Flip flopping in Oil and Gas contracts | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Flip flopping in Oil and Gas contracts

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zitto, Sep 19, 2012.

 1. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  On sunday

  "Some of the agreements are really shoddy and they need to be revoked," noted the minister

  On Tuesday


  'We are not trying to stop any business. We will not revoke any contract, we will respect all contracts,'
  Energy and Minerals Minister Sospeter Muhongo

  I said and i repeat, Prof. Muhongo as a CCM Minister is going to do nothing. Tanzania doesnt need reviews of contracts. Tanzania needs a radical approch on Oil and Gas contracts one of which is to legislate that all contracts will be made open and accessible. I have seen some of these contracts. They dont need a review done in board rooms. Once they are made public.................

  Review announcement was simply a short term publicity stunt. And here he is. A flip flopper

   
 2. p

  pembe JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  what is the impression? Does it mean we don't have lawyers who can draft a win win agreement? Or are they forced by whoever to draft shoddy contracts? Shule ya nini sasa kama mambo ni hovyohovyo tu ktk nchi hii?
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wamemnyamazisha Prof. Hawa cowboys a.k.a wawekezaji wakinyanyua simu hata mawe mazito yataondolewa. Another reason to make changes 2015.
   
 4. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Transparency is a solution. We have got lawyers at TPDC and we always use experts to write these contracts for us. Minister wants same body that entered contracts to review them. Wrong. Make them Open and Tanzanians see for themselves. Transparency is the best cure for shoddy deals.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Zitto, why did the Prof change his stance/direction on this? What caused him to change his 'plans?
   
 6. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #6
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Wamemnyamazisha? Hakuwa anamaanisha. Najua hakuwa anamaanisha. CCM haipo tayari kufanya maamuzi magumu kwneye mikataba hii.

  Ndio maana tunahitaji break ya miaka kadhaa kujiweka sawa kama nchi bila kutangaza vitalu vipya. Hii mikataba ya sasa inahitaji ukaguzi wa gharama kwanza.

  Tunaibiwa sana sana huko kwenye ukaguzi wa gharama za utafutaji. Katika mikataba 26 tumekagua mikataba 4 tu na TPDC haijapewa kibali cha kuajiri. Kwenye kikao cha kamati ya POAC tulishauri kwamba CAG apeleke wakaguzi TPDC kama wakazi pale ili kumaliza ukaguzi wa mikataba hii.

  Sekta ya Mafuta na Gesi sio sekta ya kukurupuka. Ni sekta inayohitaji umakini sana katika kuishughulikia. Hatuhitaji mapitio bali uwazi.
   
 7. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #7
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Plans? There was no plan. Alikurupuka.
   
 8. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #8
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  He shot before aiming. We must be strategic. Tactics will not work.
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Really?
   
 10. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Man you are fighting a losing battle! Ningekuwa wewe ningejifikiria mara mbili kuhusu kuendelea na siasa hapa Tanzania kwani jinsi ninavyoona kwa upande wako ni hakuna jinsi ambavyo unaweza ukawabadilisha Watz tena na kurudisha zile siku ambazo wengi walikukubali, the damage is done man wanasema Wazungu, mambo mengi sana yanasemwa kuhusu wewe, shutuma nyingi zenye madoa zinaelekezwa kwako na sioni jinsi unaweza ukarudi kwenye kiwango cha kukubalika na wananchi wa kawaida ulichokuwa nacho zamani! Game over man, sorry for that!

   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Zitto tusaidie kidogo. Ninesoma mara nyingi na sehemu mbalimbali na katika mojawapo ya habari hizi imesemwa kuwa Tanzania haina sera ya gesi na mafuta. Ninafahamu kuwa tayari gesi inachimbwa na soko la gesi kipo. Sasa hii inaongozwa na kusimamiwa vipi bika sera? Je tuna sheria yoyite inayosimamia sekta hii ukiondoa sheria ya madini?
   
 12. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Sasa Bro unauliza swali wakati unaona maisha yanaendelea asee... Kama ni Gas inauzwa, na wese watachimba na kuuza bila sera na hakuna Swali....
   
 13. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #13
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Kuna sheria ya utafutaji mafuta ya mwaka 1980 ambayo ina mapungufu makubwa sana. Hatuna Sera ya Gesi Asilia. Hatuna Mkakati (natural gas masterplan) na hatuna sheria ya matumizi ya fedha zinazotokana na mafuta na gesi.

