Kuna yule kijana mchoraji, alikuwa na jitahidi kujieleza, kuna wakati alisema kuwa moja ndege iliwahi kukamatwa na silaha na hii habari ilikuwa kwenye vyombo vya habari Tanzania , je ni kweli?
Japo baadae ilikuja kugundulika yule muuandaaji, alikuwa anawalipa hela ili waiigize anavyotaka, baada ya uchambuzi uliochakachuliwa na baadhi ya waandishi wa habari wa nchi tofauti duniani kuona alikuwa na dhamira ya kuharibu taswira yote pamoja na biashara ya minofu ya samaki.
Kwa kuwa aliiona inaiingilia na uuzaji wa silaha harumu ambazo zilikuwa zinaenda Congo DRC, au alikuwa na nia ya kujaribu kuongelea biashara ya silaha, lakini ili apate urahisi wa kibali cha kutengeneza hio filamu, akaaingiza biashara ya minofu ya samaki kama cover stori, bila yeye kujua athari iliyoleta kwa wananchi wa Mwanza kwa kuharibu biashara ya minofu ya sangara.
Na pia hata jina la filamu, lilichakachuliwa na lilikusudiwa ili kujenga mzuka kwa wazungu kuwa na shauku ya kujua hii filamu inahusu nini...
Pia kuingiza maisha ya watoto wa mtaani na madada poa, ilileta maswali mengi kwa nia yake ya hii filamu.
Japo kulikuwa na ukweli fulani labda kwenye biashara ya silaha, maana sio kwa mindege ile na kasi ya kuingia na kutua iliyoamsha shamrashamra katika mji wa Mwanza...