Filikunjombe: Serikali ya CCM imevaa miwani ya mbao

Filikunjombe: Serikali ya CCM imevaa miwani ya mbao

Kwa kweli mbunge Filikunjombe anafaa kuwa mfano wa kuigwa kwa wabunge wote wa CCM, kwa kuwa yeye siku zofe amekuwa anaweka mbele maslahi ya Taifa, kuliko kufikiria ushabiki wa chama chake!

Na yeye ni miongoni mwa wabunge wachache sana wa CCM wanaojua kuwa wajibu wao no. 1 wakiwa bungeni ni kuisimamia serikali, kwa maana hiyo ni wajibu wao kuikosoa serkali inapokuwa haitimizi wajibu wake ipasavyo, tofauti na wsbunge wengine wa CCM, ambao wanaamini kuikisoa serikali ya CCM ni sawasawa na kuwa msaliti wa chama chako!!

Big up Filikunjombe, you are really a role model!!
 
filikunjombe huwa ananifurahisha sana penye kosa anasema hapa pana kosa na penye kusifia anasema hapa pamefanyika jambo zuri.
hii ndivyo inavyotakiwa
 
nataman angekuwa mbunge wangu shinyanga. hivi Iramba hamuhitaji mtu kama huyu?????????!!!!!!!!
 
Wabunge wa ccm jihadharini, sisi huku nje tunaona mbivu na mbichi.upuuzi mnaotufanyia sisi wananchi utawaponza 2015,tumechoka na mipasho yenu ya kila mwaka,badala ya kujenga hoja yenye nguvu,mnajenga upumbaaavu wa kijiweni,na huku mnakula fedha ya walala hoi(kodi) zetu,kwa kuzungumza matusi ya nguoni,na ya kudharirisha utu wa mtanganyika. Sasa Tumechoka kusikiliza upuuzi wenu,Hivyo ndivo tuliwatuma?Laana ya machozi ya maskini,yatima na wajane itawakalia juu ya vichwa vyenu pamoja na watoto wenu hadi vitukuu.
 
Hawa wanaotukana ni kuwa wanafanya kazi ya Nape, sasa mnataka nape afanye kazi gani?? [/SIZE]

heshima kwake FN, hakika next tym magamba nec hawatampitisha kwenye kura za maoni, lakini asihofu, jimbo ni lake hadi atakapolikataa mwenyewe. big up FN.
aisee kumbe hata magamba wanajua kuwa nn kapewa kazi ya domo! maana boda ana domo sijapata kuona, sijui ccm wamemtafutia mouth wash gani akitaka kula asukutue kwanza, maana bila hivyo akila bila kusukutua anaweza kupata maradhi ya tumbo yasiyotibika. kinywa kichafu sn sijaona tena.
 
Na huenda wapo wengi kama yeye ila wanasubiria nani aanze. Usishangae nao wanafuata mmoja mmoja!
 
Mabadiliko ya kweli yataletwa na vijana bila kujali itikadi. Imani yangu ni kuwa kila kijana mtanzania ana jukumu fulani la kufanya katika kuleta mabadiliko. Ni wakati wa vijana wanao FIKIRI Kukata shauri. Chukueni naafasi zote zenye kuhusika na maamuzi makubwa kitaifa hususani UDIWANI na UBUNGE ili mabadiliko ya kweli yafanyike. Ni kwa kuingia huko tu ndiko kutakakotokea mabadiliko ya kweli kitaifa. Vijana jiungeni na siasa mkafanye mabadiliko bila kujali ni chama gani kwani mabadiliko ya kweli yatatoka katika vyama vya siasa. Kutakuwa na tatizo kama vyama vingine vya siasa havitakuwa na vijana wenye akili ni vizuri hata kujiunga na CCM ili kusaidiana na Mhe. DEO

mkuu inaelekea huijui ccm ndani na nje ukiingia kule hata kama una akili kama Newton unaambiwa acha akili nyumbani si unaona maprofessor ma phd holder ambao ni wabunge na mawaziri wa ccm wanavoshabikia hata mambo ya kipuuzi ili mradi ni ya chama chao? mfano huyu deo unafikiri kuna mtu anakaribisha mawazo yake ndani ya ccm??
 
