FINCA ni ya wa finland?

Mutual fund watu walishakiria halafu wakadhurumiana. Umeshawahi kusikia kitu kinaitwa NICOL?

Sasa hivi ni ngumu sana kuwaconvince watu, labda within your circle of friends.


Ni ngumu ndio lakini ndio moja ya vitu ambavyo vitatutoa kwa kweli na kwa population yetu ilivyo ni bonge la plan

watu wengine wakiharibu sio kila mtu ataharibu kipindi kile benki ya meridian ilivyyeyuka watu wasingeweka accounts basi kwenye benki zingine

cha msingi serikali itambue uwepo wa hizi Mutual Funds zitungwe sheria ambazo zitazi monitor
sema kwa sisi nchi zinazoendelea hizo pesa za mutual funds zisiwekwe kwenye stocks kama giant countries wanavyofanya

ziwekwe kwenye miradi mbali mbali ambayo zitawalisha wawekezaji haya vizazi na vizazi


MRADI WA KIGAMBONI serikali ingeweza kuujenga kwa kutumia Mutual Funds za Watanzania

TRUST ME
 


Mutual funds zikoje?
zinatoa mikopo?
hazina riba?
lazima serikali ianzishe?
mtu binafsi hawezi anzisha?
 


Mutual funds zikoje?
zinatoa mikopo?
hazina riba?
lazima serikali ianzishe?
mtu binafsi hawezi anzisha?
 
Mutual funds zikoje?
zinatoa mikopo?
hazina riba?
lazima serikali ianzishe?
mtu binafsi hawezi anzisha?

Mutual funds simply means kwamba kikundi cha watu kinachanga pesa na kufanya biashara.

Kinaweza kuamua kununua hisa kwenye makampuni yaliyosajiliwa, kinaweza kuanzisha biashara zake, kinaweza kuinga ubia, inaweza kufungua fixed deposit acc, kinaweza kununua treasury bills etc.

Mfano wake ni NICOL ambayo sasa hivi account zake zimefungiwa kwa sababu imeshindwa kujiendesha kwa kufuata taratibu.

Story na NICOL ni ndefe lakini in a nutshell ni kwamba viongozi wa NICOL ni Mengi na wenzake, later NICOL ikanunua kiwanda cha mdogo wake Mengi kwa bei kubwa kuliko thamani ya kiwanda kinyume na ushauri wa consultants. Jambo hilo pamoja na maamuzi mengine yasiyo sahihi yamesababisha NICOL kufirisika.

Ukiangalia utaona watu kama Mengi ambao biashara zao zinaenda vizuri kwa mafanikio lakini wanapoongoza biashara ya wengi tayari wanajifanya hawana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi! Hii ni dalili ya ubinafsi na ndio sababu watu hawataki kushiriki kwenye biashara za watu wengi wasiowafahamu.

Mimi ninaadvocate vikundi vya watu wanaofahamiana vya watu kati ya 50-100. Nilishaandika mradi unaitwa 100 millionaires project na kuwapa vijana. hata hivyo vijana walikuwa wazito kwenye utekelezaji. Mradi ulitaka kila kijana achange sh. mil 10 ili wakiwa 100 wapate sh. bil 1 na kuanzisha bishara ya maana. mnaona Dewji alianza na almost the same amount lakini sasa hivi ana revenue ambayo ni about 3% ya GDP ya Tanzania! Just imagine vijana 100 wangeweza kujijengea uwezo wa aina hiyo, isnt that amazing?

Ili biashara za watu wengi au vikundi zifanikiwe ni lazima kuwe na wachache kati yao ambao ndio wanaotekeleza mipango ya pamoja na kuisimamia kwa moyo wote. Biashara haiwezi kuendeshwa kama vyama vya siasa. NICOL iliendeshwa kama chama cha siasa, ndio maana ikafirisika.
 
Ilianza kama MicRofinance. Office zao zipo based in Manzese mda mrefu sana. Origin yake sijajua ya wApi kwa kweli.
Cheki kwenye web yao u might get the details.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Ni Magomeni Mwembechai
 

Usipo piga ulevi wa ccm kumbe akili unazo.
 
