Flora Mbasha achumbiwa, kuolewa tena

Reucherau

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
756
1,740
Sakata hilo linaweza kuibua mjadala miongoni mwa waumini wa dini ya Kikristo ambayo pamoja na kuruhusu ndoa kuvunjika, ni nadra sana kwa makanisa kuidhinisha suala hilo.

=============

Flora Mbasha achumbiwa, kuolewa tena
Dar es Salaam. Baada ya wanandoa ambao ni wanamuziki maarufu wa nyimbo za Injili, kuingia katika mzozo miaka minne iliyopita, mmoja wao Flora Mbasha amechumbiwa na anatarajiwa kufunga ndoa ya pili hivi karibuni mkoani Mwanza.

Sakata hilo linaweza kuibua mjadala miongoni mwa waumini wa dini ya Kikristo ambayo pamoja na kuruhusu ndoa kuvunjika, ni nadra sana kwa makanisa kuidhinisha suala hilo.

Habari za kuaminika ambazo Mananchi Digital imezipata zinasema vikao vya maandalizi ya harusi hiyo vimeshaanza baada ya Flora kufanikiwa kupata talaka aliyoidai Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini hapa.

Flora, ambaye ni mjukuu wa aliyekuwa muhubiri maarufu nchini, Askofu, Moses Kulola (sasa marehemu), tayari amevishwa pete ya uchumba na amebadili jina la kisanii akitaka mashabiki wake wamtambue kama “Madame Flora” badala ya jina aliloibukia la Flora Mbasha.

Asili ya neno “madame” analotumia Flora ni Ufaransa na linamaanisha mwanamke aliyeolewa.

“Kwa sasa siwezi kukwambia chochote kuhusu hilo. Sijui, labda ifikapo Machi naweza kuzungumza,” amesema Flora, ambaye alitamba na kibao cha “Jipe Moyo”.

Chanzo: Mwananchi
 
Wanapowahubiri wenzao kuhusu shetani lakini akiwapitia wao wanabwaga manyanga nakumbuka sana wimbo wake huyu Dada Wa "jipe moyo"
 
Hilo kanisa litakalofungisha ndoa Hiyo kwa Mara yapili,ili hali wanajua ni mke wa mtu,litajuta,labda ndoa ya serikali
 
Back
Top Bottom