Foleni new model

Foleni new model

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,459
Reaction score
872,114
1415755785369.jpg
 
Mshana hiyo Benki itakuwa na harufu ya shombo ya miguu kubwa sana
au ni POSTA hapo maana inanikumbusha kule Posta ya Mombasa Usangi enzi zile mthuya katuwekea
Havache thana muathu
 
Unanikumbusha enzi za Nyerere tulikuwa tunaenda makatambuga, mawe, makopo, betri zilizokufa kwenye duka la kata saa nane za usiku, hatujui kukicha tutaambulia nini.

Watoto wa sasa mshukuru, hamjayakuta hayo.

Ni enzi za RTC hizo bidhaa kwa foleni na kwa kiwango
 
Mshana hiyo Benki itakuwa na harufu ya shombo ya miguu kubwa sana
au ni POSTA hapo maana inanikumbusha kule Posta ya Mombasa Usangi enzi zile mthuya katuwekea
Havache thana muathu

Hahahahaaa ukwaju si unazungumzia Store Mombasa pale Kiriche? I real miss the place!
 
Unanikumbusha enzi za Nyerere tulikuwa tunaenda makatambuga, mawe, makopo, betri zilizokufa kwenye duka la kata saa nane za usiku, hatujui kukicha tutaambulia nini.

Watoto wa sasa mshukuru, hamjayakuta hayo.
Nyerere kwa mara nyingine ... !!!
 
Yaelekea bila kumtaja Nyerere unaugua weye! Haya bwana
 
Na hakuna aliyekuwa ananung'unika kwa sababu wote tulikuwa kwenye foleni bila kujali kiongozi au mtu wa kawaida! Lakini siku hizi wakubwa wakiumwa hata funza tu kidoleni hao nje, kajamba nani utaponea kwa mganga wa jadi!
 
Nyerere kwa mara nyingine ... !!!

Huo ndio ukweli, wakati wake ndio ilikuwa hivyo ulitaka tumtaje nani? Alipoingia Mwinyi yote hayo yakaisha kama muujiza, hata miezi sita haijachukuwa, mpaka leo hii. Wengi wenu hamjayakuta hayo.
 
Na hakuna aliyekuwa ananung'unika kwa sababu wote tulikuwa kwenye foleni bila kujali kiongozi au mtu wa kawaida! Lakini siku hizi wakubwa wakiumwa hata funza tu kidoleni hao nje, kajamba nani utaponea kwa mganga wa jadi!

Hapana, si ukweli, hakuna kiongozi aliyekuwa anakaa foleni, walikuwa wanapelekewa makwao.

Hata Nyerere alikuwa akitibiwa nje mpaka kafia hukohuko na hakufia Tanzania, au hulijuwi hilo?

Unung'unike si unapotezwa, unaujuwa udikteta wewe? muulize Ludovick Mwijage, kaandika yaliyomkuta. Alinung'unika, ni nini kilichomkuta? kama hujuwi jisomee: http://searchworks.stanford.edu/view/6346732
 
Hapana, si ukweli, hakuna kiongozi aliyekuwa anakaa foleni, walikuwa wanapelekewa makwao.

Hata Nyerere alikuwa kitibiwa nje mpaka kafia hukohuko na hakufia Tanzania, au hulijuwi hilo?
Serkali yake haikuwa na deni MSD kiasi cha kutishia uhai wa wananchi wake!
 
Unanikumbusha enzi za Nyerere tulikuwa tunaenda kupanga makatambuga, mawe, makopo, betri zilizokufa kwenye duka la kata saa nane za usiku, hatujui kukicha tutaambulia nini.

Watoto wa sasa mshukuru, hamjayakuta hayo.

na umri wote huo alafu hauna akili.
 
Yaelekea bila kumtaja Nyerere unaugua weye! Haya bwana

Mleta mada kaona hiyo ni "foleni new model", mimi namfahamisha foleni tulizokuwa tukiweka wakati wa Nyerere, hiyo ni cha mtoto, hao wako ndani wamekaa juu ya viti wanangoja huduma, sisi tulikuwa tuko nje, mtaani, saa nane za usiku tunawahi kwenda kupanga mawe na hatujuwi tutakipata nini, na huo ulikuwa wakati wa Nyerere.

Hampendi kujuwa tulipotoka? kwa sisi tuliowahi kukaa foleni wakati wa Nyerere, hii si "foleni new model".

Huo ndio ukweli.
 
Mleta mada kaona hiyo ni "foleni new model", mimi namfahamisha foleni tulizokuwa tukiweka wakati wa Nyerere, hiyo ni cha mtoto, hao wako ndani wamekaa juu ya viti wanangoja huduma, sisi tulikuwa tuko nje, mtaani, saa nane za usiku tunawahi kwenda kupanga mawe na hatujuwi tuakipata nini, na huo ulikuwa wakati wa Nyerere.

Hampendi kujuwa tulipotoka? kwa sisi tuliowahi kukaa foleni wakati wa Nyerere, hii si "foleni new model".

Huo ndio ukweli.

Inawezekana ni kweli lakini siku nyingine na mazuri pia uyakumbuke kwani bila yeye wengi wenu hata kuandika isingewezekana kabisa (Ingawa najua utapinga ukweli huu)
 
Serkali yake haikuwa na deni MSD kiasi cha kutishia uhai wa wananchi wake!

Wananchi wengi walipoteza uhai kuliko unavyofikiria.

Average Life Expectancy ya Mtanzania wakati wa Nyerere haijazidi miaka 48, fikiri.
 
Inawezekana ni kweli lakini siku nyingine na mazuri pia uyakumbuke kwani bila yeye wengi wenu hata kuandika isingewezekana kabisa (Ingawa najua utapinga ukweli huu)

Hapana, si ukweli, nimeanza kusoma kabla Nyerere hajataifisha mashule na shule zilikuwa ni bora kuliko wakati wowote ule.

Nyerere alijitahidi kuwa kila mtu ajuwe angalau kusoma gazeti la ngurumo. Matokeo? Tanzania ikawa ya mwisho kwa wasomi katika Afrika ya Mashariki.

Usidanganywe na mtu.
 
Unanikumbusha enzi za Nyerere tulikuwa tunaenda kupanga makatambuga, mawe, makopo, betri zilizokufa kwenye duka la kata saa nane za usiku, hatujui kukicha tutaambulia nini.

Watoto wa sasa mshukuru, hamjayakuta hayo.

Kumbe Faiza kikongwe!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom