Kwa wale walioiona hii movie vipi ni nzuri? Na inahusu nini?
View attachment 1445539
...Hawakupenda udhalimu uliofanywa na watu weupe kwa watu weusi..rangi zao nyeupe zikapishana lugha na weupe wenzao..wakaamua kuingia mtaani kumwaga karatasi za haki..ni karatasi hizo ndizo zilizowapeleka jela.
Yess..makao ya utetezi wao ikawa ni ndani ya jumba lenye kila aina ya unyama...askari wenye miili yenye roho za wadudu...na maisha asiyostahili mwanadamu...wakakukubali ukweli,wakaamua kuuishi..
Lakini sio kwa Kim Jenkin.
Mhuni mweupe kati ya wale wawili walioingia Pretoria prison...mwili mdogo,macho yanayohitaji miwani na upole uliopitiliza..vyote hivo vilibebwa na kichwa adhimu chenye uwezo wa kufikiria maili milioni moja kwa dakika..ndio jenkin ni genius wa kizazi cha south africa.
Wakati bwana jela anaisifu jela yake kuwa na milango ya chuma 39...jenkin alikuwa anakiamini kichwa chake kuwa ni funguo ya kila geti lililosifiwa na kiongozi yule...jenkini ndo pritoria prison gates keys.
Miaka 12 aliyoambiwa alitumikie gereza. Alihitaji siku zisizozidi 360 kuuonesha ulimwengu kile kilichobebwa na kichwa chake.. ni akili za kiufundi zinazohitaji umakini uliopitliza...jenkin ni michael scofield wa mwaka 2020.
Kila alichoangalia jenkin ndani ya gereza kiliji save kwenye kichwa chake...alihitaji dakika 5 tu kuziangalia funguo za bwana jela kwenye kiuno...na asubuhi ya siku iliyofuata alikuwa na funguo yake ya mbao iliyotokana na fagio...ni jenkin genius.
Moja kati ya vitu vinavoifanya hii movie kuwa nzuri kwetu...ni kushuhudia plan za jenkin zikipangwa kupitia msumbiji kuja Tanzania...ndio
Jenkin na wafanya
Fujo wenzie wamechora ramani ya kuitamka tanzania kwa jina...wakiamini usalama wao ndani ya nchi yetu..mpaka kufika watapoenda.
Ni presha...ni fujo...ni akili na taharuki zitazokufanya ukae roho juu muda wote ukiamini kuna kitu kitafeli...kuna muda utatamani kumsaidia jenkin...na kuna muda utaamini jenkin haitaji msaada wako.. bali wewe ndo unahitaji kuwa jenkin kwenye maisha yako.
Je watafanikiwa?
ESCAPE FROM PRETORIA...2020...
C & P