lucasmax
New Member
- Mar 1, 2025
- 1
- 0
FIRST LOVE
Imeandikwa na lucasmax
Ig.lucasmax304
Tiktok.lucasmax304
+255743163081
Episode ya 1
Mama yake alitoa macho mithili ya jambazi lililohukumiwa kunyongwa hakujua ni sababu gani iliyomfanya kijana wake wakiume kuamka asubuhi sana akijiandaa kwenda shule.
Mama huyu ilibidi amuulize mwanae kipi ni chanzo cha mabadiliko hayo.
"Mwanangu kwani kuna mwalimu mpya ambaye ni mkali kupitiliza kaingia shuleni kwenu" Mama aliuliza.
"Hapana mama binadamu tunabadilika leo nimeamua kuwahi shule"aliongea Alex huku akiwa na furaha tere usoni mwake.
Mara kiza kilitanda nyumba nzima jambo liliofanya Shirakawa la umeme tanzania TANESCO kupata matusi mazito kutoka kwa mama Alex lakini gafla haligundua umeme haukukatika ila ulikuwa umeisha katika nyumba yake jambo ambalo lilimuumiza kichwa kwani jana yake aliweka unit moja ambayo kwa matumizi yao ya kila siku ingeweza kuwasogeza siku 3.
"Mama nilisahau kukuambia kuwa jana nilinyoosha nguo zangu kupitia pasi ya umeme hivyo umeme ndo mana umeisha mapema"Alex alitoa maelezo ambayo yaliongeza wasiwasi kwa mama yake kutokana na mabadiliko hayo mazito.
Ni miaka minne tangu Alex ajiunge na shule ya sekondari ya UKOMBOZI hakuwahi kupiga pasi nguo zake hivyo leo hii ni kama miujiza ya gafla anayoshuhudia mama Alex ukiacha ile ya kuwahi shule kwa mtoto wake.
Mabadiliko makubwa ya Alex haikumshangaza mama Alex pekee kwani hata walimu na wanafunzi wenzake walijiuliza kijana huyo wa kidato cha nne amepata uponyani huo katika madhabahu gani.
Akiwa amewahi kuliko kawaida yake macho yake yaliangaza huko na kule kama fukara aliyeangusha pesa ambayo hakuwahi kumiliki hapo mwanzo.
Mara macho yake yaliganda sehemu moja zilipita dakika 5 mapigo ya moyo wake yalienda mbio zaidi ya mbio ambayo ungeitoa msomaji wangu pale ungekutana na kiumbe cha ajabu.
Hii ndo siri ya mabadiliko ya kijana Alex ni msichana wa kishua mweupe ambaye wembamba wake ulifanya mipangilio ya viungo katika mwili wake uwe katika mtiririko mzuri,alufu nzuri ya mwili wake haikuwaacha salama wanafunzi wakiume wa shule hiyo.
Sio tu wanafunzi wenzake pia walimu wakiume wa shule hiyo ya sekondari walimfwata lakini wote waliangukia pua.haikuhitaji umuangalie Mara mbili huthibitishe urembo wa msichana huyu wa kitajiri.
Ilikuwa Fimbo ya sita ikikita katika makalio ya Alex lakini hata hakujali kwani akili na macho yake ilikuwa vinamuwaza yule msichana mpaka pale ilipomkuta Fimbo iliyojaa uzito vizuri ilipokita kwenye mgongo wake ndipo Alex alipo rudi kwenye ulimwengu huu wenye safari tisa ambayo moja ilipoteza sifa na kuziacha sayari nane zikilizunguka jua.
Ndani ya darasa ambalo Alex alikuwa anasoma ni form 4 B kama kawaida la hili darasa linabeba aina nyingi ya wanafunzi.kikundi cha wanafunzi wakiume waliweka kikao Chao cha kila siku asubuhi ambapo hupiga story za mpira mpaka pale ambapo mwalimu wa some husika atakapoingia darasani.kikao hiki kimebeba wanafunzi wengi akiwemo Alex,suma ambaye ni rafiki mkubwa wa Alex pia bila kusahau cosmas,justin na erasto na leo walikuwa wakichambua mchezo wa watani wa jadi kati ya simba na yanga uliokuwa ukitarajiwa kupigwa mwisho wa wiki.
