Foleni Ubungo, Trafic Police na Rushwa ya Bodaboda

mchukiaufisadi

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
546
193
Kuna hisia kuwa vijana wa Bodaboda wa Morogoro Road wanachangia kwa kiasi kikubwa foleni ya asubuhi. Huchangishana hadi kama Tshs 50,000 kisha hupelekewa trafik anayeongoza magari ili acheleweshe kuruhusu magari yatokayo upande wa Morogoro ili abiria washuke na kupanda bodaboda.

Trafiki akikabidhiwa, ataruhusu magari yatokayo Mwenge au atatengeneza mkoroganyo wa magari pale kati na kujifanya anayapangua huku akitoa muda kidogo sana kwa magari yatokayo upande wa Moro ili kuruhusu bodaboda wafanye kazi yao na kuvuna kufidia pesa yao.

PCCB, Wizara husika waliangalie maana watu wanateseka huku wengine wanafanya biashara
 
Back
Top Bottom