Filamu ya Kiswahili, Jina la Kiingereza....

Mkuu acha masihara.
Zaidi ya asilimia 90 ya filamu za kibongo ni majina ya kizungu.

Sio filamu tu.Karibu kila kitu tunapenda majina hayo.Kwa mfano kwa sasa kuna wimbi la kuanzishwa makanisa.Na mengi yana majina ua kizungu( power of god,miracles church,victory,holliness n.k)Lakini ibada zao zote ni za kiswahili na usikute hata waumini wanaojua English labda wapo 2 tu.Hivyo hii ni kasumba tu ya sisi watanzania kwa vile tumeibukia sana kiingereza na maneno mengi pia tunayatumia moja kwa moja bila kujali pronunciation.
 
Wadau, soko la filamu linakuwa kila siku hapa nyumbani. Lakini je, kuna ulazima wa watengeneza filamu hizi kuziita majina ya Kiingereza ili hali ndani wanazungumza kiswahili mwanzo mpaka mwisho?

Naamini katika baadhi ya filamu wanachanganya lugha (Kiswahili na Kiingereza). Hiyo inaonyesha bidii ya kutaka kuitangaza zaidi filamu ieleweke kwa wasiojua kiswahili na pia inawasaidia kupata experience kuongea kiingereza. Jamani wanajitahidi, kwani mwanzo hawakuwa hivi. Filamu zao nyingi hivi sasa zinaburudisha. Kidogo kidogo watapiga hatua. Ila michango kama hii ya kuboresha zaidi filamu zao ni muhimu.

Hongereni sana The Great na The Greatest!
 
Naamini katika baadhi ya filamu wanachanganya lugha (Kiswahili na Kiingereza). Hiyo inaonyesha bidii ya kutaka kuitangaza zaidi filamu ieleweke kwa wasiojua kiswahili na pia inawasaidia kupata experience kuongea kiingereza. Jamani wanajitahidi, kwani mwanzo hawakuwa hivi. Filamu zao nyingi hivi sasa zinaburudisha. Kidogo kidogo watapiga hatua. Ila michango kama hii ya kuboresha zaidi filamu zao ni muhimu.

Hongereni sana The Great na The Greatest!

Mawazo yako ni "a big joke" and a bad one. Kutangaza movie siyo lazima kuchanganya tena ni makosa. Movie zote ama inakuwa katika lugha yake iwe ni Kihindi, Kichina, Kijerumani na nyingine nyingi kama kuna umuhimu unaweka subtitle kwa lugha sahihi siyo direct translation. Mtu hawezi kuelewa movie kwa kuchomekewa lugha zingine hapa na pale.
 
Mi nadhani waamue moja. Kiingereza mwanzo hadi mwisho au kiswahili mwanzo hadi mwisho!
 
Kuna filamu yoyote Tanzania iliyoigizwa na vijana wa kitanzania kwa kiingereza?? any filam please, nahitaji msaada
 
Diversion of love, dangerous desire, fake pastors, village pastors, yellow banana - hii sijui ilimaanisha nini coz yaliyomo ni tofauti na title yenyewe... Nafikiri mbonea ataje nyengine...

1. Diversion of love = mchepuko wa mapenzi
2. Dangerous desire= Hamu ya hatari
3. Fake Pastors = Mchungaji aliyeghushiwa
4. Village Pastor = Mchungaji wa kijijini
5. Yellow Banana = Ndizi ya njano

Kwa kweli watu wasingenunua hata sinema moja nadhani wanachagua majina ili kuuza sinema
 
Girl friend, Best friend, In the house na Lovely Gamble inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni kwa mujibu wa Asha Baraka wa ASET

Girl friend = rafiki wa kike
Best friend= rafiki bora
Lovely gamble= Kamali inayopendeza

mbona ingechekesha
 
Market selectivity: Filamu hizi zimetengenezwa mahususi kwa hadhara ya uswahilini,basic knowledge and those with incessant flat effect.

No offense,or is there?
 
Muigizaji, editor, floor manager ndiye huyo huyo, filamu hiyo itakuwa na ubora ganii?

Na ile tafsiri ya kiswahili kwenda kiingereza haieleweki kabisa kwa mtu asiyejua kiswahili. Na hadithi ndio hizo hizo mapenzi, mapenzi, mapenzi hakuna ubunifu.

Angalau wajitahidi kutafuta mwenye utaalamu wa kiingereza ili zile sentensi zieleweke.
 
Majina si Tatizo jamani, mimi shida kubwa ni kukopy baadhi ya michezo iliyochezwa kwa umahili na maprofessional Actors wa Abroad kisha kujifanya wao ndo wao kumbe wanaharibu. hahahaahahahahha tunga yako
 
eti danger zone part one and two! hawa waigizaji wetu bwana sio wala nn. si mnakkumbuka mmoja wao aliwahi kuwa kioja big brother!!!!!!!!!!!!! asa wengi wao ndo type hizo thats why wanakuwa sio creative.
 
Filamu ina title ya Kiingereza, waigizaji wanaongea kiswahili. Aibu ni pale kiswahili kinachoongelewa kinapotafsiriwa......mf. Tafuna eti inatafsiriwa Cut...aibu, hivi hakuna washauri au baraza la filamu haliyaoni haya makosa.

Ni kweli, subtitle ndo zinatia kichefuchefu.
 
Labda wanamuiga shigongo, kitabu/hadithi jina la kiingereza, ndani kiswahili kitupu
 
Back
Top Bottom