Fikra za WanaJF na mfano wa Misri katika kuingoa Serikali Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fikra za WanaJF na mfano wa Misri katika kuingoa Serikali Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by apolycaripto, Feb 12, 2011.

 1. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Mara kwa mara kumekuwa na mifano mingi ya kuhamasisha wananchi (wafuasi wa vyama) katika nchi kuiga wenzetu wa Tunisia na Misri baada ya kutimua viongozi wao kongwe wasio na mihula ya utawala bali wao tu.Historia ya nchi hizi mbili za kiarabu ama mataifa ya kiarabu ni tofauti kabisa na Taifa la Tanzania.

  Mfano wa Misri chini ya Hosni Mubarak kama kiongozi asiye wa kuigwa hawezi kufananishwa na Kikwete.Mubaraka kwa kukaa madarakani kwa miongo mitatu mfululizo,amekumbana na yafuatayo yasiyo pendeza wala kukubalika na wanaMisri.

  1.Hakuwa mtu wa kukosolewa kutoka na nguvu za kijeshi na haiba yake ya kutotaka kupingwa.
  2.Ushirikiano wake Mkubwa na Taifa la Israel (kinafiki) pia ni vuguvugu kubwa la kuondoka kwake.
  3.Uswahiba wake na Marekani na kutokuwa na Ushirikiano bora na Umoja wa Nchi za kiarabu nacho ni kigezo kikuu cha kutokubalika kwake.
  4.Utawala wa yeye kutotaka Demokrasia ya ushindani ndani ya chama chake bali kuendelea kuwa yeye tu katika chaguzi zaidi ya tano ni udikteta ulikuwa haukubaliki.
  5.Dhamira yake ya kutokuonyesha kikomo cha kuondoka madarakani na pengine kufikiria kumrithisha mwanae kipenzi Gamal Mubarak.
  6.Udikteta wa kuhujumu demokrasia na kuweka ndani kwa njia za kilaghai washindani wake katika urais (mfano. Ayman Nour wa El-Ghad Party aliyeshindana nae katika uchaguzi wa 2005)

  Tabia na mwenendo wa Mubarak pengine ulifikia hatua ya kutishia uhai wake hasa baada ya kujikuta akinusurika na matukio mabaya zaidi ya sita ya kuuwawa hii ikihusisha vikundi vya kiislam pamoja na mahasimu wake.

  Hali ya chuki hasa juu ya mwenendo mzima wa utawala wake ilifikia kiasi cha kuwanyanyua waandamanaji haikuwaacha nyuma mahasimu wake kisiasa mbali na Muslim Brotherhood(kikundi chenye nguvu kubwa ndani ya Misri),Amr Moussa(Katibu Mkuu Umoja wa Nchi za Kiarabu,mzaliwa wa Misri) pamoja na Mohammed El Baradei(Aliyekuwa mkuu wa kitengo cha Ukaguzi wa Nuclear(IAEA) UN na mshindi wa Tuzo ya Nobel),kuungana na waandamanaji kuhakikisha Mubarak anang’ooka.Japo vuguvugu hili limeibuka kwa kasi baada ya wenzao wa Tunisia kufanikiwa kwa haraka kumnyofoa Ben Alli (miaka 23 madarakani).

  Dhamira ya Wamisri.

  Tunapaswa kufahamu kuwa mabadiliko ya kisiasa Misri haya kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa ajira,hali ngumu ya kimaisha bali sehemu kubwa ni udikteta ulionyima uhuru wa kisiasa,habari pamoja na Wananchi kuhitaji mabadiliko ya SURA kwani mbali na miaka 30 ya Urais,Mubarak amekuwepo serikalini toka miaka ya 70 kama Waziri wa Ulinzi na makamu wa Rais (Chini ya Anwar Saadat).Tutambuke kuwa mbali na yote katika nchi za kiarabu huwezi kudumu ama kutawala kwa amani iwapo muelekeo wa utawala wako unauswahiba na nchi za kimagharibi.Hapa tunaona ni jinsi gani Mubarak hakuwa na msimamo wa wazi juu ya suala la Palestina pamoja na kutokuwa na support ya kutosha pindi Umoja wa kiarabu unaoongozwa na Amr Moussa unapotoa matamko mbalimbali dhidi ya Marekani na Israel kwa niaba ya Nchi za Kiarabu.

  Dhana ya Waarabu wa Misri ama Tunisia kuwaondoa viongozi wao haiwezi hata kidogo kufananishwa na dhana na matatizo tuliyonayo Tanzania.

