzi vya nje na kuponda vya kwetu ila hizo product za fl mimea wanayotumia hapa kwetu ipo ila aijapakiwa kitaalamu kama fl na zinafanya kazi sawa na kuzidi kwani vyetu vingi avijawekwa kemikali ili kuviifazi
  mwisho aiwezekani itibu ukimwi labda kuongeza kinga mwilini kama wafanyavyo wazawa kama dr ndondi
   
 14. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2010
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,749
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  asante sana... sasa je ile promotion wanayofanya hawa watu wa forever ni sawa? au wanibia wateja kwa kutoa kitu kisicholigana na sifa zake?
   
 15. U

  Urenga One Member

  #15
  Jan 19, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Are you FirstLady1 ? or Jokes? pole kumbe na wewe unatumia FL sasa njoo upate Mpako hapa Ubungo Please I beg you!!! dont worry
   
 16. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,532
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  very good points, lakini je vinajibu point ya mtoa mada?
   
Loading...