FNP90 BUNDUKI hatari saana

Robot la Matope

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
7,041
13,689
Bunduki fupi, nene, nyeusi kutoka Israeli iliyokuwa ikitumiwa na kikosi cha usalama cha rais wa Marekani cha ‘Secret Service’ kabla ya bunduki ya Kibelgiji ya FNP90 yenye uwezo wa kutoboa kinga ya risasi na yenye shabaha imara zaidi kuliko Uzi, IMI Uzi, Bunduki ya Yehuda, iliyotumiwa na magaidi wa Kolonia Santita dhidi ya Vijana wa Tume katika operesheni ya kutetea afya na amani ya dunia jijini Copenhagen na Mexico City.

Kasoro za Uzi zilizofanya zisitumiwe tena na kikosi cha usalama cha rais wa Marekani ni kutokuwa na shabaha imara katika umbali mfupi (hutawanya risasi na huleta madhara makubwa katika umbali mfupi hivyo kuweza kudhuru hata watu wasiokuwa na hatia) na kutokuwa na uwezo wa kutoboa kinga ya risasi dhidi ya magaidi wanaotumia mavazi ya kuzuia risasi, wanaotishia usalama wa rais wa Marekani.

Gaidi mwenye mavazi ya kuzuia risasi anaweza kumdhuru rais kwa maana ya USSS kushindwa kumdhibiti. Badala yake sasa USSS wanatumia FNP90, zenye uwezo wa kutoboa kinga ya risasi, ambazo hazileti madhara makubwa katika umbali mfupi na katika umbali mrefu pia.

Bunduki hizi, zenye uwezo wa kubeba risasi 100 katika chemba zake mbili za Kampuni ya Beta (‘Century Magazines’), zilitumiwa na magaidi wa Kolonia Santita dhidi ya Vijana wa Tume na dhidi ya polisi wa Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya.

Uzi ni bunduki iliyokuwa ikitumiwa na kikosi cha usalama cha rais wa Marekani katika miaka ya themanini na ni bunduki inayotumiwa na wanajeshi wa nchi mbalimbali katika masuala ya vita na kulinda amani.

Source :Enock Maregesi FB
FB_IMG_1494683109381.jpg
 
Back
Top Bottom