  Watanzania matatizo yetu hayako katika utawala wa kidikteta,kwani tumekuwa na fursa ya uhuru wa kisiasa,habari na mabadiliko ya uongozi hata kama yanatoka chama kimoja lakini kila awamu imekuwa na Rais wake toka Nyerere,Mwinyi,Mkapa na hatimaye Kikwete.Marais hawa kila mmoja amepita ama anapita na mazuri pamoja na mapungufu yake ambalo ni jambo la kawaida katika utendaji.Viongozi hawa wamekuwa wakipatikana kwa njia ya sanduku la kura,kupitia mchakato wa chama kwa maana ya wanachama kuwachagua katika hatua za awali na hatimaye ushindani wa vyama.Ushindi wao si wa kidikteta wa asilimia zaidi ya 90% (Mubarak,Sadam n.k) bali wamekuwa wakitofautiana kwa aidha kuanza kwa kushuka na kumalizia kwa kupanda kama ilivyokuwa kwa Mkapa(61.8% na 72%) na kinyume kwa Kikwete (82% na 61%).Kuyumba huku kwa matokeo ndio demokrasia ya kweli kwa maana wananchi wanaweza kukuongezea ama kukupunguzia ushindi.

  Msingi wa Matatizo yetu Watanzania.

  Watanzania tuna tatizo kubwa sana la ukosefu wa Maadili,hii ni tabia ambayo inakuwa siku hadi siku na sehemu kubwa inajengwa na utashi wa kiroho.Rushwa na matumizi yasiyo sahihi ya taaluma zetu hasa kwa watendaji mbali na wanasiasa ndicho chanzo cha kutuweka pabaya.

  Iwapo watendaji kwa maana ya Makatibu wakuu hadi ngazi za chini tungekuwa na maadili bora ya kizalendo na yanayozingatia taaluma zetu kamwe Wanasiasa wasingethubutu kuingiza ubinafsi wao.Mtu mwenye maadili bora,ujengwa na roho ya kutokuwa na uoga hivyo Wanasiasa wasingeweza kutuondoa wote katika nafasi zetu za kazi kwa sababu ya kutokubaliana nao.Hii ingekuwa fursa ya wazi kwa wao kuadhibiwa na Wananchi.

  Kutokuwa na maadili ndio kumetufikisha hapa leo kwenye giza(kutokuwa na watu wenye kufikiri mbele zaidi kabla ya tatizo ila maslahi binafsi),kushuka kwa elimu(mitaala isiyo eleweka(Mungai etal),maandalizi mabovu yasiyo na hofu(shule bila waalimu wala vifaa),ufisadi (kutoka juu mpaka chini ndani na nje ya serikali) n.k.

  Tunahitaji uthubutu hapa tulipofikia,hatuwezi kutegemea kazi kubwa kufanywa na mahakama bali ni wakati sasa kuanzia ngazi za chini kuwaondoa kwa nguvu wale wote wabadhilifu hasa katika Halmashauri ambazo moja kwa moja zinawajibika kwa wananchi kupitia madiwani.Funzo hili huko chini itakuwa fundisho kwa watendaji wa Serikali kuu (wachache) kuanza kushika nidhamu,huu utakuwa msaada bora kwa Rais aliyepo na atakaye kuepo.

  Hii ni badala ya kufikiri kuwa watanzania wanaweza kujikusanya mnazi mmoja na kuipinga serikali mpaka iondoke madarakani.Wakenya wako juu sana katika vuguvugu za kisiasa na hata katika usababishaji wa ghasia za kisiasa,lakini pamoja na Utawala mbaya na wa kiimla aliokuwa nao Mkongwe Moi,kamwe hawakuthubutu kuandamana mpaka Kasarani kumpinga mstaafu huyo mbali na miongo aliyokaa madarakani.

  Watanzania bado tunanafasi kubwa ya kupambana kitendaji badala ya kukalia siasa na majigambo ya vyama na Wanasiasa kila mahali nchini.Tukumbuke kuwa hakuna aliyekwisha “scan” na kuona usafi wa wanasiasa wetu,wawe wapya katika chama tawala ama vyama shindani.Pengine kelele zao uwenda ni kwa sababu hawajapata nafasi za kuwafanya kusahau maadili yao.Wanasiasa wamekuwa wakipewa dhamana ama kutwaa madaraka katika Nchi wakiwa wasafi na wenye kukubalika kwa watu ata akina Ben Ally na Mubarak lakini kadri muda unavyokwenda ubadilika na kuwa “wataka vitu” badala ya “watakatifu”.

  Hivyo kwa dhana hiyo,ata kama tutafikiri kuwa chama kingine mbadala kinaweza kuchukua dola hali ya kuwa mzizi unaotuangamiza (maadili) bado hujakatwa tutaishirizia kubadilisha vyama kila wakati na hatimaye nchi kuingia katika machafuko kutokana na urafi wa wanasiasa kama ilivyotokea Kenya (Kibaki na Raila) baada ya KANU kung’ooka.  Ndugu wanaJF haya ni mawazo yangu,nakaribisha changamoto zenye kuleta tija na wala si ushabiki wa kisiasa kwani mimi si Mwanasiasa wala shabiki wa chama cha siasa.Vile vile nashauri mchangiaji kusoma na kuelewa badala ya kuishia kwenye “heading” na kuanza “shambulizi”.
   
 2. Isaac

  Isaac JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 627
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  nice defence mechanism!
   
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mkuu karibu JF kuwa tayari kwa changamoto na uwe tayari kushambuliwa kama mpira wa kona karibu sana hii ni JF na huyo hapo juu ndio Isaac
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kweli km wewe sio makamu mwenyekiti bara pius msekwa basi wewe ni mtoto wake, au la mnafanana mawazo na akili, nae pia kwenye mdahalo wa katiba ulioandaliwa na itv alisema katiba haina tatizo, tatizo ni utekelezaji wake, kwamba tatizo ni watendaji ndani ya serikali lakini sio katiba. sijui hapo kuna tofauti gani na mawazo yako??? dont get me wrong.
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  asizungushe maneno,anadhani mifuko na matumbo ya wamisri yangekua vizuri nani angetaka kumuondoa.point ni moja tu maisha mabaya iwe Tunisia,misri au Tanzania.
   
 6. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #6
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  mkuu hujamuelewa isaac???
   
 7. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,924
  Likes Received: 12,127
  Trophy Points: 280
  Watu wa serikali mnajitahidi sana kutaka watu wasilinganishe matukio ya Misri, Tunisia na hali ya watanzania, mna hofu gani? Nasema hivyo kwa sababu siku kama mbili hivi limetokea wimbi la watu(members) likisema hayohayo. Kifupi ya Tunisia ya Misri na Algeria hayana tofauti na ya Tanzania ni maisha magumu period, wala usizungushe mpira eti sisi tuna demokrasia kwa vile tunafanya uchaguzi kila mwaka, uchaguzi my foot.

  Lakini kwa mada zenu mnazotoa zinaonyesha kiasi gani hili wimbi la mageuzi limewashtua na kuishtua serikali.
   
 8. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #8
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  well said mkuu!! ndo maana isaac akasema 'well defence mechanism"
   
 9. L

  LAT JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu...hofu lazima itawale kwani serikali kuu inahitaji complete overhaul from messanger to katibu mkuu hakuna jinsi... na hofu hii ipo sana tu
   
 10. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #10
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Tatizo lugha aliyoitumia imekuwa ngumu kwa msomaji wake heheheh JF raha sana lol
   
 11. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #11
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni uchambuzi sahihi kabisa! hongera mtoa mada! Kuna msemo usemao "IGIZA TEMBO PASUKA MTAMBA" TZ hatuna sababu yoyote ya kuigiza yanayotokea ktk nchi za Kiarabu! tofauti iliyoko ni kubwa sana kati yetu na wao!
   
 12. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45


  mtu wa system wewe,
  umetumwa kusoma upepo nini?mwambie tunajiandaa
   
 13. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #13
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa Zubeda sijui nikuete dada maana naona moyo wangu unasita, misri na Tanzania ni mbingu na ardhi watanzania ni wavumilivu sana na tutaendelea kuvumilia ila humu JF tutatukana sanaaaaa kwa majina bandia hii inaonyesha dhahiri hamna uthubutu! na hamtakuwa nao sembuse wa kusema mtaandamana kuitoa serikali madarakani? Acheni ndoto si mmemsikia Mwenyekiti wa CDM kamkubali JK kamwita Rais tena kasema "mheshimiwa Rais" nadhani tungoje tu tuangalie mchakato wa kurekebisha katiba na tusiwe sababu ya ndugu zetu wengine kupoteza maisha halafu baada ya wiki tatu anaechochea anapeana mkono na yule alietaka wananchi wamuone mbaya!
   
 14. T

  Topical JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Serikali yetu itatolwe kwa njia ballot box..2015, kama umeshindwa kufanya siasa kalime mashamba yako mengi ok

  Huwezi kulinganisha dicteta kama mubarak na rais mwana-demokrasia kama JK (unfair comparison)

  wananchi tunataka graduall changes ..overnight changes
   
 15. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #15
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kuandika mithread yenye manano mengi mimi haini saidii na wala sihitaji upupu huo .....sahizi mimi nipo gizani umeme umekatwa na kero nyingine kama vile kupanda bei ya vitu sokoni na shindwa hata kununua matunda.

  unadhani nitawapenda unadhani nitafikiria mnafanana au hamfanani na mwingine niukweli usio pingika kuwa siwezi kuwa penda kwasababu sielewi kodi mnayo chukua kwangu na wengine mna peleka wapi. nasasahivi nilvyo na hasira sana hata watoto wangu nimesha wafundisha wa kimwona mtu kavaa nguo za sisiemu wa teme mate chini maanayake ni mkosi mkubwa sana kukutana na watu kama hao
   
 16. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #16
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  <br />
  <br />
  Tatizo kweli ni ''maadili'' !!!!!! kama hayakuanzia nyumbani,mtu kukosa matunda anarithisha nidhamu mbovu kwa watoto,hii ni kazi kweli kweli!!
   
Loading...