Filikunjombe: wabunge wa CCM waoga wanajipendekeza kwa chama badala kwa wananchi

Huyu anasumbuliwa na ULANZI; anajitafutia misifa ambayo itamtokea puani. Kama anataka kutoka CCM atuachie chama chetu kiusalama, hana sababu ya kuwadhalilisha wabunge wetu

Wewe Na Mwenyekiti wako ndiyo mmelewa ulanzi...tabu yenu hampendi kuambiwa ukweli!
 
Huyu anasumbuliwa na ULANZI; anajitafutia misifa ambayo itamtokea puani. Kama anataka kutoka CCM atuachie chama chetu kiusalama, hana sababu ya kuwadhalilisha wabunge wetu
Umeaidiwa nini mpaka ukapiga debe hivyo usijijua? eti Chama chetu ndio nyie mazuri wanakula wenyewe wewe unakauka koo tuu ebu amkaa uone nchi za wenzenu zinavyoendelea husafiri hata TV huangalii??? loh fisadi wa maendeleo yako na yawenzio...
 
Au ccm wAtamwambia wakati wa kuzaliwa alitanguliza miguu badala ya kichwa hivyo hafai
Endelea kumkubali kwakuwa safari yake ya kuhamia cdm imeanza siku ile aliyoweka siignature kwenye karatasi ya zitto. uchaguzi ujao magamba watamshibuda tu. kama hawatasema ana uraia wa botswana na hajaukana watasema utotoni aliugua degedege hivyo hafai kumbea. ndio hapo ss atakapohamia cdm
 
Huyu anasumbuliwa na ULANZI; anajitafutia misifa ambayo itamtokea puani. Kama anataka kutoka CCM atuachie chama chetu kiusalama, hana sababu ya kuwadhalilisha wabunge wetu

Magamba utawajua tu mapovu yanavyowatoka ukiwagusa
 
Huyu mlima viazi kuna siku alimanusura apigwe na wabunge wa Chadema kisa kuwa aambia wanapinga mno!!!!!!

Sasa aombe msamaha live kwa makamanda, la sivyo bado ntamwona mnafiki pia....!!!! atoke basi CCM tuje tujenge Kikosi cha maana!

alikua HAJAKUA
 
Ulanzi ni kinywaji kizuri sana na sidhani kama kina mdhala.Deo sidhani kama amewadhalilisha hao wabunge wenu isipokuwa kawaambia ukweli kwani nijukumu lake kusema ukweli.kwani kweli mara zote hutuweka huru.mwacheni aseme ukweli siku moja utawakomboa msipende kujidanganya someni alama za nyakati msiishi

Deo anajenda ya siri baada ya kuona upepo sio mzuri kwake kwa uchaguzi ujao hata hivyo shida hii haipo kwake tu bali kwa wabunge wote wa chama kikongwe, wanakaubinafsi na alwys kupanga mbinu mpya kuendelea kubaki kwenye nafasi zao, iwe kwa kuwaibia wananchi au kwa kuwafurahisha wananchi, lakini jambo moja zuri ni kwamba kwa kuhangaika kwao ili kuendelea kubaki iwe ni kupitia chama kikongwe au chama kingine chenye kuonyesha matumaini kwao, ukiwasikiliza kina Filikunjombe unaweza kufikiri wanania njema na nchi hii lakini nionvyo mimi ni mipango ile ile ya kuendelea kuhodhi nafasi walizo nazo wako tayari hata kuhama chama kama watahakikishiwa kuendelea kuhodhi nafasi walizonazo ukiona wanacharurani wa chma kikongwe ujue huko ndani hakuna uhakika tena wa keundelea kuhodhi nafasi walizo nazo hata hivyo kulumbana kwao sisi wananchi tunazidi kuwafahamu na tuanzidi kujua wanasiasa wa bongo wailivyowabinafsi na siku moja watanzania wataweza kufanya mageuzi ya kweli kiuchumi kisiasa na kijamii kwa kuweka mifumo itakayowawajibisha viongozi sehemu zao za kazi
 
kweli akili ni mali,mbona hata wabunge wa chadema wanaogopa chama kuliko wananchi. ulimbukeni una msumbua filikunjombe
 
Source Mtanzania

Mh mbunge Filikunjombe kawachana wabunge wa CCM na kuwaita waoga na wanafiki kwa kuogopa chama zaidi kuliko wananchi walio watuma bungeni.

