Flora Mbasha na Edward Lowassa

Flora Mbasha na Edward Lowassa

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
15,638
Reaction score
20,248
Copy%2Bof%2BDSC07478.JPG

Mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh.Edward Lowassa akiwa pamoja na Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. John Komba na wengineo wakitest ubora wa Studio hiyo kwa kusikiliza baadhi nyimbo kadhaa zilizorekodiwa na studio hiyo ambayo imezinduliwa hivi karibuni nyumbani kwakwe Flora Mbasha (mwenye gauni damu ya mzee) huko Tabata Kisukulu jijni Dar wikiendi hii

Copy%2Bof%2BDSC07470.JPG

Baadhi ya vyombo vya studio hiyo ya Msanii Flora Mbasha vikiwa tayari vimefungwa. Studio hiyo itatumika kurekodi nyimbo za muziki wa Injili na hata kuwasaidia wasanii wachanga wenye vipaji kwa ajili ya kuviendeleza. Flora Mbasha anakuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike wa nyimbo za Injili kufungua studio yake mwenyewe

Huyu dada ambaye watu wanaamini ana upako huwa simwelewi,..kwanza nilimwona kavaa manguo ya kijani mwaka jana kikwete alipotangazwa rasmi kuwa mgombea kwa tiketi ya ccm,..nafikiri ni mwanachama wa ccm sababu aliwapigia hata debe wakati wa uchaguzi!!sasa hii ya kumwalika lowasa ndo imeniacha hoi,.lowasa amethibitika beyond reasonable doubt kuwa ni fisadi papa,may be iam wrong lakini sina heshima na huyu dada na gospel zake nilishaacha kuzisikiliza
 
hayo ni maendeleo. pongezi dada flora umekula matunda ya uchaguzi mkuu kwa kazi inayoonekana kwa macho. wakuu yafaa tumpongeze kwa hilo tuache roho ya kwa nini!
 
Mkuu kwani hujui kuwa waimbaji wa Gospel karibu woooooote wapo kibiashara zaidi? Na wengi wao wanadhani kuji-atach na ccm ndio kufanikiwa mapema. Huenda ni sawa lakini hiyo ni dalili kubwa sana ya unafki uliotukuka. wengi wa hawa ni wanafki.

Jaribu kufanya utafiti kama kweli wanaimba kwa nia ya kutangaza injili, ni kiasi gani cha mapato yao wanatoa kama sadaka kwa njia tofauti tofauti?
 
Hii hela ndo ilimuua YESU...Hii hela ndo shetani kuu la hii dunia.
Kila mtu amekua msaliti kwa ajili ya hela.
 
Yesu alikula na mtoza kodi Zakayo, ana dhambi gani Lowasa ya kutoalikwa na Mbasha?
 
Mtume paulo tayari alikwisha kusema wanawake waache kuwa waropokaji makanisani na kama wana maoni wakawaeleze waume zao baada ya kutoka makanisani..........................sasa huyu kweli aijua Biblia Takatifu au anaisigina tu ili mradi apate mkate wake wa kila siku......................................

Soma Corithians 14: 34-38 na 1 Timothy 2: 11-15
 
Huyu dada ambaye watu wanaamini ana upako huwa simwelewi,..kwanza nilimwona kavaa manguo ya kijani mwaka jana kikwete alipotangazwa rasmi kuwa mgombea kwa tiketi ya ccm,..nafikiri ni mwanachama wa ccm sababu aliwapigia hata debe wakati wa uchaguzi!!sasa hii ya kumwalika lowasa ndo imeniacha hoi,.lowasa amethibitika beyond reasonable doubt kuwa ni fisadi papa,may be iam wrong lakini sina heshima na huyu dada na gospel zake nilishaacha kuzisikiliza
Mkuu, mbona huyu ni "kada" wa ccm; na wasee wa ccm wamemtunuku ubunge wa viti maalum ili wasee (EL) waendelee kufaidi ?
 
Mkuu kwani hujui kuwa waimbaji wa Gospel karibu woooooote wapo kibiashara zaidi? Na wengi wao wanadhani kuji-atach na ccm ndio kufanikiwa mapema. Huenda ni sawa lakini hiyo ni dalili kubwa sana ya unafki uliotukuka. wengi wa hawa ni wanafki.

