Labda kwa sababu tunawa-spoil sana. Tunawasikiliza. Karibu kila wakitakacho tunawapa. Hatujui kusema hapana (hivi baba utaanzaje kusema hapana binti yako akikuomba umnunulie hereni za almasi?).
Hatutaki wanune. Hatupendi kuwaona hawana furaha. Tunataka muda wote wawe na furaha tu. Tunapenda kuwaona wakiwa wamependeza. Nywele ziko vizuri. Nguo nzuri.
Tunapenda kuona wanafanikiwa katika yote mema watakayo kufanya. Tunajivunia kuwaona wakifanya vizuri shuleni. Tunafarijika tukiwaona wakiwa kwenye mkondo sahihi maishani.
Naweza kuandika kitabu kizima kuhusu kwa nini binti ananipenda kuliko hata maisha yenyewe!
Owh ahsante sana hii naona sana kwa binti yangu na baba ake its beautiful....
Shukraan Nyani Ngabu
Last edited by a moderator: