Fisadi wa kwanza wa hii nchi ni hii katiba.. ndugu za bila katiba mpya tunapoteza muda..

baba anjela

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
431
310
Jamani mbona Tanzania tunawasomi wengi ...naona mijadala yote ni Chenge...kikwete...mkapa... Karamagi...accacia....

jamani... hiki ni kipindi kizuri cha kudai katiba mpya ... lazima watanzania tujuwe kucheza na nyakati....

Watanzania mkombozi wa kweli ni Katiba ya Warioba tu...wala si hiyo mikataba...mnayopigia makelele ....

Unapotatua tatizo anza kwenye chanzo ... kwanza utafanikiwa milele... katiba hii ya sasa ni chanzo cha matatizo yote...
 
itafumuliwa tu siku zijazo.

ila tuanze na hayo kwanza

kama itawezekana
mikataba na sheria zinazo tuumiza zifumuliwe
 
Jamani mbona Tanzania tunawasomi wengi ...naona mijadala yote ni Chenge...kikwete...mkapa... Karamagi...accacia....

jamani... hiki ni kipindi kizuri cha kudai katiba mpya ... lazima watanzania tujuwe kucheza na nyakati....

Watanzania mkombozi wa kweli ni Katiba ya Warioba tu...wala si hiyo mikataba...mnayopigia makelele ....

Unapotatua tatizo anza kwenye chanzo ... kwanza utafanikiwa milele... katiba hii ya sasa ni chanzo cha matatizo yote...

Tulia, nchi ngapi zina katiba nzuri ! Na ustaarabu wa watu wenyewe unahusika! Tulia yumalize hili tulilonalo usitutoe kwenye mstari!!!!
 
Jamani mbona Tanzania tunawasomi wengi ...naona mijadala yote ni Chenge...kikwete...mkapa... Karamagi...accacia....

jamani... hiki ni kipindi kizuri cha kudai katiba mpya ... lazima watanzania tujuwe kucheza na nyakati....

Watanzania mkombozi wa kweli ni Katiba ya Warioba tu...wala si hiyo mikataba...mnayopigia makelele ....

Unapotatua tatizo anza kwenye chanzo ... kwanza utafanikiwa milele... katiba hii ya sasa ni chanzo cha matatizo yote...
Nakuunga mkono kwa asilimia mia.Bila katiba mbadala
juhudi zote hizi za rais Magufuli zitatoweka mbele ya macho
yetu na macho ya rais mwenyewe akiwa ameishastaafu
tusipokuwa makini.

Angalia leo anahangaika kujenga viwanda,niulize
vile vilivyojengwa na Nyerere viko wapi? Si ajabu akajenga
akija mwingine asiyeona umuhimu wake akaviuza kwa bei chee.

Ni vyema kutekeleza malengo ya kitaasisi badala
ya mtu binafsi aliyepo kwa wakati huo.
Namaanisha rais ni taasisi,tusipoipa hii taasisi
mipaka ya kikatiba,tutaishia kuona akija rais mwenye
maono nchi inastawi,akija asiyejali anavunja mema yote
ya yule aliyemtangulia anafanya vya kwake.

Ni vema katiba iboreshwe,na rais alazimike
kuifuata katiba ili kulinda maslahi
mazima ya nchi yetu
 
Hii sinema tutaendelea kuchezewa vizazi hadi vizazi. Ikiwa kuna nia ya dhati ya kuitoa nchi hapa ilipokwama nia hiyo itadhihirishwa kwa kuifanyia katiba mabadiliko. Inashangaza leo kuaminishwa kuwa Chenge ni miongoni mwa walioitumbukiza nchi kwenye mgogoro wa madini unaoendelea wakati ndiye aliyekuwa kwenye kamati iliyopendekeza kinga ya Raisi na jambo hilo likashangiliwa kwa sherehe kubwa. Aliyeturoga ni yule aliyefanya tukabadilisha maoni ya wananchi juu ya katiba mpya na kuwawekea kinga watu ambao tulijua kuwa wametuingiza katika mikataba ya hasara. Siamini ninachokishuhudia leo kuwa ni hatua mpya ya mapinduzi au ni muendelezo wa maigizo. Kama ni kweli tumeingia kwenye vita ya kuikomboa nchi kwa nini mchango wa watu fulani unaonekana kutokubalika? Mapendekezo ya Kamati ya pili mbona yamerejea kwa sehemu kubwa kupendekeza yale yaliyokuwa yanapigiwa kelele na kambi ile isiyopendwa? Au mawazo yanakuwa mazuri yanapokuwa hayajatoka moja kwa moja kwa wale wanaodhaniwa kuwa ni maadui? Kama tumeamua kufukua makaburi basi tuyafukue yote vinginevyo itakuwa utaratibu wa kuwatoa kafara wachache kwa nia ya kujisafisha na kuwaacha wengine huru wakati tukijua hao ndiyo kiini cha hao wengine kufanya hayo waliyoyafanya. Hatuwezi kufika kokote kwa utaratibu huu wa kuwa na vipimo viwili kwa kosa linalofanana "Double Standard"

Kuwa na mitazamo tofauti katika jambo linalowagusa wote na hsa tofauti inapokuwa katika namna ya kulitatua ni jambo la kawaida na lenye afya kwa watu wanaoamini katika faida ya uwingi. Waswahili husema penye wengi haliharibiki neno. Kinachofanya neno lisiharibike si uwingi peke yake lakini ni nidhamu ya kupokea maoni tofauti na kuyafanyia kazi. Kuna wanaodhani nchi hii ingeendelea sana kama kusingekuwepo na mawazo mbadala - yaani kama tungekuwa tunawaza kwa namna inayofanana. Tena ipo dhana inayopata nguvu sana siku hizi kuwa wazalendo wa kweli ni wale wasiotoa tahadhari kwa maamuzi ya hatari tunayochukua. Huku ni kurogwa kukubwa pengine kuliko kwingine kokote. Hata katika kipindi cha "Zidumu fikra..." kulikuwepo na waliotofautiana na baadhi ya fikra hizo na ambao leo wasingependa watu watofautiane na fikara zao. Kwa nini?

Tukubali kama nchi kuna mahali tulikosea. Na tukubali kukusanya mawazo yetu yote ili kutengeneza upya ramani ya kule tulikokuwa tunatarajia tufike. Na njia bora ya kufanya hilo ni kurejea mapandekezo ya wananchi kuhusu katiba mpya. Haiwezekani tutumie muda na fedha kuandaa mapendekezo ya katiba ya wananchi halafu iishie katika namna ilivyoishia. Huenda haya yanayoendelea ni laana ya kile tulichofanya kwenye mapendekezo ya katiba mpya. Kuendelea kulalamika kwa nini tumefika hapa bila kufungua mjadala huru kwa watu wote ni kulifanyia dhihaka tatizo tulilo nalo. Mungu Ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom