Fly over kujengwa Mloganzila

Fly over kujengwa Mloganzila

Drainage system iko chini sana Dar
Wangewekeza zaidi hapo
Kwa kweli sasa tuko kwenye right track
Ila nimependa huu msemo wa siku hizi kuwa " hela zote ni za walipa kodi hakuna hata senti ya wafadhili"
hahah itakuwa msemo mpya huu wafadhili wamepumzishwa
 
Ile ya tazara wameandika mfugale flyover, who is mfugale by the way in this beautiful country, kodi tulipe sisi majina mjiandike nyie.
 
Swafiiii sana
Mola a tuongoze walahi
 
Yaani wasijenge Mbezi waende kujenga Kibamba? Hilo ni ajabu lingine.
 
Mradi wa barabara ya njia sita kutoka Kimara hadi eneo la Maili Moja jijini Dar es Salaam, utahusisha ujenzi wa madaraja makubwa pamoja na barabara moja ya juu (flyover).

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Babarabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale amebainisha hayo alipokuwa akikagua mradi huo unaogharimu Sh140 bilioni, ukitarajiwa kukamilika Januari 2020.

Amesema kuwa barabara ya juu itajengwa katika eneo la Mloganzila, hivyo kuongeza idadi ya barabara za juu baada ya ile ya njia panda ya Tazara.

Mfugale ameeleza kuwa mradi huo unatekelezwa na kampuni ya Estim Construction, chini ya usimamizi wa Tanroads.


“Hii barabara itakuwa na urefu wa Kilometa 19.2, na baada ya kukamilika barabara hii itakuwa na uwezo wa kupitisha magari 8,000 kwa kila barabara kwa siku,” alisema na kuongeza kuwa hivi sasa magari takribani 50,000 yanayopita yanasababisha msongamamo mkubwa.

Amefafanua kuwa hadi sasa ujenzi wa mradi huo unaotumia fedha za ndani umefikia asilimia 5.8. Zaidi ya nyumba 2000 zilivunjwa ili kupisha utekelezaji wa mradi huo.


Serikali imeendelea kufanya juhudi za kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, ambapo mbali na ujenzi wa barabara ya juu ya Tazara (Mfugale Flyover), daraja la Kigamboni pamoja na mpango huo wa Mlonganzila, maeneo mengine yanayotajwa ni pamoja na njia panda ya Ubungo, Kamata na Morocco.

Flyovers saba ziko kwenye mpango wa kujengwa katika mpango wa awamu ya kwanza ya kukabiliana na msongamano wa magari jijini humo.

Screenshot_2018-10-24-10-53-08.jpeg
 
Njia tatu kwenda tatu kurudi kwa highway inabidi ifuate Motorway code ambapo kila junction inapaswa kuwa na flyover zitakazowezesha gari kutoka na kuingia kwenye highway bila kuathiri traffic flow.
 
Ile ya tazara wameandika mfugale flyover, who is mfugale by the way in this beautiful country, kodi tulipe sisi majina mjiandike nyie.
Kuna Uzi humu kuhusu Eng mfugale mkuu, fukua makaburi utapata
Kingine acha roho ya kwanini, roho ya inda kijana mdogo haitokusaidia
 
Hizo kodi zetu ingependeza zikajengwa na kampuni za wazawa hela yetu ibaki nchini
 
Huyo mtu kafanya makubwa sana katika nchi hii,
Ndo maana nikasema punguza roho ya kwanini
Mwanzoni mwa uzi huu, nilitaka CV ya huyu mtu. Mbona hujaiweka hdi sasa ikiwa amewahi kufanya mambo makubwa hivyo? Sikubali awekwe the same level na akina JK Nyerere, R.M. Kawawa na akina Sokoine
 
Mwanzoni mwa uzi huu, nilitaka CV ya huyu mtu. Mbona hujaiweka hdi sasa ikiwa amewahi kufanya mambo makubwa hivyo? Sikubali awekwe the same level na akina JK Nyerere, R.M. Kawawa na akina Sokoine
Rejea maneno yangu ya awali mkuu, nilisema kuna Uzi humu unamuhusu mfugale
Kiufupi huyu ni Mhandisi, madaraja mengi unayoyaona ukienda mikoani yamebuniwa na mfugale, hivyo kwa vile kila siku wanasiasa ndio wanaopata credit kwenye mitaa, barabara n.k basi wakaona hapo Tazara apewe mfugale,
 
Back
Top Bottom