Filikunjombe: Serikali ya CCM imevaa miwani ya mbao

Filikunjombe: Serikali ya CCM imevaa miwani ya mbao

Aangalie wasije wakam ulimboka na kumkibanda hawa jamaa wameshakuwa hatari sana ase!
 
Nimefurahishwa sana na namna ambavyo mbunge wa Ludewa Mh Deo Filikunjombe anavyofanya siasa zake.

Mtazamo wake kisiasa ambao kimsingi umejikita kwenye maslahi ya wananchi na sio matakwa ya chama chake, msimamo thabiti alionao wa kusema bila uoga kile anachokiamini kwamba ni sahihi, mtazamo wake kuhusu vyama vya upinzani na mambo mengine, vinaonyesha kwamba mh.Deo amekomaa vizuri kisiasa sana sana siasa hizi za mfumo wa vyama vingi.

Nikiri kwamba ni muda mfupi tangu nimfahamu Mh Deo ila kwa muda hui mfupi nimemsoma kwamba huwa hafanyi mambo ya siasa kwa kufuata upepo bali anafanya kwa kuzingatia matakwa ya wananchi wake, taifa kwa ujumla na utashi wake wa kutambua jema na baya.

Mtazamo wake kuhusu vyama vya upinzani pamoja na ujasiri wake wa wazi wa Kukataa kupitisha jambo ambalo kwa utashi wake anaona halikidhi vigezo kama alivyofanya leo asubuhi bungeni pamoja na mambo ambayo nimeyaeleza hapo juu ndivyo vilivyo nisukuma kuandika uzi huu. Napenda kuwashauri wabunge wengine wa Chama tawala kama kweli wanataka chama chao kiendelee kuongoza nchi hii basi wabadilike. waweke mbele maslahi ya nchi kuliko ya chama, wachangie hoja basipo kuegemea upande wa chama bali upande wa taifa, wazichunguze hoja za wapinzani na kuzifanyia kazi sio kubeza kwa misingi ya utofauti wa vyama. Pia ushauri huo huo unafaa kwa vyama vya upinzani.

Hakika Mh Deo ni mfano wa kuigwa hasa hasa kwa wabunge wa chama tawala.
 
Wabunge wa CCM Tanganyika wengi moyoni hawafurahii deal ya Bagamoyo
 
Mungu amulinde Filikunjombe,maana yale magaidi ya ccm yakina Nchemba yasije yakampa sumu au kumbambikia hata madawa ya kulevya......maana ccm huwa hawawataki watu kama Deo filikunjombe maana ni mwiba kwa kina Nchemba
 
This is what it means to be peoplessssss power!!BIG UP D.F.K
 
Wazee wa Ludewa wameshamuambia kuwa kama anataka kurudi bungeni 2015 sharti lazima ajiunge na CHADEMA lakini kama ataendelea kuwa katika CHAMA CHA MAFISADI bungeni 2015 hawampeleki.
 
Kama CCM kuna Somo la Unafiki basi Deo hakuelewa

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Miwani ya mbao ni tinted full ili uweze kuona unahitaji seremala mwaminifu atakaye toboa taratibu bila kukujeruhi kazi hiyo ni nzito badala yake bora kubadili wasio na miwani wanaoona vizuri bila matatizo.

Namshukuru sana Mh Kinana amewaambia CCM wasibeze kila kitu toka kwa wapinzani. Kama wanaweza kukubaliana nami ni kwamba ushindi wa Jimbo la Ubungo kwa mfano ulikuwa simple and clear kwasababu Hawa Ng'umbi alihamaki sana sasa hawa wamekuwa wakihamaki kila wanapoelezwa jambo hii inawapa mwanya mzuri sana Chadema.

Hizi kesi zilizopo mahakamani badala ya kuibomoa Chadema zimeiweka Chadema kwenye chart nzuri sana kwani wananchi kwa ahadi fake ambazo serikali ilizitoa na bado hazijatekelezwa ukiondoa yale ya Loliondo, wananchi wametokwa na imani kwa CCM.
Ni kwali kabisa, kuna kila dalili ya upinzani wa kweli kutokea CCM. Ni vizuri basi tukamfuata Mhe. Deo huko huko, hivi akina deo wangelikuwa watano ccm ingelikuwaje. Karibuni Magwanda.
 
jamani mbona mimi naona kuwa mizengo pinda anafanya kazi yachuchota maji katika kisima na kujaza baharini?
 
jamani mbona mimi naona kuwa mizengo pinda kazi yachuchota maji katika kisima na kujaza baharini?
 
Wabunge na Kiongozi wa Mfano huu wa Deo ndio unaotakiwa, Haijalishi upo Chama gani, Maslahi ya Taifa na Wananchi Kwanza. Mungu azidi kumpigania Mbunge Deo na wengine wote wanaoweka Maslahi ya Taifa mbele.


Yaani kweli Bungeni ukuwasema wapinzani kwa lugha mbaya unasifiwa, kama jana Mkamia alivyoendelea baada ya kumtukana Sugu, leo Filikunjombe kalazimishwa kutoa neno miwani ya Mbao, ila ndo hivyo Waziri Mkuu hapo anapata machungu na kukumbuka yale majina ya wabunge waliosaini kutokuwa na imani naye, Filikunjombe alikuwa muwazi na si mnafiki kama wengine:rockon:
 
deo ni mbunge hasa wa kuchaguliwa.....anajua nini maana ya uwakilishi bungeni hana unafiki kama mwigulu...
 
Back
Top Bottom