Ubungoubungo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2008
- 2,502
- 739
Zitto, najua tayari tunayo gas. lakini je? mafuta tunayo tayari? si muwaache watutafutie kwanza jamani tukiyapata ndo mbele kwa mbele tutapambanaga hukohuko chadema ikiwa imeshachukua nchi (kama na wewe bado utakuwa chadema au utasepa..naongea hivi kutokana na nyendo zako), kuliko sasa ambapo kwa harakati zenu mnaweza mkazuia hata watafutaji wapya ambao wangetusaidia kujua wapi kuna mafuta na wapi hakuna na pengine tungejijua tz kama tunayo mafuta au la. nchi kama kenya wamepata mafuta, wamefanya kitu gani cha tofauti na sisi.....hatuwezi kuwa tunazuia wawekezaji kama tunafanya kila kitu complicated jamani...tusicomplicate maisha saaana kihivyo kuna faida na hasara zake.Kuna sheria ya utafutaji mafuta ya mwaka 1980 ambayo ina mapungufu makubwa sana. Hatuna Sera ya Gesi Asilia. Hatuna Mkakati (natural gas masterplan) na hatuna sheria ya matumizi ya fedha zinazotokana na mafuta na gesi.
Ndio kwa sasa tunapinga kugawiwa kwa vitalu vipya mpaka tumalize nyaraka hizi muhimu sana kwa nchi yetu. Vile vile tunatakiwa kumaliza ukaguzi wa gharama za utafutaji zinazofanywa na haya makampuni.
Kimsingi ilipaswa kusimama kufanya lolote kwa sasa maana unafanyaje mambo haya bila sera na sheria madhubuti?