Fly over kujengwa Mloganzila

Fly over kujengwa Mloganzila

Rejea maneno yangu ya awali mkuu, nilisema kuna Uzi humu unamuhusu mfugale
Kiufupi huyu ni Mhandisi, madaraja mengi unayoyaona ukienda mikoani yamebuniwa na mfugale, hivyo kwa vile kila siku wanasiasa ndio wanaopata credit kwenye mitaa, barabara n.k basi wakaona hapo Tazara apewe mfugale,
Ok, searching it. I"ll be back
 
Wanazidi kuniwekea kibaha kwangu kama ulaya vile, karibuni kibaha
 
Mwanzoni mwa uzi huu, nilitaka CV ya huyu mtu. Mbona hujaiweka hdi sasa ikiwa amewahi kufanya mambo makubwa hivyo? Sikubali awekwe the same level na akina JK Nyerere, R.M. Kawawa na akina Sokoine
Basi utawekwa wewe.
 
View attachment 906937MRADI wa ujenzi wa barabara sita kutoka Kimara hadi Kibaha Maili Moja mkoani Pwani, utakuwa na madaraja mapya matatu pamoja na fly over moja itakayojengwa eneo la Mloganzila.

Hayo yalielezwa juzi na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale, wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi huo utakaogharimu zaidi ya Sh. bilioni 140. Mradi huo unatekelezwa na kampuni ya Estim Construction Co. Ltd ya jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Tanroad. Akizungumza kwenye ukaguzi huo uliofanywa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe Mfugale , alisema madaraja hayo yatajengwa maeneo ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji, pamoja daraja la juu eneo la Mloganzila. “Ujenzi wa barabara hii utahusisha barabara sita, tatu kwenda mjini na tatu kwenda Kibaha na itakuwa na urefu wa kilometa 19.2,” alisema Mfugale.

Aliongeza kuwa uwezo wa barabara ya Morogoro ni kupitisha magari 8,000 kwa siku, lakini kwa sasa zaidi ya magari 50,000 yanapita.

Alisema mradi wa ujenzi wa barabara hiyo utachukua miezi 27 na utakamilika Januari 2020 na kwamba hadi sasa mkandarasi ameshafanya kazi kwa asilimia 5.8. Kwa upande wake Waziri Kamwelwe alisema fedha zitakazotumika ujenzi wa mradi huo zimetolewa na serikali ya Tanzania na hakuna hata senti moja kutoka kwa wafadhili. “Ni fedha zilizotokana na kodi za Watanzania, hakuna senti ya wafadhili, serikali imedhamiria kuendeleza uwekezaji katika miundombinu ya barabara, lengo likiwa ni kupunguza msongamano,” alisema Kamwelwe.

Alisema serikali ilijenga njia nne katika barabara ya Morogoro, lakini hazikutosha, ikalazimika kujenga mradi wa mabasi yaendayo ingawa lakini haikusaidia na ndiyo sababu ikajenga mradi wa njia sita. Zaidi ya nyumba 2,000 zilizokuwa ndani ya hifadhi ya barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kiluvya zilibomolewa ili kupisha ujenzi wa mradi huo. Tanroad iliwahi kueleza kuwa barabara ya Morogoro ipo kisheria tangu mwaka 1932 na ubomoaji nyumba hizo ulifanyika kisheria kwa kuwa wakazi hao walijenga ndani ya mita 121.5 za hifadhi ya barabara.
Lakini serikali ilipaswa kutoa taratibu za ujenzi kwa watu wake fikiria tangu 1932 hadi labda mtu alijenga miaka ya 70 hadi 80 angejuaje. Watendaji wa barabara na waziri wa ujenzi. Kwa tawala zote walikua wapi wasitoe maelekezo kwa wananchi ?
 
View attachment 906937MRADI wa ujenzi wa barabara sita kutoka Kimara hadi Kibaha Maili Moja mkoani Pwani, utakuwa na madaraja mapya matatu pamoja na fly over moja itakayojengwa eneo la Mloganzila.

Hayo yalielezwa juzi na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale, wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi huo utakaogharimu zaidi ya Sh. bilioni 140. Mradi huo unatekelezwa na kampuni ya Estim Construction Co. Ltd ya jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Tanroad. Akizungumza kwenye ukaguzi huo uliofanywa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe Mfugale , alisema madaraja hayo yatajengwa maeneo ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji, pamoja daraja la juu eneo la Mloganzila. “Ujenzi wa barabara hii utahusisha barabara sita, tatu kwenda mjini na tatu kwenda Kibaha na itakuwa na urefu wa kilometa 19.2,” alisema Mfugale.

Aliongeza kuwa uwezo wa barabara ya Morogoro ni kupitisha magari 8,000 kwa siku, lakini kwa sasa zaidi ya magari 50,000 yanapita.

Alisema mradi wa ujenzi wa barabara hiyo utachukua miezi 27 na utakamilika Januari 2020 na kwamba hadi sasa mkandarasi ameshafanya kazi kwa asilimia 5.8. Kwa upande wake Waziri Kamwelwe alisema fedha zitakazotumika ujenzi wa mradi huo zimetolewa na serikali ya Tanzania na hakuna hata senti moja kutoka kwa wafadhili. “Ni fedha zilizotokana na kodi za Watanzania, hakuna senti ya wafadhili, serikali imedhamiria kuendeleza uwekezaji katika miundombinu ya barabara, lengo likiwa ni kupunguza msongamano,” alisema Kamwelwe.

Alisema serikali ilijenga njia nne katika barabara ya Morogoro, lakini hazikutosha, ikalazimika kujenga mradi wa mabasi yaendayo ingawa lakini haikusaidia na ndiyo sababu ikajenga mradi wa njia sita. Zaidi ya nyumba 2,000 zilizokuwa ndani ya hifadhi ya barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kiluvya zilibomolewa ili kupisha ujenzi wa mradi huo. Tanroad iliwahi kueleza kuwa barabara ya Morogoro ipo kisheria tangu mwaka 1932 na ubomoaji nyumba hizo ulifanyika kisheria kwa kuwa wakazi hao walijenga ndani ya mita 121.5 za hifadhi ya barabara.

Mlogazira flyover ya nini?
 
Kama mbezi hakuna interchange basi huu mradi ni wa ovyo.
 
Nakubali, kama Mbezi hakuna interchange au flyover basi project ina mapungufu makubwa. Ila kuna jinsi wanataka kufanya pale ili magari yasikatize sana, huenda foleni ikapungua kwa kiasi kikubwa.
 
Shida kubwa sana ni miji kutokupangwa manake ni mhimu miji hii iwe imepangwa vzr iendane na mahitaji ya watu..
 
Back
Top Bottom