Fisi Afanya Mauaji Shinyanga

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
6177314.jpg

Picha kutoka katika maktaba ya nifahamishe
Sunday, January 08, 2012 9:22 PM
Vyombo vya habari vya Tanzania vimeripoti tukio la kuhuzunisha lililotokea mkoani Shinyanga. Tukio hilo linahusiana na fisi aliyevamia na kumnyakua mtoto wa miaka minne na kumjeruhi vibaya kiasi cha kupelekea mtoto huyo apoteze uhai.
Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Diwani Athumani alisema majira ya saa 12 za jioni huko katika kijiji cha Giriku kata ya Bunamhala wilaya ya Bariadi, mtoto Wande Manjale (4) akiwa anacheza na dada yake Sabuhi Manjale (10) mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Giriku walivamiwa na fisi.

Watoto hao wakiwa umbali wa mita 50 kutoka nyumbani kwao walivamiwa na fisi. Fisi huyo alimrukia Wande na kumng’ata shingoni na kukimbia nae vichakani, ndipo dada yake Sabuhi alipopiga kelele za kuomba msaada na baba yao mzee Manjale Giriku (40) alipojitokeza kwa kushirikiana na wananchi wengine kumkimbiza fisi huyo.

Fisi alimuacha mtoto huyo na kukimbilia vichakani baada ya kuwa amemjeruhi kichwani na sehemu za siri na kusababisha kifo chake.

Kwa wasiojua mazingira ya Tanzania wanweza kushangaa sana kusikia habari hizi. Lakini ukweli ni kuwa, vijiji vya Tanzania vina hatari nyngi, na hii ni kutokana na mazingira duni ya vijijini.
 
Teh teh kama wewe una akili ya kichadema mi nina akili ya kibinadamu, nasikia mmepanga maandamano kisa kikwete hajamzuia fisi asing'ate mtu!
 
Hiyo yaitwa human wildlife conflict,maeneo hayo ya bariadi yamepakana na maswa game reserve na Serengeti national park,hivyo matukio ya namna hiyo hutokea
 
Back
Top Bottom