Fly over TAZARA badilisheni muda wa mataa

Fly over TAZARA badilisheni muda wa mataa

Aliyekwambia interchange ya tazara itapunguza foleni za magari Ni nani....Lile dili la watu washapiga washatembea...

Acheni kudangaya watu imesaidia sana kupunguza foleni kwa wale wanaotoka airport kwenda mjini na mjini kwenda airport pale juu magari yasepa ile mbaya
 
Hbr wadau, Jana (jumapili)nimepita kwenye junction flyover ya Tazara nikitokea ubungo to Mbagala via Mandela road baada ya kusikia fly over imeeanza nikajua mambo mpeto, maana huwa natumia morogoro road na kilwa road siku zote kukwepa foleni. Sasa nilichostaajabu bado niliganda buguruni sheli na pia baada ya buguruni sheli pia tukaganda kusubiri mataa maana mnyororo bado mrefu na timing za mataa ni zilezile za kabla fly over.
Mapendekezo yangu.
Wahusika wabadili timing za Mataa; kama ifuatavyo.
1. Mandela road- Mandela road iwe sekunde 120 (dk mbili) kama pale junction ya kamata gari zinazotoka posta ...
2. NYERERE ROAD - NYERERE/MANDELA( Sec 30) gari nyingi zipo fly overs ni chache tu zitazokatiza kwenda Temeke
3. Waruhusu pia zinazotoka NYERERE ROAD (TBC)TO MANDELA ( KUPINDA KULIA) SEC 30
4. MATAA YA MANDELA TO MANDELA YAWE YANURUHUSU GARI SAMBAMBA IE YANAYOTOKA FROM NORTH-SOUTH NA SOUTH -NORTH KAMA YALE YA CHANGOMBE.
5. mabadiliko haya ili yafanye kazi ipasavyo pia Timing ya mataa ya BUGURUNI SHELI YASETIWE UPYA.
6. Kwa mabadiliko haya Fly over itakuwa na msaada sana, bila haya mabadiliko Mandela road bado itakuwa ni mateso sana.
Ahsante sana kwa ushauri wako, wahusika fanyieni kazi haya mapendekezo
 
Kuna member mmoja alikuja na mchoro ukuonyesha kituo cha bus kipo karibu na mataa sikuelewa ali refer kituo gani kumbe moonhoni mwa maeneo yanayofanana na ule mchoro ni Buguruni
Haswaaa..., hicho cha buguruni ndio kilinisukuma kuchora
 
Umepita pale au unabwabwaja nyuma ya keyboard? Kutoka airport hadi veta nimetumia less than 20 leo.
Aisee, hii ni habari njema sana, maana nilishaanza kuhisi mradi umekuwa white elephant, atleast umenipunguzia wasiwasi
 
Mie nilisha sema humu flyover TAZARA wakati Buguruni kuna makutano ya barabara haitasaidia. Mfano Ubungo pale mradi ukikamilika subiri uone foleni za kwenda Mwenge, Buguruni na Magomeni.
Flyover ni nzuri kwa kupendezesha jiji tu.
Flyover imewekwa kusolve shida ya pale tazara na sio shida ya jiji zima mbona wabongo ni wagumu namna hii
 
Aisee, hii ni habari njema sana, maana nilishaanza kuhisi mradi umekuwa white elephant, atleast umenipunguzia wasiwasi
Huwa nikipitia kinyerezi-airport-city center natumia zaidi 1hr45mins asubuhi, leo nimetumia 1hr tu. Sasa utaacha kusema mradi una faida?
 
Hbr wadau, Jana (jumapili)nimepita kwenye junction flyover ya Tazara nikitokea ubungo to Mbagala via Mandela road baada ya kusikia fly over imeeanza nikajua mambo mpeto, maana huwa natumia morogoro road na kilwa road siku zote kukwepa foleni. Sasa nilichostaajabu bado niliganda buguruni sheli na pia baada ya buguruni sheli pia tukaganda kusubiri mataa maana mnyororo bado mrefu na timing za mataa ni zilezile za kabla fly over.
Mapendekezo yangu.
Wahusika wabadili timing za Mataa; kama ifuatavyo.
1. Mandela road- Mandela road iwe sekunde 120 (dk mbili) kama pale junction ya kamata gari zinazotoka posta ...
2. NYERERE ROAD - NYERERE/MANDELA( Sec 30) gari nyingi zipo fly overs ni chache tu zitazokatiza kwenda Temeke
3. Waruhusu pia zinazotoka NYERERE ROAD (TBC)TO MANDELA ( KUPINDA KULIA) SEC 30
4. MATAA YA MANDELA TO MANDELA YAWE YANURUHUSU GARI SAMBAMBA IE YANAYOTOKA FROM NORTH-SOUTH NA SOUTH -NORTH KAMA YALE YA CHANGOMBE.
5. mabadiliko haya ili yafanye kazi ipasavyo pia Timing ya mataa ya BUGURUNI SHELI YASETIWE UPYA.
6. Kwa mabadiliko haya Fly over itakuwa na msaada sana, bila haya mabadiliko Mandela road bado itakuwa ni mateso sana.
Ni Fly over au Daraja!!?
 
Wewe ndio unapotosha uma.
Ile iwe flyover lazima chini kuwe na Barabara chini.
Ili liwe daraja lazima chini kuwe mto, reli sehemu ya bahari kama kigamboni na the like.
Hapana, mimi nakupinga,inamaana unataka kuniambia ile ya manzese ni flyover?
 
Wewe ndio unapotosha uma.
Ile iwe flyover lazima chini kuwe na Barabara chini.
Ili liwe daraja lazima chini kuwe mto, reli sehemu ya bahari kama kigamboni na the like.
Daraja la Manzese kuna MTO chini? au Kimara stendi ya mwendokasi lile tuliite fly over ya Kimara!!?
 
Utakuta hilo la taa hawakuwaza hata maana hawa jamaa zetu wanaopewa dhamana ya kusimamia maendeleo ya hii nchi mambo mengi wafanya kwa kutumia akili ndogo sana. Kila kitu mpaka wakosolewe ndo kinakaa vizuri
Jamani tuwe na positive mind kwa manufaa ya maendeleo ya nchi. Mwenzako amechangia kutoa mapendekezo kwa tatizo aliloliona. Hii ndiyo inahitajika na si kulalamika tu. Wewe unakuja na habari ya akili ndogo ya watendaji. Wewe mwenye akili kubwa toa pendekezo lako tulipime.
 
Hii italeta msongamano mkubwa buguruni, mataa ya chang'ombe na ukanda wa majumbasita
 
Back
Top Bottom