FINCA is a non-profit, tax-exempt charitable organization under Section 501(c)(3) of the United States Internal Revenue Code. Donations are tax-deductible. ©2013

1101 14th Street NW, 11th Floor, Washington, DC 20005
P 202.682.1510
info@FINCA.org
​
 
Kaka kampuni hii ni ya wamarekani

FINCA is a non-profit, tax-exempt charitable organization under Section 501(c)(3) of the United States Internal Revenue Code. Donations are tax-deductible. ©2013

1101 14th Street NW, 11th Floor, Washington, DC 20005 ​
P 202.682.1510 ​
​
info@FINCA.org

 

Ha ha ha mkuu umeua, KFC ya bongo ni usanii sio original ya kentuky inayoo operate world wide,

Kinachoshangaza cha kwanza KFC ya Dar es salaam ina Coca cola umbrella kwenye restourant yake wakati ki uhalisia KFC anafanya biashara na Pepsi kwenye refreshment na Pepsi Co. Ni shareholder wa KFC, unaweza pitia wikipedia ay google for more details..

Tembea popote duniani kama utaona KFC anatumia coca cola beverages but ya bongo hadi miamvuli wamechukua Coca cola
 
ni wa American
 
Kwa hapa kwetu safari ya maendeleo bado ni ndefu sana.
 
Ilianza kama MicRofinance. Office zao zipo based in Manzese mda mrefu sana. Origin yake sijajua ya wApi kwa kweli.
Cheki kwenye web yao u might get the details.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Sio manzese ni magomeni mwembe chai
 

FINCA haijawahi kuwa NGO,NGO husajiriwa wizara ya mambo ya ndani.

Finca imesajiriwa brela kama a limited by gurantee company toka iliponza operations zake hapa mwanzoni mwa miaka ya tisini.

Ni kampuni iliyokuwa ikimilikiwa asilimia mia moja na wamarekani,hasa mmarekani mmoja anaitwa lupert kama sikosei.

FINCA kwa sasa sio bank,kwa mujibu wa sheria zetu,Bank ni taasisi ya fedha inayomaintain current accounts kwa wataje wake,FINCA ni deposit taking Microfinance institutions.

Kwa sasa,FINCA ni limited by shares company ambayo majority shareholder ni FINCA International PLC na hakuna mtanzania hata mmoja ambaye ni shareholder.
 
yaan huwa sitaki hata kuwasikia hao finca ki ukweli wanatumia umasikini wa watu kuwapa mkopo,mimi ni shahidi in my family.walikopesha kama kikundi pale kijijini kwetu then wale wakagawana kila mtu afanye biashara anayoona but week ya pili from siku wamepewa mkopo walitakiwa kuanza kulipa mkopo huo kiasi kwamba wengi walijikuta wanazirdisha hizo hela kuzilipa na hakuna biashara waliyoanzisha na bado wakawapora vitu vyao vya ndani,mimi mama yangu hadi walichukua simu yake ya tochi kuiuza aweze kulipa rejesho la week ilifika hadi kipindi wakataka kuuza nyumba yetu kisa wameshindwa kulipa kwa wakati niliingilia kati nikawaambia nyumba ya watoto wawachukue waliowakopesha hiyo ikaishia hapo.kikweli watu wanaonewa sana na hawa finca mara pride unawatia umasikini mara mia zaidi na kuacha mtafaruku kwenye familia za watu...
 

Acha pumba kiongozi.
Sijui unaposema FINCA inariba kubwa sana unakuwa unafananisha na riba ipi?

FINCA haijawahi kuwa na mabounser toka itie mguu nchi hii miaka ya mwanzo ya tisini acha kuongea mambo ya kwenye bao kwenye issue serious.

Na wala haijawahi kuwa na mkopo unaofikia interest ya asilimia 5%,wewe inaonyesha hauelewi hata kidogo microfinance zinavyofanya kazi na theories & facts behinds their practices.

FINCA ni microfinance company inayoendeshwa kwa umakini wa hali ya juu kuliko hata baadhi ya mabank sasa sielewi hizi lugha za kebehi unazitumiaje juu yake.
 

Tatizo lako umeoea kubishana.
Tuambie FINCA interest yake ni kiasi gani?
Iwapo mtu atashindwa kulipa FINCA wanamfanya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…