  Ndio kwa sasa tunapinga kugawiwa kwa vitalu vipya mpaka tumalize nyaraka hizi muhimu sana kwa nchi yetu. Vile vile tunatakiwa kumaliza ukaguzi wa gharama za utafutaji zinazofanywa na haya makampuni.

  Kimsingi ilipaswa kusimama kufanya lolote kwa sasa maana unafanyaje mambo haya bila sera na sheria madhubuti?
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,499
  Likes Received: 19,913
  Trophy Points: 280
  well saidi Zitto sitaki kukusifia ila kwenye sekta ya gesi tumekurupuka na kuna wakubwa wanafaidika sana kwa sasa , kabla hawajaenda mbali na kujijenga zaidi kwenye hii sekta inabidi tuwakurupue . We have to wake up najua ni kazi sana kumuelewa zitto but he s making a good and open point ukitaka kuelea anachofanya just sit down think you will understand kuwa jamaa kwa nini anapiga makelele. ccm imetuchoka
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  kwa nini jambo hili hukuwapelekea wenye nchi kupiti M4C ambao wangeweza kuandamana kutetea maslahi yao, badala yake unajifanya mwanadiplomasia kulitegemea bunge lenye nguvu (ccm) ya kuwashinda hoja zenu (chadema) hata ziwe bora vipi!!!!
   
 16. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Mbona wewe kwenye nakala yako dhidi ya waziri ya "Public stunt" waliweka nakala yako yote tukaisoma kuilewa na kutoa maoni na sio kukunakili sentensi moja kama wewe unavyomfanyia huyu Waziri? Huoni kwamba haumtendei haki? Mbona wewe hawakukufanyia hivyo?

  Mimi naona wewe unaugomvi binafsi na huyu Waziri, kwa nini unamquote sentensi moja, siutuwekee nakala nzima ili tuweze kuona alikuwa anamaanisha nini?

  Ni kama vile maadui wa Irani wanavyosema Raisi wao alisema anataka kuifuta Israel wakachukua kasentensi kamoja kumbe ukisikiliza hotuba nzima hakumaanisha hivyo mimi nina Rafiki Muirani akaniambia Hotuba nzima ya Raisi wao hakumaanisha hivyo, kwa hiyo na wewe tuwekee hapa article nzima zote mbili tusome na kuweka judgement zetu kwamba Waziri alikuwa anamaanisha nini alivyosema hivyo, vinginevyo mimi kwangu naona ni kama alivyosema Lowasa shida ni Uwaziri Mkuu!
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  kwa mtazamo mpana zaidi naye kama angekuwa anaweza kuzuia asingetuletea tujadili, sasa anapoleta mjadala kwa baadhi ya jamii ya watanzania linakuwa kosa lilelile la usiri wa baraza la mawaziri, sitaki iwe na taswira ya muungano kuwa na ufichouficho, tujadili kwa kiswahili lugha yetu ya kwanza. Kizungu mbwembwe tu!
   
 18. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..Mh.Zitto Na Je endapo Watanzania watakuteua leo uongoze timu ya kuwatengenezea Sera nzuri ya Gesi asilia, unadhani nini vitakuwa vipaumbele vyako vitano katika Sera hio?
   
 19. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #19
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Sera haitengenezwi na mtu mmoja. Sera hutengenezwa na wadau wote. Moja tu lipasa kuongoza sera 'kwamba nchi inufaike zaidi ya makampuni katika rasilimali hii ya mafuta na gesi'
   
 20. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #20
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Huyu Waziri mimi sigombane naye nini? Sina jambo la kugombana naye. Mimi ni Mbunge wa upinzani na kazi yangu kubwa sana ni kuonyesha kuwa CCM na Mawaziri wake wote hawawezi kuongoza nchi yetu kwa manufaa ya wananchi. Pia sipendi mtu awafanye Watanzania mabwege. Anajua kabisa kwamba hawezi fanya asemacho lakini anasema tu ili kuonyesha kuwa Serikali ya CCM inafanya kazi wakati haifanyi kazi. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye sekta ya Madini na miaka kumi tukawa tunafanya kazi ya ku review tu lakini dhahabu inasombwa. Hili ndio ninalolikataa
   
Loading...