Sifa ya database ni kutunza kumbukumbu kulingana na zilivyohifadhiwa, kwa mantiki hiyo alama za vidole zilizohifadhiwa katika mfumo haziwezi futika labda itokee mfumo umeleta hitilafu, kuna uvamizi wa kimtandao ulioharibu data, kuharibika kwa storage system beyond repair n.k
Alama za vidole zilizo katika vidole vya kila mmoja wetu nazo huwa hazibadiliki isipokuwa kuwe na external factor, mfano mtu anayetumia sana mikono pasipo kufunika ncha ya vidole vyake kuna muda hupoteza patterns za fingerprints, lakini kwa puwa ngozi huwa inajirekebisha basi alama hizo hurudia hali yake baada ya muda...
Kwa mtu ambaye ameungua vidole, kapata matatizo ya kiafya yenye kuharibu ngozi n.k, mtu huyu anaweza kupoteza kwa kiasi kikubwa alama za vidole vyake...