Jaribu kufanya utafiti kama kweli wanaimba kwa nia ya kutangaza injili, ni kiasi gani cha mapato yao wanatoa kama sadaka kwa njia tofauti tofauti?

Acha uwongo wewe! Kwa nini mnapenda kuandika vitu msivyofanyia utafiti. Tatizo lenu kila kitu ni ku-generalize. You should be fair mnapotoa comments zenu.
 
Ukiona hivyo ujue Mzee EL katia mchango wake kwenye hiyo studio.
Ila sishangai kwa Florah kula pesa ya EL, mbona maaskofu wanalamba bila ubishi na wala hatujasikia ametengwa kama wanayotengwa wazinzi makanisani?

ANGALIZO: Chonde chonde kina Mbasha na wengine kuleni hela yake ila msitujie hapa 2015 na kauli za "EL ni chagua la Mungu"!
 
hayo ni maendeleo. pongezi dada flora umekula matunda ya uchaguzi mkuu kwa kazi inayoonekana kwa macho. wakuu yafaa tumpongeze kwa hilo tuache roho ya kwa nini!

umesema vyema
 
Acha uwongo wewe! Kwa nini mnapenda kuandika vitu msivyofanyia utafiti. Tatizo lenu kila kitu ni ku-generalize. You should be fair mnapotoa comments zenu.

Ni vizuri ukanukuu uongo ni upi na ukweli unaoujua wewe ni upi katika hayo sio unaongea kama umetoka maliwato.
 
Lowassa sijui alikuwa anatengeza track hapo kama vile anashusha chorus
 
Ukiona hivyo ujue Mzee EL katia mchango wake kwenye hiyo studio.
Ila sishangai kwa Florah kula pesa ya EL, mbona maaskofu wanalamba bila ubishi na wala hatujasikia ametengwa kama wanayotengwa wazinzi makanisani?

ANGALIZO: Chonde chonde kina Mbasha na wengine kuleni hela yake ila msitujie hapa 2015 na kauli za "EL ni chagua la Mungu"!

Ha ha ha ha ha
 
Hii hela ndo ilimuua YESU...Hii hela ndo shetani kuu la hii dunia.
Kila mtu amekua msaliti kwa ajili ya hela.
Acheni kugeuza jumba la Baba Yangu kugeuzwa kuwa kama pango la wanyang'anyi Flora Mbasha!!!
 
icon1.png
Re: Flora mbasha na edward lowassa

quote_icon.png
Originally Posted by Gosbertgoodluck
Acha uwongo wewe! Kwa nini mnapenda kuandika vitu msivyofanyia utafiti. Tatizo lenu kila kitu ni ku-generalize. You should be fair mnapotoa comments zenu.

Acheni kugeuza jumba la Baba Yangu kugeuzwa kuwa kama pango la wanyang'anyi Flora Mbasha!!!

Unaona unafiki niliongea? Anatuimbia hivyo halafu yeye anashirikiana na wanyang'anyi hao hao. JE HUU SI UNAFIKI?
Nazidi kusema hawa watu wapo kibiashara zaidi, no more?
 
Haya mamaa Flora Mbasha,
Sijui vizuri lakini,
Mmmmmmmmm sikuelewi kabisaaaaaaa!!
 
Mkuu kwani hujui kuwa waimbaji wa Gospel karibu woooooote wapo kibiashara zaidi? Na wengi wao wanadhani kuji-atach na ccm ndio kufanikiwa mapema. Huenda ni sawa lakini hiyo ni dalili kubwa sana ya unafki uliotukuka. wengi wa hawa ni wanafki.

Jaribu kufanya utafiti kama kweli wanaimba kwa nia ya kutangaza injili, ni kiasi gani cha mapato yao wanatoa kama sadaka kwa njia tofauti tofauti?

Hata kama wakitoa sadaka kiasi gani haimaanishi kuwa ndiyo wako sawa. Napenda pia kuwambia wana JF kuwa wengi hufunika maovu yao kwa kujifanya kuwa ukitoa sadaka ndiyo wametenda vyema kwa Mungu.
 
Back
Top Bottom