Flyover inayofaa Ubungo ni hii hapa

Flyover inayofaa Ubungo ni hii hapa

ridculouz

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
910
Reaction score
504
KWA MAONI YANGU NADHANI MCHORO HUU UNAFAA UKIJENGWA PALE UBUNGO MATAA , KUMEKUWA NA MICHORO MINGI ISIO ENDANA NA UFINYU WA NAFASI YA PALE UBUNGO NA NI YA GARAMA KUBWA LAKINI HUU KIDOGO UNABANA NAFASI NA NI RAHISI MTU UPANDE WOWOTE KUINGIA NA KUTOKA . NAFIKIRI WENGI WETU MNA JUA ADHA YA KUINGIA UBUNGO TERMINAL UKIWA UMETOKEA MJINI LAKINI KUNGEKUWA NA FLYOVER YA NAMNA HII TUSINGEPATA ADHA YA KUINGIA STAND KUU NA KUELEKEA MJINI,MWENGE NA BUGURUNI NA KIMARA.

ASANTENI.

ANGALIZO .

MSIINGIZE SIASA HILI NI WAZO BINAFSI.

liB3dh9.jpg
 
Mchoro mzuri sana unafanana na Sinsen Interchange Oslo, Norway.

Ila sasa huwa kuna tatizo la foleni kwenye huo mzunguko hapo kati.. hasa kwa wanaotoka mwenge kwenda magomeni.. kusubiriana na wale wanaotoka tabata kwenda magomeni..

Huu mchoro ungefaa sana Tazara maana traffic kubwa huwa ni airport-mjini na ubungo-kurasini.

2cf210229652b92c63ae27747ae33c3e.jpg
 
good explanation, pengine itasaidia kubana bajeti pia,maana nimeona michoro mingi ya gharama sana, awnway tunasubiri final SELECTION
 
Magari yanayotoka barabara ya mandela kuelekea Mwenge yatapita barabara ya juu kabisa (mshale mwekundu) vivo hivyo magari yanayotoka Mwenge, Mlimani city mikocheni n.k kuelekea Tabata ,Buguruni, Bandarini n.k yatapita barabara ya juu. (mshale wa blue)


FhfFmAZ.jpg
 
Upande wa Magari yanayotoka Mwenge, Mlimani city, n.k kuelekea kimara , Mbezi n.k yatapita kwenye mzunguko (round about ) (mshale wa blue)

Na kama unaelekea mjini na Ubungo terminal unachepuka (kushoto mshale wa blue)


lhknd9N.jpg
 
Mchoro mzuri sana unafanana na Sinsen Interchange Oslo, Norway.

Ila sasa huwa kuna tatizo la foleni kwenye huo mzunguko hapo kati.. hasa kwa wanaotoka mwenge kwenda magomeni.. kusubiriana na wale wanaotoka tabata kwenda magomeni..

Huu mchoro ungefaa sana Tazara maana traffic kubwa huwa ni airport-mjini na ubungo-kurasini.

2cf210229652b92c63ae27747ae33c3e.jpg
Ni kweli mkuu lakini tutakwa tumepunguza foleni kidogo maana hata Tazara kuna upande wanapita juu bila kusimama na kuna upande lazima wasimame
 
Wanaoelekea Kimara, Mbezi n.k watachepuka mapema kushoto (mshale mwekundu)
ambapo wataenda kuunganika na barabara ya Morogoro na mara nyingi Kwa wenzetu hizi lane zinakuwa ndefu kidogo kama mita 600 kwa sababu zinakuwa zina magari mengi yanaenda kuingia Barabara moja . Hapa kwetu hakuna kitu kama hicho, nimeona pale Urafiki lane ya kuingia Sinza ni ndogo sana .



eF2Ingn.jpg
 
Mkuu, naomba nikuchallenge kidogo...
Ulianza kujua vipimo vya eneo husika ndo ukachora plan au umeanza kuchora kwanza ndo ukaipa jina la mahali?

Na je umefikiria kuhusu ukubwa wa eneo husika?

Kwa haraka inaonekana Songas wahamishe mashine zao zote (200 MW) na upande wa pili Ubungo Main substation ihame....
Bomba la gesi pia linalokatiza hapo?

Gharama ya project?
Vipaumbele?

Mwisho nakupongeza kwa ubunifu mzuri.
 
Huo upana number 2 ukikadiria ni kama meter ngapi hivi?. Sidhani kama utaweza ku-fit pale Ubungo. Hata huo upana number 1 (horizontal) hauwezi.
sB9tgWg5.jpg
 
Mkuu, naomba nikuchallenge kidogo...
Ulianza kujua vipimo vya eneo husika ndo ukachora plan au umeanza kuchora kwanza ndo ukaipa jina la mahali?

Na je umefikiria kuhusu ukubwa wa eneo husika?

Kwa haraka inaonekana Songas wahamishe mashine zao zote (200 MW) na upande wa pili Ubungo Main substation ihame....
Bomba la gesi pia linalokatiza hapo?

Gharama ya project?
Vipaumbele?

Mwisho nakupongeza kwa ubunifu mzuri.
Ni kweli ila hawatabomoa kwa kiasi kikubwa kama ile flyover ya mwanzo hii watabomoa kidogo , na hicho ndoo Serikali yetu haipendi kuwalipa fidia watu.

Asante kwa pongezi mkuu

Mara nyingi natumia barabara ya morogoro , changamoto huja napotaka kuingia Ubungo stand nikitokea mjini maana kunyoosha ili nikapige u turn kibo mbali sana nikiingia mandela pale songas pia hamna u turn ukiingia sinza ili upite nyuma ya stand uje utokee Petrol station kuna kuwa na trafiki na Efd zao wanakwambia ile sio barabara yaani ni shida.
 
Ni wazo zuri. Ila ukifanya research kidogo utagundua nyingi ya flyover za namna hii hazipo katikati ya changanyikeni kama Ubungo. Huwa ziko kidogo nje ya mji, ambako utaenda na kugeuza kushika njia unayotaka. Flyover za namna hiyo kukaa katikati ya mji ni vema zikapanda juu zaidi ili huku chini maisha mengine yaendelee kama kawaida. Mathalani mzunguko wa kutoka Mwenge kuelekea Magomeni ungepita mpaka juu ya mageti ya Tanesco, bila kuathiri kilicho chini. Kwahiyo baadhi ya mizunguko ya flyover ipite juu ya Tanesco na Songas, na stracture nyingine ambazo si lazima kuzibugudhi. Hiyo nadhani italeta tija zaidi na kwa gharama ndogo. Ni wazo tu.
 
Mi nadhani kwa sababu rais ni mtaalamu wa haya mambo atajenga tu ila lazima aanze na pale salenda kuelekea coco beach
 
Back
Top Bottom