Fly over kujengwa Mloganzila

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
160603155228_barabara_kuu_512x288_bbc_nocredit.jpg
MRADI wa ujenzi wa barabara sita kutoka Kimara hadi Kibaha Maili Moja mkoani Pwani, utakuwa na madaraja mapya matatu pamoja na fly over moja itakayojengwa eneo la Mloganzila.

Hayo yalielezwa juzi na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale, wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi huo utakaogharimu zaidi ya Sh. bilioni 140. Mradi huo unatekelezwa na kampuni ya Estim Construction Co. Ltd ya jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Tanroad. Akizungumza kwenye ukaguzi huo uliofanywa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe Mfugale , alisema madaraja hayo yatajengwa maeneo ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji, pamoja daraja la juu eneo la Mloganzila. “Ujenzi wa barabara hii utahusisha barabara sita, tatu kwenda mjini na tatu kwenda Kibaha na itakuwa na urefu wa kilometa 19.2,” alisema Mfugale.

Aliongeza kuwa uwezo wa barabara ya Morogoro ni kupitisha magari 8,000 kwa siku, lakini kwa sasa zaidi ya magari 50,000 yanapita.

Alisema mradi wa ujenzi wa barabara hiyo utachukua miezi 27 na utakamilika Januari 2020 na kwamba hadi sasa mkandarasi ameshafanya kazi kwa asilimia 5.8. Kwa upande wake Waziri Kamwelwe alisema fedha zitakazotumika ujenzi wa mradi huo zimetolewa na serikali ya Tanzania na hakuna hata senti moja kutoka kwa wafadhili. “Ni fedha zilizotokana na kodi za Watanzania, hakuna senti ya wafadhili, serikali imedhamiria kuendeleza uwekezaji katika miundombinu ya barabara, lengo likiwa ni kupunguza msongamano,” alisema Kamwelwe.

Alisema serikali ilijenga njia nne katika barabara ya Morogoro, lakini hazikutosha, ikalazimika kujenga mradi wa mabasi yaendayo ingawa lakini haikusaidia na ndiyo sababu ikajenga mradi wa njia sita. Zaidi ya nyumba 2,000 zilizokuwa ndani ya hifadhi ya barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kiluvya zilibomolewa ili kupisha ujenzi wa mradi huo. Tanroad iliwahi kueleza kuwa barabara ya Morogoro ipo kisheria tangu mwaka 1932 na ubomoaji nyumba hizo ulifanyika kisheria kwa kuwa wakazi hao walijenga ndani ya mita 121.5 za hifadhi ya barabara.
 
View attachment 906937MRADI wa ujenzi wa barabara sita kutoka Kimara hadi Kibaha Maili Moja mkoani Pwani, utakuwa na madaraja mapya matatu pamoja na fly over moja itakayojengwa eneo la Mloganzila.

Hayo yalielezwa juzi na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale, wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi huo utakaogharimu zaidi ya Sh. bilioni 140. Mradi huo unatekelezwa na kampuni ya Estim Construction Co. Ltd ya jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Tanroad. Akizungumza kwenye ukaguzi huo uliofanywa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe Mfugale , alisema madaraja hayo yatajengwa maeneo ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji, pamoja daraja la juu eneo la Mloganzila. “Ujenzi wa barabara hii utahusisha barabara sita, tatu kwenda mjini na tatu kwenda Kibaha na itakuwa na urefu wa kilometa 19.2,” alisema Mfugale.

Aliongeza kuwa uwezo wa barabara ya Morogoro ni kupitisha magari 8,000 kwa siku, lakini kwa sasa zaidi ya magari 50,000 yanapita.

Alisema mradi wa ujenzi wa barabara hiyo utachukua miezi 27 na utakamilika Januari 2020 na kwamba hadi sasa mkandarasi ameshafanya kazi kwa asilimia 5.8. Kwa upande wake Waziri Kamwelwe alisema fedha zitakazotumika ujenzi wa mradi huo zimetolewa na serikali ya Tanzania na hakuna hata senti moja kutoka kwa wafadhili. “Ni fedha zilizotokana na kodi za Watanzania, hakuna senti ya wafadhili, serikali imedhamiria kuendeleza uwekezaji katika miundombinu ya barabara, lengo likiwa ni kupunguza msongamano,” alisema Kamwelwe.

Alisema serikali ilijenga njia nne katika barabara ya Morogoro, lakini hazikutosha, ikalazimika kujenga mradi wa mabasi yaendayo ingawa lakini haikusaidia na ndiyo sababu ikajenga mradi wa njia sita. Zaidi ya nyumba 2,000 zilizokuwa ndani ya hifadhi ya barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kiluvya zilibomolewa ili kupisha ujenzi wa mradi huo. Tanroad iliwahi kueleza kuwa barabara ya Morogoro ipo kisheria tangu mwaka 1932 na ubomoaji nyumba hizo ulifanyika kisheria kwa kuwa wakazi hao walijenga ndani ya mita 121.5 za hifadhi ya barabara.
Asante kwa taarifa Msemaji wa sirikali.
 
Drainage system iko chini sana Dar
Wangewekeza zaidi hapo
Kwa kweli sasa tuko kwenye right track
Ila nimependa huu msemo wa siku hizi kuwa " hela zote ni za walipa kodi hakuna hata senti ya wafadhili"
 
Hiyo barabara haioneshi kama kuna mwendokasi hapo katikati Lkn juzi Magu kasema mwendokasi mpaka kibaha
 
Back
Top Bottom