PENDO huyu ndo binti aliyembadilisha Alex kimaisha yeye pia alikuwa akipiga story zao za kike na rafiki ake mkubwa machepele wa jiji aliyeitwa Veronica
Veronica alisifika kwa tabia za kiswahili darasani hapo alikuwa ni mama maneno lakini alikuwa na urafiki mkubwa na mtoto wa kishua pendo aliyewaliza wavulana wengi kwa urembo wake wa asili.
Gafla upepo wa darasa hilo ulibadilika na kuwa kimbunga kizito baada ya kusikika sauti ya mwanafunzi mmoja akisema mwalimu wa somo la mathematics anakuja.
Hapa ndipo wanafunzi wa hili darasa B wanaosifika kwa ukaidi na matokeo mabovu hapo shuleni walianza kuangaika na kuzipotezea story za uchambuzi wa mpira na story za wasanii huku wale wa kusimuliana movie mbalimbali wakitafuta pakukimbilia.
"Oya kumbe jana teacher mathe aliacha maswali mwanangu"
"Oya umefanya"
"Dah mwanangu mimi nilitaka kufanya kila swali nalogusa nikawa sielewi nikaacha"haya yalikuwa maongezi ya baadhi ya wanafunzi hapo darasani.
"Kiongozi wa darasa Alex tafadhari kusanya madaftari ya mathe sasa hivi na asiye kusanya daftari amekwisha"ulikuwa mkwala mzito wa mwalimu wa somo la hisabati uliyoacha mitetemo kwenye matumbo ya wanafunzi huku wengine wakishindwa kujizuia kuonesha hofu iliyowakumba katika miili yao.
Sura ya mwalimu huyu haikuonesha hata chembe ya masihara huku macho yake yakimtoka kilichowaacha hoi wanafunzi ni ile fimbo yenye muonekano wa kutisha jambo liliowafanya wanafunzi wale kuvuta picha kama ile fimbo ikitua kwenye ngozi yao itakuwaje?
Hakika zilikuwa ni muda wa kuchukia shule mwalimu aligundua hata kiongozi wa darasa hilo Alex hakuwa na hata hilo daftari la mathematics lakini kwa kuwa hilo darasa lilijulikana kwa tabia hizo hivyo halikumshangaza mwalimu.
"Najua hakuna aliyefanya kazi yangu sasa ikifika saa 4 naomba kiongozi wa darasa ukusanye madaftari sawa"ni kauli ya mwalimu iliyowafanya wanafunzi wacheke kimoyomoyo.
Nyuma ya kiti cha Alex ndipo alipokaa binti mrembo pendo ambaye Alex alimpenda lakini kwa kuwa hali ya kimaisha ya Alex haifanani na ya pendo ilimfanya Alex kusita kumfwata.pia rafiki yake Alex ambaye alikuwa ni suma alikuwa na familia yenye uwezo kiuchumi hii ilisababisha kuwa na mazoea na pendo jambo lililosababisha kila mwanafunzi kunua suma na pendo ni wapenzi lakini haikuwa kweli.
Hatimae kipindi bora kwa wanafunzi kikafika hiki si kingine ni kili cha mapumziko kama kawaida watoto wakiume waliwahi sehemu ya msosi kwa ajili ya kuweka oda ya chakula chao pendwa ambacho ni BANGUADI.
BANGUADI ni ukoko wa wali wanafunzi wakiume ukipenda chakula hiki kwasababu ni bei nafuu lakini unajaziwa sahani.
Alex aliona fursa ya kuwa na pendo haiwezekani kulingana na maisha yao kuwa na tofauti kubwa pia pendo ilisemekana kuwa anatoka kimapenzi na rafiki yake suma na yeye aliamini kuwa ni kweli kwani mara nyingi aliwaona wapo pamoja.
Jioni shuleni hapo ikiwa masomo yote yameisha na wanafunzi wakianza kwenda nyumbani
Alex alikuwa amekaa na rafiki yake mwingine mudy ambaye alikuwa ni mpole darasani wakipiga story lakini gafla sauti nyororo iliyojirudia mara kumi kwenye masikio ya Alex ilisikika
"Mambo alex"ilikuwa sauti ya kimalaika iliyotamkwa na Pendo.
Ilibidi Alex achukue dakika kadhaa kuthibitisha kama yeye ndio mlengwa wa salamu hiyo kutoka kwa mrembo huyo..........
FIRST LOVE
Imeandikwa na lucasmax304
Ig.lucasmax304
Tiktok.lucasmax304
+255743163081
ITAENDELEA