Hayo yamejiri baada ya wabunge hao kuwa waoga kutia saini ya kutokuwa na imani na waziri mkuu pinda na kukaa kuzungumzia mambo hayo chini chini.

Mbaya zaidi wamekuwa wabunge wa kujipendekeza kwa chama na viongozi wake na kuwatupa wananchi wao.

My take

Sishangai ndo maana hata JK kashindwa kuvunja baraza hadi apate idhini ya chama

huyu mbunge ajue uwaziri ameukosa...wenzie wamekaa kimya hawakusign ile form coz wanavizia uwaziri hili baraza la sasa likivunjwa...watu wana akili huko bungeni lazima kula wapokezane sasa hivi ni zamu ya wengine
 
ujumbe huu umfikie mbunge wetu wa kigamboni mh kingwendulile, kwa hili ni wazi kabisa umetuaibisha pia umetusaliti tulokupa kura,
umeamua kuwaunga mkono mafisadi wanaotuletea maisha magumu watanzania na kukataa kusaini waraka wa kumg'oa waziri mkuu kwa kushindwa kuwajibika na kuamua kuunga mkono ccm na kutupuuza sisi,
na kama uko dhati kutuudumia wananchi wa kigamboni tunaomba majibu kwa nini hukusaini na kwanini tusikuchukulie kama mbunge mfuata mkumbo
mwisho tunaomba munguuko mbeleni atupe mbunge jasiri aliye tayari kuwatumikia wananchi na si anayejipendekeza kwa mafisadi na pia mchumia tumbo

sio mbunge wa kigamboni tu.wabunge wote dar ni waunga mkono ufisadi waondoeni hao magamba 2015
 
Kwani cdm kuna mbunge yupi ambae unaweza kumlinganisha na jembe letu Filikunjombe

Huyo huwezi kumlinganisha na majembe mbali ya CHADEMA labda 2mfananishe na mbunge wa Rombo Joseph Selasini ndo saizi yake.
 
for sure ushabiki wa vyama utatuponza tujaribu kubadili njano kuwa nyekundu,ccm hakuna wabunge mahiri ni wanafiki tu kwa waliowachagua wanaogopa kivuli chao,pamoja na kwamba hata upinzani nao si wakweli sana ila wanajitahidi kuwa jirani na kuwatetea waliowachagua, nafikiri kauli ya masabuli kuwa wabunge wanafiri kwam kutumia ........... iliwalenga sana wa chama tawala ccm
 
ujumbe huu umfikie mbunge wetu wa kigamboni mh kingwendulile, kwa hili ni wazi kabisa umetuaibisha pia umetusaliti tulokupa kura,
umeamua kuwaunga mkono mafisadi wanaotuletea maisha magumu watanzania na kukataa kusaini waraka wa kumg'oa waziri mkuu kwa kushindwa kuwajibika na kuamua kuunga mkono ccm na kutupuuza sisi,
na kama uko dhati kutuudumia wananchi wa kigamboni tunaomba majibu kwa nini hukusaini na kwanini tusikuchukulie kama mbunge mfuata mkumbo
mwisho tunaomba munguuko mbeleni atupe mbunge jasiri aliye tayari kuwatumikia wananchi na si anayejipendekeza kwa mafisadi na pia mchumia tumbo

Huyu jamaa hata mimi nilimuuliza kwanini hakutia sahihi, kaogopa kujibu, kwa kweli kwa mbunge kijana ambaye tulimuamini ametutia aibu.. ni mnafiki naweza sema kwa uhakika... na hili doa hawezi kulitoa, anadai hakuwa Dodoma, je alipofika Jtatu, mbona hakufanya hivyo kama mpaka Mkono aliamua kufanya jambo sahihi... unafiki na uchumia tumbo period!
 
Nadhani hapa anamsema H. Kigwangala anayesubiri uwaziri mkuu kwa kutumia jasho kidoogo tu, yaani kutoa sababu za kwa nini hakusaini.
 
Back
Top Bottom