Ford Everest Titanium 2022

profesawaaganojipya

JF-Expert Member
Apr 21, 2015
1,485
3,134
Msaada kwa wanaoifahamu, waliowahi kuendesha au hata kumiliki hii gari aina ya FORD EVEREST TITANIUM 2022.

Kuna rafiki yangu anataka kununua hiyo gari 0 km anaulizia;

1. Upatikanaji spea hapa Tanzania

2. Uvumilivu wa barabara za rafu, anakaa dar ila atakuwa anaenda makete mara kwa mara

3. Speed barabarani

4. Durability na comfortability

IMG_20230530_065548.jpg
 
Anaetaka kununua hyo 0.km ya 2022 ndo kakutuma uje kuulizia umu
ndio mkuu,kila mtu ana malengo yake, huyu mzee anakaribia kustaafu tunafanya wote kazi,kesha miliki daladala tata zilikuwa sita na alinunua mpya pale vngunguti,baada ya kuja mwendokasi akauza zote.

Hajawahi kununua gari ndogo ya kutembelea,yeye anasema akistaafu na ataanza kuishi kama yuko peponi,hata smatphone hana,ana kiswaswandu tu,ni mkinga wa makete..
 
ndio mkuu,kila mtu ana malengo yake,huyu mzee anakaribia kustaafu tunafanya wote kazi,kesha miliki daladala tata zilikuwa sita na alinunua mpya pale vngunguti,baada ya kuja mwendokasi akauza zote...
Kutoka kumiliki daladala tata ndo anataka kumiliki Ford everest 0.km ya 2022??.mshauri atafute gari ndogo ya kawaida tu,change inayobaki aendelee kukuza mtaji wake kwanza
 
Kuna dogo anayo ya 2021 alinunuan
km elf 3 tu na amekuwa akipiga nayo kazi mkoa kwa mkoa now ina km 60k haijawah pappta shida yoyote zaid ya kuifanyia service pekee
Unaponunua gari 0 km acha mawazo ya spear za nn? Gari ni nzima na mpya! Hakikisha service tu inafanyika kwa oil sahihi
 
Kutoka kumiliki daladala tata ndo anataka kumiliki Ford everest 0.km ya 2022??.mshauri atafute gari ndogo ya kawaida tu,change inayobaki aendelee kukuza mtaji wake kwanza
kwa sasa hana biashara yeyote,hela iko saccos,amepanda mbegu huko,anasema akistaafu hataki usumbufu wa biashara,yeye atakuwa anatumia hela kidogokidogo na mshahara unaingia kama 1m kila mwezi,na viakiba vyake vitamtosha kuishi hapa dar,hataki stress za biashara..
 
Msaada kwa wanaoifahamu, waliowahi kuendesha au hata kumiliki hii gari aina ya FORD EVEREST TITANIUM 2022.

Kuna rafiki yangu anataka kununua hiyo gari 0 km anaulizia;

1. Upatikanaji spea hapa Tanzania

2. Uvumilivu wa barabara za rafu, anakaa dar ila atakuwa anaenda makete mara kwa mara

3. Speed barabarani

4. Durability na comfortability

View attachment 2639963

1. CMC zipo hizi anaweza kununua atapata warranty

2. Spare zote zipo CMC, cheki instagram fordtanzania
 
Back
Top Bottom