Deo is sailing in the wrong boat. Angalia usije toswa kwenye kina kirefu. Think twice. Darasa unalosomea hivi sasa halikufai. Inabidi kurushwa madarasa.
 
There are currently 544 users browsing this thread. (86 members and 458 guests)
 
Tunatakiwa kuelewa siasa si ugomvi siasa haijaletwa kuwatenganisha watanzania,wapinzani na chama tawala lazima tuelewe TANZANIA ni muhimu kuliko vyama vyetu,vyama vinapita tu hapa TANZANIA,tokea harakati za uhuru mpaka leo kuliwa na vyama na vingine vimebaki historia,ningetegemea wabunge wetu wangepigania ustawi wa jamii ya watanzania kuliko vyama vyao,wanasahu wananchi na kuweka mbele vyama,haikubaliki hata kidogo
 
Big up deo!Naamin mungu alimpa akili,busara na uwezo wa kutambua kzur na kibaya..!wote wangekuwa km huyu nicngeona aja ya kuwa chadema wkt mcmamo inayotakiwa inafuatwap!
 
Wabunge wa CCM wameacha kile walihotumwa na wananchi sasa wanafanya yao,kazi yao kubwa sasa ni kupambana na wale wote wanaotetea maslahi ya wanyonge na hasa chadema,namkubali sana Deo Filikunjombe Ni mmoja kati ya wabunge wa CCM mwenye kuipenda nchi yake na kuweka chama pembeni.2015 watamtosa kwa sababu tu sio mnafiki,watamtosa kwa sababu anasema ukweli,watamtosa kwa sababu anatetea maslahi ya wananchi na sio maslahi ya chama,watamtosa kwa sababu si mwenzao!

Hongera Deo,Watanzania watakukumbuka kwa kuwatendea wema na si kitu kingine!
 
Unapokuwa na mbunge kama Deo Filikunjombe jimboni kwako hata CCM wasipopeleka maendeleo huko bado una sababu ya kujivunia kwamba una mbunge anayejitambua. Anajua alichotumwa na Walalahoi wa kule Ludewa. Anaipenda nchi yake na mzalendo wa kweli hana unafiki ndani yake, anajua anachosema na anakiamini ni mkweli nafsini mwake, maneno yake yanadhihirisha hilo.
Hata kama serikali na CCM watakususia jimbo bado usiogope kama ulikuja duniani kuwatumikia watu basi utawatumikia tu hata pasipo na chama chochote, amini unaweza!! Usife moyo ifanye kazi uliyoia pasipo na hofu wala mashaka!!
 
Filikunjombe ni mbunge makini anayejua majukumu yake, nini kilichompeleka bungeni na kuwakilisha kile alichotumwa na wananchi, anajua tofauti na mipaka ya ukada na ubunge ILA ASIBADILIKE TU!
 
Serikali ya ccm imevaa haedphone kubwa kubwa Kama za maDJ na miwani ya mbao, kwa hiyo haisikii wala haioni ukweli halisi wa maisha.
 
Yule jamaa ni jembe sio siri. CCM lazima watampiga chini awamu ijayo

Ni kweli kabisa 2015 hawatakuwa nae, maana hawapendi kuambiwa ukweli, tuona jinsi wabunge wa CCM walivyogeuka na kuwa sehemu ya serikali badala ya kuisimamia serikali.
 
Pole sana myawe! I can understand you really well. Jamaa wamekushika vibaya sana; nakuona kabisa unavyofanya yote haya kinyume kabisa na matakwa ya nafsi yako, lakini utafanyeje sasa!! Najua unatamani kukaa kimya kabisa uendelee na mambo yako lakini makubaliano hayaruhusu. What a shame, you've got to go out there regularly and make yourself heard loud, much as your heart would refuse! Vakwiyibete fivi muno muyawe veve!
Bela longee lunofu,
Amaligo igo si manofu ha!
 
Back
Top Bottom