First time in the city. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

First time in the city.

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Jaguar, Apr 30, 2012.

 1. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa mara ya kwanza maishani mwao,mzee mmoja,mkewe pamoja na mtoto wao mtshepo walitia maguu jijini johanesburg. Walipofika jijini walimwacha mama mtshepo aendelee kufanya shopping supermarket,wao wakaendelea kuosha macho kwa kupita mitaa mbali mbali ya jiji.Mara mtshepo na baba yake wakafika mbele ya jengo fulani refu sana.Chumba cha chini kabisa cha lile jengo ilionekana milango miwili ya rangi ya silver iliyoumana katikati. Mara akafika bibi kizee mmoja,akabonyeza button fulani,ile milango ikaacha mwanya katikati,yule bibi akaingia,ile milango ikajibana tena.Mara wakashuhudia namba kwenye kioo zikiongezeka mpaka #50.Mara tena zile namba zikaanza kupungua mpaka ya chini kabisa,ile milango ikafunguka na akatoka mwanadada mmoja mrembo haswaa.Baba Mtshepo huku akiwa amepigwa na butwaa na kutoyaamini macho yake akasema,"Mtshepo,tafadhali kimbia ukamwite mama yako naye aje aingie kwenye milango hii ili arudi kuwa binti mrembo kama nilivyomuoa miaka 25 iliyopita!".
   
 2. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  teh teh nimeipenda baab!
   
 3. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hahaha iko poa, maana hakujua kuwa ile ni lift.
   
 4. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ndo ivo tena.
   
Loading...