Tafuta semina ya mchungaji Christopher Mwakasege juu ya mtoto wa kwanza.Anasema kuna vita kubwa sana kati ya shetani na uzao wa kwanza,mara nyingi mtoto wa kwanza huwa ni tatizo...sijui ni kwanini....Lakini hebu tuanze na uzao wa kwanza kabisa duniani wa Adam na Hawa ambae ni Kaini, Kaini alimuua mdogo wake kwasababu ya wivu,mdogo wake alifanya vizuri kuliko kaka yake ikawa bifu zito.Twende uzao ya Isaka..Esau na Yakobo,ilitokea timbwili kubwa sana baada ya Yakobo kubarikwa badala ya Esau,kwa kuogopa kuuliwa na kaka yake Yakobo ilimbidi akimbie nyumbani miaka na miaka..Uzao wa Yakobo, Yusuph ambae sio mtoto wa kwanza wa yakobo alifanya vizuri kuliko kaka zake wakataka kumuua.Na hata uzao wa Yesse,Daud alifanya vizuri kuliko kaka zake.The list is endless... Hivyo basi unaweza kuona watoto wa kwanza huwa hawafanyi vizuri sana,sijui ni kwanini.Lakini mchungaji Mwakasege anasema ni kwasababu ya kuwa mtoto wa kwanza ni malango ya wazazi.Hivyo shetani hupiga vita kubwa sana malango hayo.Hivyo ni vema sana kuwaombea na kuwasaidia