WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Kama ni kweli watu bongo bado wanatumia mbinu hizi kuhalalisha uhusiano, basi wengi wao wanaingia mkenge kirahisi mno. Maana asilimia kubwa za familia zinazojulikana kama za kitajiri (hasa zile za old money) zimeshachoka mbaya long time. Kilichobakia ni jina na majivuno ya kulinda heshima....lakini mfukoni kweupeee.
Usomi hau-guarantee maisha mazuri, na ubosi umejaa "show-of" ya company resources (nyumba, magari, viji safari vya hapa na pale), lakini akaunti haziko stable. Ukitaka kujua ukweli ngoja ubosi huo umwagiwe unga.
Dizaini watu bado wanaingizwa kanyaboya kwa sana tu...
QM,
Pamoja na maneno mazuri uliyosema hapo juu, bado hujahitismisha vizuri.Unadhani ipi ni ideal situation?
Hii mada inafurahisha sana maana ukianza kuijadili, mawazo na mitizamo ya kila aina inajitokeza:
1.Ni mzazi gani asiyetaka mwanae awe na maisha mazuri? Mara nyingi sana wazazi wa binti husumbuka na kufadhaika sana pale wanapoona au kuhisi kuwa binti anataka kuolewa na bwana asiye na mwelekeo kimaisha.Kuna baadhi inasemekana hata huwapiga interview hao wanaotaka kuposa na maswali na majibu ni kama hivi-
Q. una nyumba?
A.HAPANA
Q.UNA GARI
A.HAPANA
Q.UNA kazi , biashara (PESA)
A.HAPANA
Q.UNA DEGREE
A.HAPANA
Q.UNA DIPLOMA
A.HAPANA
Q. SASA HAPA UMEFUATA NINI?
Kwa maana nyingine mzazi anapima ni kwa vipi muoaji atamudu kuendesha familia kama hana kitu chochote hata angalu cheti ( elimu ni ufunguo wa maisha!)
Huu ni ukweli jamani hata tukikataa....